Tafuta

Vatican News
Monsinyo Paolo Rudelli ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi na Askofu mkuu. Monsinyo Paolo Rudelli ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi na Askofu mkuu. 

Monsinyo Paolp Rudelli ateuliwa kuwa Balozi na Askofu mkuu

Askofu mkuu mteule Paolo Rudelli alizaliwa tarehe 10 Julai 1970 huko Gazzaniga, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 10 Juni 1995 akapewa daraja Takatifu ya Upadre. Katika masomo yake, amebahatika kupata shahada ya uzamili katika Sheria za Kanisa na Shahada ya uzamivu kwenye Taalimungu maadili. Alijiunga na utume wa kidiplomasia tarehe 1 Julai 2001.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Paolo Rudelli, kuwa Balozi wa Vatican na wakati huo huo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu lakini atapangiwa kituo cha kazi taratibu za kidiplomasia zitakapokamilika. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Paolo Rudelli alikuwa ni Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya huko Strasbourg, nchini Ufaransa. Askofu mkuu mteule Paolo Rudelli alizaliwa tarehe 10 Julai 1970 huko Gazzaniga, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 10 Juni 1995 akapewa daraja Takatifu ya Upadre. Katika masomo yake, amebahatika kupata shahada ya uzamili katika Sheria za Kanisa na Shahada ya uzamivu kwenye Taalimungu maadili.

Askofu mkuu mteule Paolo Rudelli, alijiunga na utume wa kidiplomasia mjini Vatican kunako tarehe 1 Julai 2001. Na tangu wakati huo, ametekeleza utume huu nchini Equador, Poland na  kama afisa mwandamizi kitengo cha masuala ya kumla kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican. Tarehe 20 Septemba 2014 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya huko Strasbourg, nchini Ufaransa.

03 September 2019, 17:50