Tafuta

Vatican News
Askofu mkuu Antoine Camilleri ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Ethiopia, Gjibouti, Mwakilishi Maalum wa Vatican kwenye Umoja wa Afrika na Msimamizi wa Kitume nchini Somalia. Askofu mkuu Antoine Camilleri ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Ethiopia, Gjibouti, Mwakilishi Maalum wa Vatican kwenye Umoja wa Afrika na Msimamizi wa Kitume nchini Somalia. 

Askofu mkuu Antoine Camilleri: Balozi: Ethiopia, Gjibouti na UA!

Askofu mkuu Antoine Camilleri alizaliwa mwaka 1965 huko Silema, nchini Malta. Akapewa Daraja ya Ukasisi tarehe 5 Julai 1991. Alijiunga na utume wa Diplomasia ya Kanisa mwaka 1999. Tarehe 22 Februari 2013 akateuliwa kuwa Katibu mkuu msaidizi mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa. Tarehe 2 Septemba akateuliwa kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 4 Oktoba 2019.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Antoine Camilleri kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ethiopia na Gjibouti. Atakuwa pia Mwakilishi Maalum wa Vatican kwenye Umoja wa Afrika na Mwakilishi wa Kitume nchini Somalia. Kabla ya uteuzi huu Askofu mkuu Antoine Camilleri alikuwa ni Katibu mkuu Msaidizi wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Antoine Camilleri alizaliwa tarehe 20 Agosti 1965 huko Silema, nchini Malta. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 5 Julai 1991 akapewa Daraja takatifu ya Upadre.

Baadaye akajiendeleza na hatimaye, akajipatia shahada ya uzamivu kwenye Sheria na taratibu za uendeshaji wa kesi Mahakamani. Askofu mkuu Antoine Camilleri alijiunga na utume wa kidiplomasia mjini Vatican kunako tarehe 9 Januari 1999. Tangu wakati huo, ametekeleza utume huu nchini New Papua Guinea, Uganda, Cuba na hatimaye, kwenye Kitengo cha mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Tarehe 22 Februari 2013 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Katibu mkuu msaidizi wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 3 Septemba 2019 akamteuwa kuwa Askofu na hatimaye kumweka wakfu tarehe 4 Oktoba 2019 kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Askofu Mkuu Antoine
31 October 2019, 12:59