Vatican News
Amteuliwa Askofu Mario Grech wa Jimbo katoliki la Gozo kisiwani Malta kuwa Katibu Mkuu mwambata wa Sinodi ya Maaskofu Amteuliwa Askofu Mario Grech wa Jimbo katoliki la Gozo kisiwani Malta kuwa Katibu Mkuu mwambata wa Sinodi ya Maaskofu 

Askofu Grech ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mwambata wa Sinodi ya Maaskofu!

Baba Mtakatifu Francisko ameteuwa Askofu Mario Grech wa Jimbo Katoliki la Gozo kisiwani Malta kuwa Katibu Mkuu mwambata wa Sinodi ya Maaskofu ambaye mara baada ya kung'atuka Kardinali Baldisseri atashika nafasi hiyo,kwa mujibu wa maelezo ya Kardinali Baldisseri aliyotoa kwa wandishi wa habari siku chache kabla ya kuanza Sinodi ya Maaskofu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Askofu Mario Grech, wa jimbo la kisiwa cha Malta ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Mwambata wa Sinodi ya Maaskofu ambaye atashirikiana na Kardinali Lorenzo Baldisseri, ambaye ni Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu. Hata hivyo ni Kardinali Baldisseri mwenyewe, aliyetangaza saa sita kamili tarehe 2 Oktoba  2019, siku chache kabla ya kuanza Sinodi kwa ajili ya Kanda ya Amazonia  inayotatajiwa kufunguliwa tarehe 6 Okotba 2019. Akizungumza na waandishi wa habari amesema Askofu Mario Grech, wa jimbo la  Gozo  pia ametangazwa kuwa Msimamizi wa Kitume katika jimbo hilo hilo hadi atakapoteuliwa Askofu  mwingine. Katibu Mkuu mwambata atabeba majukumu moja kwa moja akiwa karibu na Kardinali Baldisseri  ili kumfanya awe na uzoefu, utambuzi mzuri na washiriki wake na kupata  ufahamu wa michakato mbalimbali ya uendeshaji wa mikutano na  hali halisi ya ustadi wa kazi  ukatibu mkuu katika Sinodi.

Kardinali Baldisseri amesema, Askofu Grech atakamilisha ofisi yake  ya kuwa Katibu Mkuu wa Sinodi  hadi  hapo Yeye atakapo ng'atuka katika utumea wakati atakapo timiza miaka 80 kunako mwezi Septemba 2020. Aidha Kardinali Baldisseri amehitimisha kwamba, kutangazwa kwake kama Katibu mwambata wa Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu  pia atashiriki kama mjumbe katika Sinodi  ijayo itakayoanza  tarehe 6 Oktoba 2019. Askofu Grech alizaliwa tarehe 20 Februari 1957 huko  Qala. Askofu Grech alipewa daraja la Upadre kunako mwaka 1984 na kutangazwa kuwa Askofu wa jimbo la Gozo huko Malta, kunako Novemba 2015 na Baba Mtakatifu benedikto XVI.

02 October 2019, 14:05