Vatican News
Askofu Mkuu Dal Toso Katibu Mwambata,Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa,tarehe 23 Septemba 2019 amehutubia maaskofu wa Canada Askofu Mkuu Dal Toso Katibu Mwambata,Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa,tarehe 23 Septemba 2019 amehutubia maaskofu wa Canada 

CANADA:Kuna ulazima wa kufanya utume kwa watu wasio mtambua bado Kristo!

Katibu Mwambata,Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa,Jumatatu tarehe 23 Septemba 2019,ametoa hotuba yake katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Canada amesema kuwa haitoshi kusema Kanisa ni la kimisionari,nilazima kusema malengo ya utume wa kimisionari.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Askofu mkuu Giampietro Dal Toso, Katibu Mwambata, Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa, Jumatatu tarehe 23 Septemba 2019, ametoa hotuba yake katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Canada ambao utamalizika tarehe 27 Septemba 2019 katika Kituo cha Kiroho cha Nav, Cornwall, Ontario. Katika hotuba yakeAskofu Mkuu Dal Toso amesema haitoshi kwa urahisi kusema kuwa Kanisa ni la Kimisionari bali ni lazima kueleza malengo ya kitume ambayo ni ya utume wa (ad gentes), kwa mtu na watu ili kutoa tangazo la imani yaani Kristo alikufa  na akafufuka kwa ajili ya kujenga jumuiya mpya za Kikristo. Kwa kukazia kwa namna ya pekee juu ya asili ya utume, Askofu Mkuu Dal Toso amesisitiza maana yake akiangaziwa na   Mtaguso wa II wa Vatican katika Hati ya Kimisionari Ad gentes na kuonesha kuwa, wakati uliopita mara nyingi utume huo ulitambulia kama utume wa kusaidia katika kukuza maendeleo, hivyo ulisababisha matatizo nchini Canada kwa maana kile kilichoanzishwa kama msaada kwa ajili ya utume, kilibadilishwa kama vile ni msaada kwa ajili ya maendeleo.

Kuna ulazima wa kutangaza Neno kwa nchi ambazo imani imelegea

Miaka mingi hivi iliyopita tangu kumalizikwa kwa Mtaguso wa II kwa upande wake, haikuweka kizuizi bali kunyume  chake ni ambacho kinaonesha ulazima wa kufanya utume na utume wa ad gents, ikiwa na maana ya wale ambao bado hawamtambui Kristo. Aidha Askofu Mkuu akiongeza ufafanuzi wake amebainisha juu ya suala la asili ya umisionari na ambako amekazia kuwa juo upo katika mchakato wa mpango wa Baba Mtakatifu Francisko tangu kuteuliwa kwake kuwa kiongozi wa kusimamia Kanisa na kuongeza kusema kuwa  shughuli za kimisionari ndiyo kama mwavuli wa kila shughuli ya Kanisa. Hata hivyo amebainisha kuwa zaidi ya hali halisi yenyewe ambayo inajikita katika utume wa watu, ki urahisi ni kutazama takwimu  ambazo ni kwamba Uingereza asilimia 53 % ya watu wanathibitisha hawana habari yoyote kuhusu kidini; Ujerumani takwimu zinathibitisha kuwa kufikia mwaka 2060 wakristo watakuwa nusu ya wakristo wa sasa, kutokana na kwamba  vijana kati ya miaka 23-40 hawabatizi tena watoto wao katika Makanisa. Kwa njia hiyo hata katika nchi za magharibi, kuna ulazima wa kufanya  utume wa watu (Missio ad gentes), kwa maana ya kutangaza  tena imani kwa wale wasioamini.

Kubadilishana utume wa watu

Sambamba na mantiki hiyo ya utume wa watu, ndiyo kubadilishana binafsi na umisionari ambao Kanisa la Canada kwa miaka iliyopita walikuwa wanatuma  watu kwenda na kwa sasa wao wanapokea. Kwa dhati nyanja ya kimisionari ni nyanja mwafaka kwa ajili ya kuonesha uhusiano wa pamoja na wenye utajiri kati ya Kanisa la ulimwenguni na Kanisa mahalia amesisitiza Askofu Mkuu Dal Toso. Lakini kama kweli kwamba Kanisa la ulimwengu linapatikana kwa dhati ndani ya Kanisa mahalia, ni kweli kwamba, Kanisa mahalia haliwezi kuishi bila Kanisa la ulimwengu. Kati yao kuna uhitaji wa ule uhusiano unaozuia Kanisa mahalia lisijifungie lenyewe binafsi na  kugeuka kuwa Kanisa moja la Kitaifa. Na kadiri ya Kanisa mahalia linapojifungulia utume, linajigundua zaidi kwamba ni Kanisa pia la ulimwengu, linalojifunguliwa kwa watu wote wenye kuhitaji. Na ndiyo kwa njia ya shughuli ya kimisionari  zinaweza kuthibitisha wazi na kuonesha kuwa hakuna Kanisa linalo jitegemea peke yake, kwa maana linaishi kwa njia ya mkondo mzima wa maisha ambayo yanaunganisha Makanisa yote duniani.

