Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko akutana na Rais Aleksandar Vučić, wa Serbia na ujumbe wake. Baba Mtakatifu Francisko akutana na Rais Aleksandar Vučić, wa Serbia na ujumbe wake.  (Vatican Media)

Rais wa Serbia akutana na Papa Francisko mjini Vatican

Papa Francisko pamoja na Rais Aleksandar Vučić katika mazungumzo yao, wamezama zaidi katika hali halisi ya Serbia, ambayo imekwisha kupiga hatua kubwa katika mchakato wa kuingizwa kwenye Umoja wa Ulaya. Baadaye, wamegusia pia masuala ya kikanda, kwa kukazia zaidi umoja na ushirikiano wa kimataifa ili kujenga na kudumisha amani pamoja na kuthamini mchango wa dini.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 12 Septemba 2019 amekutana na kuzungumza na Rais Aleksandar Vučić wa Serbia pamoja na ujumbe wake. Baadaye Rais Aleksandar Vučić amebahatika kuzungumza pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher. Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu Francisko na mgeni wake, wameridhishwa na uhusiano mwema uliopo kati ya Vatican na Serbia pamoja na kushukuru kwa dhati kabisa mchango unaotolewa na Kanisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya wananchi wa Serbia, hususan katika sekta ya maendeleo fungamani ya binadamu.

Baba Mtakatifu Francisko pamoja na Rais Aleksandar Vučić  katika mazungumzo yao, wamezama zaidi katika hali halisi ya Serbia, ambayo imekwisha kupiga hatua kubwa katika mchakato wa kuingizwa kwenye Umoja wa Ulaya. Baadaye, wamegusia pia masuala ya kikanda, kwa kukazia zaidi umoja na ushirikiano wa kimataifa ili kujenga na kudumisha amani pamoja na kutambua mchango chanya unaoweza kutolewa na dini mbali mbali katika mchakato wa upatanisho wa kitaifa.

Rais wa Serbia

 

13 September 2019, 15:29