Tafuta

Vatican News
Tarehe 14 Mei 2020 utafanyika mkutano wa kimataifa mjini Vatican kuhusu kuujenga upya mkataba wa elimu Tarehe 14 Mei 2020 utafanyika mkutano wa kimataifa mjini Vatican kuhusu kuujenga upya mkataba wa elimu  

Ask.Mkuu.Zani:Mkutano kuhusu kuujenga upya mkataba wa Elimu duniani!

Askofu Mkuu Zani,Katibu wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki anasema kuwa,mkutano kuhusu Elimu mjini Vatican 2020 ni kukuza zaidi uwajibikaji kwa ajili ya wema wa kibinadamu.Watu wote wanaalikwa kuwa sehemu ya mapendekezo binafsi na yenye maana katika ulimwengu wa kisiasa,kiutamaduni na kidini,kwa namna ya pekee kwa vijana ambao ndiyo wakati endelevu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mkutano unaotarajiwa kufanyika 2020 kuhusu elimu mjini Roma lengo lake ni kutaka kukuza dhamiri ya utambuzi na uhamasishaji wa wimbi kubwa katika uwajibikaji kwa faida ya binadamu, kuanzia kwa vijana hadi kuwafikia watu wote wenye mapenzi mema. Ni maneno ya Askofu  Mkuu Vincenzo Zani, Katibu wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki akikifafanua katika gazeti katoliki la Sir,  kuhusu  sababu iliyomfanya Baba Mtakatifu Francisko aitishe Mkutano kuhusu Elimu unaotarajiwa kufanyika tarehe 14 Mei 2020 katika Ukumbi wa Papa Paulo VI mjini Vatican. Mkutano huo uitaongozwa na mada isemayo “Kujenga kwa upya Agano la Elimu”. Katika ufafanuzi wake Askofu  mkuu Zani amesema kwamba kuhusiana na suala la elimu kuna mipasuko mitatu ya kuponya.

Akifafanua kuhusu hiyo mipasuko mitatu ya kuponya anasema wa kwanza ni ule ambao hunatenganisha hali halisi kutoka juu. Hii ikiwa na maana ya kwamba kipeo kikubwa cha elimu kwa ujumla, hasa cha elimu katika mtazamo wa ukristo kimekuwa na ile tabia ya kujifungia binafsi kutoka kwa aliye juu. Mpasuko wa pili na ambao elimu inahitaji kuuponyesha au kuunganisha ni ule wa  kupungua kwa uhusiano kati ya vizazi na mambo mengine tofauti, na ambayo kati yake ni tamaduni na mali. Askofu Mkuu anabainisha kwamba Elimu inafikia lengo lake, ikiwa inaweza kuunda watu wenye uwezo wa kutembea pamoja kwenye njia za kukutana, majadiliano na kushirikishana, kwa heshima, kujaliana na kukaribishana pamoja.

Na hatimaye mpasuko wa tatu anautaja kuwa ni ule kati ya mtu, jamii, asili na mazingira. Hizi ni mipasuko ambayo mara kwa mara Baba Mtakatifu Francisko ameweza kuiripoti amesisitiza Askofu Mkuu na kuongeza kwamba, inahitaji jitihada kubwa na ushirikiano wa wote na  kwa ngazi zote. Aidha kwa kuhitimisha Askofu Mkuu Zan amekumbusha kwamba katika tukio la mkutano  utakao fanyika jijini Roma 2020,  hata hivyo utatanguliwa na safu kadhaa za semina zinazohusiana na eneo haki msingi za binadamu na sayansi ya amani,  eneo la majadiliano kati ya dini, mada zinazogusa maswala kuhusu makubaliano ya kielimu kati ya vijana na watu wazima, makubaliano ya asili na mazingira au mada kuhusu demokrasia, uchumi, ushirikiano wa kimataifa, masuala ya elimu isiyo rasmi au yale yanayohusu wahamiaji na wakimbizi.

Ikumbukwe kwamba Baba Mtakatifu tarehe 12 Septemba 2019 ametangaza tukio la mkutano huo wa kidunia utakao fanyika tarehe 14 Mei 2019 ambao itaongozwa na mada ya “Kuujenga upya mkataba wa Elimu Ulimwenguni”  huku akiangazia “Hati ya Udugu wa Kibinadamu iliyotiwa kwa pamoja sahini na Imam Mkuu wa Al Azhar huko Abu Dhabi tarehe 4 Februari 2019. Baba Mtakatifu Francisko anasema ni “kuujenga upya mkataba wa elimu duniani” ambao unaelimisha “mshikamano ulimwengu” na “ubinadamu mpya” na hatimaye kuweza kukabiliana na changamoto za dunia katika  “mwendelezo wa mabadiliko” na “ambayo yanapitia katika vipeo vingi”. Aidha Baba Mtakatifu ametoa ujumbe huo kwa wahudumu wote katika nyanja za elimu na tafitii , kwa wahudumu  wote wa umma na ambao wanashika nafasi ya uwajibikaji kwa ngazi ya ulimwenguni na ambao kwa hakika wana jali rohoni mwao hatima za vizazi vipya!

 Kuujenga wakati endelevu wa sayari: Baba Mtakatifu Francisko anawaalika watu wote wenye mapenzi mema kuunganisha nguvu zao kwa ajili ya kupyaisha majadiliano kuhusu namna ambayo tunajenga wakati ujao wa sayari na kuunda makubaliano mpana sana ya elimu ili  kuwaudana watu waliokomaa, na wenye uwezo wa kusuluhisha migawanyiko na kinzani, na wakati huo huo kuweza kujenga tena ile tishu ya uhusiano kwa ajili ya ubinadamu zaidi na kindugu.  Baba Mtakatifu Francisko aidha amesema haya ni makubaliano kati wazalendo wa ardhi na nyumba ya pamoja, ambayo ni lazima tuitunze na kuheshimu. Ni muungano ambao hutunza haki, amani na kukaribishana kati ya watu wote wa familia moja ya binadamu na majadiliano kati ya dini!

13 September 2019, 16:13