Kunahitajika uhamasishwaji wa urafiki,kati ya sekta za Serikali,binafsi,taasisi za elimu,mitandao ya kijamii na jamii yote ili kutokomeza biashara ya binadamu na kuwasaidia waathiri Kunahitajika uhamasishwaji wa urafiki,kati ya sekta za Serikali,binafsi,taasisi za elimu,mitandao ya kijamii na jamii yote ili kutokomeza biashara ya binadamu na kuwasaidia waathiri 

Kard.Parolin:wekeni mikakati madhubuti ya kufuta biashara ya binadamu duniani!

Katika kikao cha tarehe 26 Septemba 2019 huko New York Marekani,Kardinlai Parolin Katibu wa Vatican akihutubia amewataka wajumbe wa Umoja wa Mataifa kuweka mikakati itakayofutilia mbali biashara ya binadamu duniani.Kuna hitaji la jamii ya watoto inayofanya takribani,theruthi mbili ya idadi ya raia wote,misaada tofauti ya kimalezi na ki-afya!

Na Padre Angelo Shikombe, - Vatican

Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican na mwakilishi wa Mamlaka ya kipapa katika mkutano wa 74 wa Umoja wa Mataifa, kwa kitengo cha Mawaziri wa Jumuhuri ya Afrika ya Kati, uliofanyika mnamo tarehe 26 Septemba 2019 huko New York Marekani, amewataka wajumbe wa Umoja wa Mataifa kuweka mikakati itakayofutilia mbali biashara ya binadamu ulimwenguni.

Huku akiwapongeza wajumbe wa baraza la Umoja wa Mataifa kwa kusimamia mkakati uliosababisha kupunguza vitendo vya kiharifu katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Kardinali Pietro Parolin amesema, jukumu kubwa linalolikabili Baraza la Umoja wa Mataifa ni kusimamia chaguzi za desemba 2020 na 2021 ili ziweze kuwa za haki na kidemokrasia. Jukumu hilo ni pamoja na kuwalinda wawakilishi wa haki za binadamu kwa sharia za kimataifa.

Kardinali Pietro Parolin amebaini pia hitaji la jamii ya watoto inayofanya takribani, theruthi mbili ya idadi ya raia wote, wanahitaji misaada mbalimbali ya kimalezi na ki-afya. Pamoja na Vatican kujihusisha kila mara katika kutatua tatizo hilo, lakini inazidi kutoa mwaliko wa kushirikiano zaidi na zaidi.

Akisisitiza juu ya hoja hiyo, Kardinali Parolin amesema kuwa kunahitajika uhamasishwaji wa urafiki, kati ya sekta za Serikal, sekta binafsi, taasisi za elimu, mitandao ya kijamii, na jamii yote katika kutokomeza biashara ya binadamu na kuwasaidia waathirika wa nyanyaso hizo. Akiyataja jumuiya zinazoshirikiana na Kanisa Katoliki katika kupambana na vita hiyo amesema, Jumuiya ya Mtakatifu Marta na Jumuiya ya Talitha Kum. Pia kitengo cha kupambana na biashara ya binadamu nchini Vatican kimechapisha miongozo ya maendeleo fungamano ya miongozo ya kichungaji ili kuimarisha jitihada ambazo zinachukuliwa na Kanisa. 

Kardinali Parolin amesisitiza kuwa, namna ya pekee ya kupambana na biashara ya binadamu ni ni kuhamasisha udugu, mshikamano na uwajibikaji. Mbinu hizi zinaweza kusaidia kuondoa sintofahamu inayosababishwa na mtandao wa biashara ya binadamu. Hatimaye amewaomba kuyaishi matamko wanayojiwekea kila wakutanapo. 

26 September 2019, 13:50