Tafuta

Vatican News
Picha ya pamoja ya Makardinali sita washauri wa Papa na makatibu wakiwa pamoja na Patriaki Bartholomeo I mara baada ya kusalimiana na kuzungumza nao Picha ya pamoja ya Makardinali sita washauri wa Papa na makatibu wakiwa pamoja na Patriaki Bartholomeo I mara baada ya kusalimiana na kuzungumza nao 

Papa akutana na Patriaki Bartholomeo I mjini Vatican!

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 17 Septemba 2019 amekutana mjini Vatican na Patriaki Bartholomeo I.Kwa mujibu wa msemaji Mkuu wa Vatican Bwana Matteo Bruni anathibitisha kuwa mkutano wao ilifanyika katika hali ya kidugu, na wakati huo huo patriaki amepata kusalimiana na wajumbe wa Baraza la Makardinali 6 washauri wa Papa wakiwa na makatibu wao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na Patriaki Barthomoleo I ambapio katika mkutano wao  pia wamebadilishana zawadi, baadaye ikafuatia  chakula cha mchana kwa pamoja na wawakilishi wake katika nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 17 Septemba 2019. Kabla ya mkutano huo, kwa mwaliko wa Askofu Semeraro, anbaye ni Katibu wa Baraza la Makardinali, Patriaki amewasalimia kwanza wajumbe wa Baraza la Makardinali ambao wameanza Mkutano wao kuanzia tarehe 17 hadi 19 Septemba. Katika mazungumzo nao amesisitizia juu ya thamani ya mikutano ya Kanisa la Kiorthodox,  na zaidi kuwahakikishia uwepo karibu nao katika sala zake.

Hata hivyo kwa mujibu wa msemaji mkuu wa Vatican ni kwamba  kabla ya mkutano wa siku hiyo, Baba Mtakatifu Francisko alikuwa amemtumia barua Patriaki. Katika barua hiyo, Baba Mtakatifu ameweka bayana maana ya zawadi ya hivi karibuni ya baadhi ya masalia matakatifu ya Mtakatifu Petro kwa Kanisa la Constantinopoli, na ambayo kwa sasa yamewekwa karibu na masalia ya  Mtakatifu Andrea.  Hii ni kutaka kuthibitisha kwamba chombo kinacho tunza masalia  aliyuo mzawadia Patriaki wa Costantinopoli, ndani mwake kuna aina tisa za mifupa ya Mtakatifu Petro, na ambayo ni sehemu ya mifupa iliyo kuwa imetunzwa katika kifaa maalum jijini Vatican.

18 September 2019, 12:11