Tafuta

Papa Francisko amemteua Askofu mkuu Giampiero Gloder kuwa Balozi mpya wa Vatica nchini Cuba. Papa Francisko amemteua Askofu mkuu Giampiero Gloder kuwa Balozi mpya wa Vatica nchini Cuba. 

Askofu mkuu Giampiero Gloder, ateuliwa kuwa Balozi nchini Cuba

Askofu mkuu Gloder alizaliwa kunako tarehe 15 Mei 1958. Akapadrishwa tarehe 4 Juni 1983. Kunako mwaka 1990 akajipatia shahada ya uzamili katika Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thoma wa Akwino. Na mwaka 1992 akatunukiwa shahada ya Uzamivu katika Mafundisho Sadikifu ya Kanisa. Mwaka 2013 akateuliwa na kuwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Giampiero Gloder, kuwa Balozi wa Vatican nchini Cuba. Kabla ya uteuzi huu Askofu mkuu Gloder alikuwa ni Rais wa Taasisi za Kipapa Kikanisa. Itakumbukwa kwamba, alizaliwa kunako tarehe 15 Mei 1958. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa tarehe 4 Juni 1983. Kunako mwaka 1990 akajipatia shahada ya uzamili katika Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thoma wa Akwino, Angelicum. Na mwaka 1992 akatunukiwa shahada ya Uzamivu katika Mafundisho Sadikifu ya Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, kilichoko mjini Roma.

Utafiti wake wa kisayansi ulijikita zaidi katika taalimungu mintarafu Mtakatifu Paulo VI. Askofu mkuu Giampiero Gloder alianza utume wake wa kidiplomasia mjini Vatican, tarehe 1 Julai 1992. Tangu wakati huo, akabahatika kutekeleza utume huu nchini Guatemala na Vatican. Baba Mtakatifu Francisko hapo tarehe 21 Septemba 2013, kuwa Balozi na Rais wa Baraza la Kipapa la Taasisi za Kikanisa. Tarehe 11 Oktoba 2019 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Cuba.

Balozi Cuba

 

12 October 2019, 14:03