Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu Paglia yuko Marekani katika mfululizo wa mikutano ambapo ni katika harakati za maandalizi ya Mkutano mkuu wa 2020 utakaohusu mada ya akili bandia kwa viboresho vya Microsoft Askofu Mkuu Paglia yuko Marekani katika mfululizo wa mikutano ambapo ni katika harakati za maandalizi ya Mkutano mkuu wa 2020 utakaohusu mada ya akili bandia kwa viboresho vya Microsoft 

Ziara Ask.Mkuu Paglia nchini Marekani katika harakati za maandalizi ya Mkutano Mkuu 2020!

Katika harakati za kuandaa Mkutano Mkuu ujao 2020 wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha,Askofu Mkuu Paglia yuko Marekani.Katika fursa ya ziara hiyo ni kukutana na wakuu mbalimbali wa taasisi na pia atakutana na Rais wa Microsoft,Bwana Brad Smith.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Askofu mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha na Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Ndoa na Familia ya Yohane Paulo II, yuko ziara nchini Marekani. Katika ziara hii inajikita katika maandalizi ya Mkutano mkuu wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Februari 2020 kwa kuongozwa na mada ya Akili bandia na yenye viboreshaji kama Microsoft na IBM.  Na kazi ya mkutano wa mwaka 2019 ulikuwa unaunganisha pamoja  na vodokezo vya kutazama  mkutano huo wa kimataifa wa mwaka 2020 kuhusu akili bandia  na ambapo, mantiki hizi mbili za roboti na akili bandia zinatofautiana, lakini wakati huo huo zinaunganika pamoja kwa sababu ya kushirikishana mantiki ya maendeleo ya kiteknolojia na matumizi ya maadili.

Akiwa Marekani, Askofu Mkuu tarehe 3 Septemba amekutana  na wanafunzi na maprofesa wa Chuo Kikuu cha Loyola huko Marymount (Los Angeles kwa kutoa mada kuhusu Elimu ya viumbe kwa ujumbe kwa ujumla, ambapo amegusia mada alizojikita nazo Baba Mtakatifu Francisko katika Barua ya Humana Communitas iliyotangazwa na mwezi Januari katika fursa ya miaka 25 tangu kuundwa kwa taasisi hiyo. Katika mantiki hiyo Baba Mtakatifu Francisko alitoa ufafanuzi wazi juu ya umuhimu wa kukabiliana na changamoto ambazo hazijawahi kutolewa majibu yake na teknolojia za leo,zinazoibuka na dharura zake au na kubadili teknolojia, habari za mawasiliano na roboti. Kufuatia na fursa ya matokeo yaliyo patikana kutoka na  fizikia, na sayansi inawezekana kuingilia kati kwa kina katika maisha ya mwanadamu. Hata hivyo mwili wa binadamu unahusika na hatua hizo ambazo zinaweza kubadilika na siyo tu kazi na utendaji wake, lakini pia hali za uhusiano, kwa ngazi binafsi na kijamii (Humana Communitas, 12). Huko Marymount, katika  Chuo Kikuu cha Loyola  Askofu Mkuu Paglia amewakilishwa kwa  wanafunzi na Profesa Roberto Dell’Oro, ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha Bioethics na Taaasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha.

Ratiba ya ziara yake pia inaonesha kuwa tarehe 5 Septemba, huko Redmomd, Askofu Mkuu Paglia atakiungana na Wanataasisi Padre  Paolo Benanti na Padre  Carlo Casalone; pia Monsinyo Lucio Ruiz, Katibu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Vatican na Padre  Andrea Ciucci mratibu wa Askofu Mkuu Paglia  kwa kuudhuria mfululizo wa mikutano na wakurugenzi tofauti wa maeneo ya maedeleo na utafiti wa Microsoft  juu ya mada ya akili bandia na faida ya pamoja. Mchana Askofu Mkuu Paglia atakutana na Rais wa Microsoft, Bwana Brad Smith, kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano mkuu wa mwaka 2020 wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha ambapo Rais  Smith alikubali ushiriki huo. Mkutano wa tarehe 5 Septemba ni mwendelezo wa ziara iliyofanywa jijini Vatican na Rais wa Macrosoft  Bwana Simith, tarehe 13 Februari 2019. Katika fursa hiyo, alizungmza na Askofu Mkuu Paglia na baadaye kukutana na Baba Mtakatifu Francisko. Katika mkutano huo Bwana Smith aliafikiana na kuthibitisha juu ya kuingilia kati akiwa na shauku na jihatada ya Microsoft kuelekea katika  maswala ya mada ya  maadili inayohusiana na maendeleo ya Akili bandia na umakini wa mada za kimaadili.

Tarehe 8 Septemba Uwakilishi wa Taasisi ya kipapa kwa ajili ya Maisha, watakwenda New York kukutana kwa siku mbili na wakuu wa IBM. Tarehe 9 Septemba watakabiliana na mada ya maadili katika nyakati za akili bandia huku wakizungumza na wahusika wa mpango wa elimu na mafunzo kwa ajili ya kizazi kipya  ambacho kinajihusisha na wanafunzi kutoka nchi 18, huko Brooklyn jijini  New York. Siku itakayofuata ratiba ya kazi yao inatazama kutembelea Kituo cha Utafiti cha «Thomas J. Watson» huko Yorktown Heights, ili kujadili uvumbuzi, jukumu la akili ya bandia na usimamizi wa data, kulingana na kanuni za IBM katika matumizi ya teknolojia mpya. Mkutano huo utaongozwa na John E. Kelly, makamu  rais mtendaji wa Ibm, Mkurugenzi wa eneo la Utafiti Bwana  Dario Gil na Afisa wa Siri, Bi,  Christina Montgomery. Hata hivyo  Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha imewaalika IBM kutuma wawakilishi wake katika Mkutano Mkuu kwa mwaka 2020!

04 September 2019, 10:39