Tafuta

Vatican News
Huduma za tiba shufaa (palliative care) inahitaji mshikamano wa kila mtu katika kuwasindikiza wagonjwa wote ambao hawawezi kupona na hata wazee Huduma za tiba shufaa (palliative care) inahitaji mshikamano wa kila mtu katika kuwasindikiza wagonjwa wote ambao hawawezi kupona na hata wazee 

Taasisi ya Kipapa ya Maisha kukabiliana na huduma za tiba shufaa!

Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha na Mkutano wa ubunifu wa afya Kimataifa huko Qatar wameandaa Kongamano la siku mbili kuanzia tarehe 11-12 Desemba 2019 ili kukabiliana na maada ya“Dini na maadili ya matibabu:huduma za tiba shufaa na afya ya akili ya wazee”,katika dunia ya wakristo na waislam.Kwa maana hii,jukumu muhimu la msaada wa kiroho litasisitizwa,kwa kuheshimu tofauti za kidini,katika utunzaji unaowahusu hata wauguzi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuanzia tarehe 11 hadi 12 Desemba 2019 litafanyika mjini Roma Kongamano la Kimataifa  ambalo litakaloongozwa na mada ya  “Dini na maadili ya matibabu: huduma za tiba shufaa ya afya ya akili ya wazee”. Ni Kongamano ambalo limeandaliwa na  Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha (PAV wakishirikiana na Mkutano wa Kimaifa wa  ubunifu wa afya (Wish) ambao ni mpango ulioanzishwa na Chama cha Qatar. Katika siku ya kwanza ya kazi ya Kongamano hilo, itaanza na suala kuhusu huduma za tiba shufaa (Palliative care).

Katika kazi hiyo waweza kuwakilisha hali halisi iliyopo huko Qatar na Kanda ya Ghuba hiyo, ambapo watajadiliana na kupanuana mawazo  zaidi juu ya njia zinazo tumika katika nchi za Magharibi. Vikao vingine tofauti vya siku vitajadili mada za mafunzo na mapungufu ambayo yanatakiwa kutulizwa, aidha watajifunza njia za kukabiliana na  changamoto za kimaadili na ambazo zinaingiliana na huduma za tiba shufaa (palliative care) na njia ya kibaiolojia kulingana na  imani tofauti za kidini. Kwa ufafanuzi zaidi katika Kongamano hili wataangazia mambo ya pamoja kati ya ulimwengu wa Kiislamu na Kikristo juu ya mada ya huduma za tiba shufaa(palliative care) na ili kufikia njia bora ya huduma ya matibabu. Kwa maana hii, jukumu muhimu la msaada wa kiroho litasisitizwa, kwa kuheshimu  tofauti za kidini, katika utunzaji unaowahusu wauguzi.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kipapa ya Maisha wanafafanua zaidi kwamba, siku ya pili, itajikita katika mada ya afya ya akili ya wazee. Kutokana na hilo watoa mada mbali mbali wataonyesha uwezo uliopo wa dini na hali ya kiroho kwa ujumla, katika kazi ya kukuza ustawi na maisha bora kwa wazee wagonjwa. Mada nyingine zinazotajiwa katika siku hizo mbili zinahusu utunzaji wa watoto wachanga na wazee kujiua. Rais wa Taasisi ya Kipapa ya Maisha (Pav) Askofu Mkuu, Vincenzo Paglia, katika maandalizi haya ameelezea kwamba  huduma ya tiba shufaa na afya ya akili ya wazee ni mada mbili maalum zenye kupendekezwa na Taasisi hiyo na kwamba, mazungumzo na ulimwengu wa Kiislam hunajibu jukumu maalum walilopewa  na Baba Mtakatifu Francisko.

Huduma za tiba shufaa maana yake ni nini? (Palliative care): Huduma za tiba shufaa linatokana na neno la lugha ya kilatino  ambapo ni kufunikwa kwa vazi, na kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, wanaona kwamba neno hilo linafaa na  ni njia bora inayolenga kuboresha zaidi maisha ya watu walioathiriwa na magonjwa ambayo hayawezi kutibika na familia zao kwa njia ya kuzuia na kutuliza kutokana na mateso, na zaidi kupitia kutambuliwa mapema na matibabu bora ya maumivu na shida nyingine asili za mwili, kisaikolojia na kiroho (taz, World Health Organization, National cancer control programmes. Policies and managerial guidelines, 2002, p. 84).Huduma shufaa ni utaratibu wa jumla unaokusudia kuboresha maisha ya wagonjwa na familia zinazokabiliwa na matatizo ya maradhi yanayohatarisha uhai. Ni huduma inayomhusisha mgonjwa na familia, inayotegemea ushirikiano kati ya watoa huduma, wagonjwa na familia zao. Utoaji wa huduma hii huanzia pale ubainishaji wa ugonjwa unapofanyika, kifo kinapotokea pamoja na maombolezo, pia matakwa na thamani ya utu wa mtu vinaheshimiwa kwa kiwango kikubwa kadiri inavyowezekana.

Huduma shufaa inampa mgonjwa tumaini la kuendelea kuishi na kuchukulia kifo kama mchakato wa kawaida wakati huo huo inawezesha tathmini sahihi na matibabu mwafaka ya maumivu na matatizo mengine, ikiwa ni pamoja na matatizo ya kimwili, kisaikolojia, kijamii, lishe au kiroho. Aina nyingi za huduma shufaa huanza kutolewa mapema katika kudhibiti mwenendo wa ugonjwa hatari. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO huduma za tiba shufaa ni utaratibu wa matibabu unaoboresha ubora wa maisha ya mgonjwa na familia iliyo katika matatizo yatokanayo na kuuguliwa kwa kuzuia na kupunguza matatizo katika maana ya kutambua mapema dalili za tatizo na namna ya kuhakiki tatizo na kutuliza maumivu na matatizo mengine ya kimwili, kijamii, kiakili na kiroho kwa wagonjwa wenye magonjwa sugu. Kupitia tiba hiyo, mtoa huduma anapaswa kumtembelea mgonjwa nyumbani kwa ajili ya matibabu ya mara kwa mara huku akisaidia kuwapa ushauri wanaomuuguza mgonjwa huyo

Sheria ya 38 ya tarehe 15 Machi 2010 inalinda haki ya raia kuweza kupata huduma ya utunzaji mbadala wa afya (Palliative Care) na matibabu ya maumivu. Huduma shufaa( palliative care ) lakini pia ni pamoja na ile ya kutumia madawa ya kutuliza tu kwa kina, ambayo hufafanuliwa na sheria kama seti nzima ya hatua za matibabu, utambuzi na msaada, unaolenga mgonjwa na familia yake, kwa lengo la utunzaji kamili na ukamili wa wagonjwa ambao unaonyeshwa na maendeleo yasiyoweza kuzuiwa, na ugonjwa mbao hawezi kujibu tena matibabu maalum. Lakini wahusika wa haki hii ni wagonjwa wote na siyo tu wale wanaosumbuliwa na ugonjwa ambao hautibiwi na mbao lakini pekee yake wanaweza kutumia hata dawa ya kutuliza tu kwa kina, kwa mujibu wa maelekezo ya kisheria.

13 September 2019, 15:55