Uhusiano kati ya Kanisa mahalia na la ulimwengu

Kadhalika Askofu Mkuu Dal Toso pia amesisitizia juu ya uhusiano kati ya Kanisa la ulimwengu na uhusiano wa mahalia kwa sababu mabaya mengi yanatokana  na Makanisa mahalia ambayo yamejitokeza katika ulimwengu mdogo na kukumbuka kuwa utumishi wa kiaskofu kwa mujibu wa Mtaguso wa Pili wa Vatican  unapaswa kueleweka kwa maana hiyo. Kwa maono mapana ya namna hiyo ya utume wa watu na uhusiano kati ya Kanisa mahalia na ulimwengu linajikita katika karama  za masharika ya kipapa ya kimisionari, ambao ni mtandao wa dunia katika huduma ya kipapa ili kusaidia utume na vijana wa Makanisa kwa sala na upendo, ambapo Askofu Mkuu pia ameonesha asili yake, lengo na muundo, huku akijikita kwa kina kuhusiana na  uhusiano na shughuli za kijimbo kichungaji.  Akitazama kuhusu ushirikiano wa kimisionari kati ya majimbo, Askofu Mkuu Dal Toso ameonesha kuwa hauwezi kubadilishwa umisionari wa ulimwengu ambapo Mfuasi wa Petro anahudumu kama Mchungaji duniani na ambao unapelekea ubinadamu kuwa kiini kipya hata katika makanisa ya utamaduni wa kizamani.  Vile vile ameonesha kuwa ukarimu wa kikuhani na kidini katika nchi za mashariki, lazima yajibidhishe kwa kina na kwamba makubaliano kati ya Maaskofu wa majimbo katika  kuanza na kukaribisha ambap pia  lazima yaanze kutazamia kuandaa huduma za kudumu katika nyakati kutokana na kwamba hawezekani kuwatoa  katika maeneo ya kitume wachungaji ambao wao wenyewe bado wanahitaji.

Maandalizi ya Mwezi wa kimisionari Oktoba 2019

Katika sehemu yake ya mwisho ya hotuba yake, Askofu Mkuu amegusia kuhusu mwezi Maalum wa kimisionari Oktoba 2019, huku akionesha asili yake ya kihistoria lengo ka  kitaalimungu katika uchungaji na baadhi ya matarajio katika matendo ya dhati. Wakati mwingine mtu anaweza kuwa na kishawishi cha  kuzingatia utume kama mwelekeo wa ziada wakati utume wa kimisionari ni muhimu, pia ni muhimu kuelewa uhusiano kati ya uchungaji wa kawaida na uchungaji wa kimisionari. Ufahamu wa kimisionari siyo kitu kilicho kandoni, kulingana na shughuli za kichungaji, kwa njia fulani ni upeo. Mashirika ya kipapa ya kimisionari yataka kuhudumia katika hatima  hiyo na Mwezi wa Kimisionari na ambapo ni fursa maalum katika hilo hasa katika kusadia shughuli za kichungaji ili kutoa mwamko wa nguvu zaidi katika utume wa kimisionari ambao pia unatoa msukumo zaidi  na zaidi.

Ikumbukwe kwamba  Mwezi  Maalum wa Kimisionari Oktoba 2019 unaongozwa na kauli mbiu “Mmebatizwa na kutumwa”. Na hii ni kuwa Mwezi Oktoba 2019 Kanisa litakuwa linaadhimisha Jubilei ya Miaka 100 tangu Papa Benedikto XV alipochapisha Waraka wa Kitume uituwao “Maximum Illud" yaani “Kuhusu Shughuli za Kimisionari.” Kwa njia hiyo Kanisa linaendeleza wito na utume wake wa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu hadi miisho ya dunia, ambalo ni agizo kutoka kwa Kristo mwenyewe kwa wafuasi wake.  Mathayo 28:19-20 “basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina …”. Na Injili ya Marko 16:15-18 Yesu akawaambia, “Nendeni ulimwenguni kote, mkawahubirie watu wote Habari Njema. Yeyote atakayeamini na kubatizwa ataokolewa”.

24 September 2019, 14:25