Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Paolo Borgia kuwa Balozi wa Vatican pamoja na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Paolo Borgia kuwa Balozi wa Vatican pamoja na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu  (Vatican Media)

Monsinyo Paolo Borgia ateuliwa kuwa Balozi na Askofu mkuu

Askofu mkuu mteule Paolo Borgia alizaliwa huko Manfredonia, Foggia, nchini Italia hapo tarehe 18 Machi 1966. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa daraja Takatifu ya Upadre tarehe10 Aprili 1999. Ana shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa. Tarehe 1 Desemba 2001 alijiunga na utume wa Kidiplomasia mjini Vatican. Utume: CAR, Lebanon, Israeli, na Mexico.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Paolo Borgia kuwa Balozi wa Vatican na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. Kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Afisa mwandamizi aliyekuwa anashughulikia masuala ya jumla kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican. Atapangiwa kituo cha kazi, mara baada ya taratibu za kidiplomasia kukamilika. Askofu mkuu mteule Paolo Borgia alizaliwa huko Manfredonia, Foggia, nchini Italia hapo tarehe 18 Machi 1966. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa daraja Takatifu ya Upadre tarehe10 Aprili 1999. Ana shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa.

Tarehe 1 Desemba 2001 alijiunga na utume wa Kidiplomasia mjini Vatican na tangu wakati huo, ametekeleza utume wake huko Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, Mexico, Israel na Lebanon. Baadaye alibadilishiwa utume na kupelekwa kwenye kitengo cha mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican na mwishoni, tarehe 4 machi 2016 aliteuliwa kuwa afisa mwandamizi aliyekuwa anashughulikia masuala ya jumla katika Sekretari kuu ya Vatican.

03 September 2019, 18:01