Vatican News
Waandamanaji mbele ya Bunge la Quito nchini Equador wakipinga maoni ya kutaka kupitishwa mswada wa sheria ya utoaji mimba. Waandamanaji mbele ya Bunge la Quito nchini Equador wakipinga maoni ya kutaka kupitishwa mswada wa sheria ya utoaji mimba.  

Ecuador:Jibu la Bunge nchini Ecuador ni hakuna ruhusa ya utoaji!

Askofu mkuu Alfredo José Espinoza Mateus wa Jimbo kuu Katoliki la Quito,nchini Ecuador amesema,mwaliko ulitolewa na Baraza la Maaskofu nchini humo,siku za karibuni ukiwataka wabunge kutafakari kwa makini juu ya sheria ya utoaji mimba sasa umepata jibu la 'hapana ruhusa ya utoaji mimba'.

Na Padre Angelo Shikombe - Vatican

Mwaliko wa Kanisa Katoliki katika kutetea haki za watoto na kupinga utoaji mimba umetekelezwa na bunge la Ecuador barani Amerika ya Kusini. Askofu mkuu Alfredo José Espinoza Mateus wa Jimbo kuu katoliki la Quito, Ecuador  amesema, mwaliko huo ulitolewa na Baraza la Maaskofu nchini humo, siku za karibuni ukiwataka wabunge kutafakari kwa makini juu ya sheria ya utoaji  mimba ambayo haijatambuliwa na Katiba ya nchi hiyo na badala yake wazingatie haki za kulinda wasio na hatia, au uwezo wa kujitetea wenyewe, na wanaosongwa na changamoto ya kuawawa kabla ya kuzaliwa kwao.

Mafanikio hayo makubwa ya nchi ya Ecuador ni mfano wa kuigwa kwa nchi mbalimbali ulimwenguni. Na hii ni kwamba  utoaji mimba hautakuja kukubaliwa kisheria. Maamuzi hayo ya mefikiwa katika mkutano wa kitaifa unaoelezea bunge kuwa umepitisha vifungu saba na maelekezo yake katika vipengere 65 ambavyo vimepigiwa kura ya ndiyo juu ya kukataa mswaada wa sheria ya utoaji mimba. Takribani wabunge 71 walipiga kura ya kupinga mswaada huo na wabunge 59 walipiga kura ya ndiyo kwa mswaada huo.

Askofu Mkuu  José Alfredo Espinoza Mateus, wa Jimbo la Quito akieleza hisia zake amesema, Kanisa Katoliki likiwa katika furaha ya kuona haki za watoto na wanyonge zinazingatiwa linaridhika na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Bunge katika kulinda haki za watoto hususani katika harakati za kupinga vitendo vya utoaji mimba. Hata hivyo bado Kanisa linatambua kazi iliyoko mbele kuwa ni pevu hasa katika sekta za elimu, afya na utamaduni katika kuwasaidia akinamama.  Askofu mkuu Espinoza Mateus, akielezea mapendekezo ya sheria hiyo ambayo yanatokana na mijadala mipana iliyofanyika siku za karibuni amesesisitiza kuwa udhibiti wa utoaji mimba hapo mwanzoni ulilinganishwa na ukatili kwa akina mama lakini siyo hivyo, bali ni kujali haki za mama na mtoto bila kumbagua yeyote. 

Katika kufikia hatua hii kubwa bungeni, watu wanapaswa kumshukuru Mungu na kuendelea kumwomba ili kufikia ukamilifu wa haki zake kwa wote. Askofu mkuu Spinoza ameendelea kusema kuwa Kanisa limefanya kazi kubwa katika kuhamasisha wananchi na wabunge likitoa elimu juu ya madhara ya kuwaua viumbe wasio na hatia na wasio na uwezo wa kujitetea wenyewe. Katika hali hiyo Kanisa limesali kumwomba Mungu awaguse wanahusika na utunzi wa sheria ili kuliokoa taifa katika janga hilo.  Kama Baraza la maaskofu Katoliki lilivyolivalia njuga suala hilo ndivyo bunge limetambua wajibu wake wa kusimamia haki za wanyonge. Ikumbukwe kuwa nchi hiyo ina idadi ya wakristo takribani 80% ya idadi ya watu wote. Utume wa Kanisa daima utajipambanua katika kulinda haki za wanyonge ha kupanda mbegu ya matumaini. Hata hivyo Kanisa linaendelea kutambua kuwa kazi iliyoko mbele ni kubwa ya kuendelea kulelimisha na kupambana na mila potofu sinasosigina haki za wanyonge na kuweka mikakati madhubuti ya kuwafanya watoto wayafurahie maisha yao na kujiandalia maisha yao ya badaye.

Ikumbukwe hivi karibuni Maaskofu nchini Ecuador walitoa wito kwa waamini ili kuomba, kutafakari na kushiriki kikamilifu katika matendo ya dhati ya utetezi wa maisha hai ya mwanadamu, kufuatia na matazamio ya mjadala wa bunge juu ya uamuzi  wa mada za utoaji wa mimba na hasa kwa viumbe ambao bado hawana uwezo wa kujitea. Kwa maelezo zaidisoma: https://www.vaticannews.va/sw/church/news/2019-09/ecuador-wasiwasi-wa-kanisa-kuhusu-uhalishwaji-wa-utoaji-mimba.html

ECUADOR
20 September 2019, 09:17