Vatican News
Ijumaa tarehe 30 Agosti 2019 yamefanyika mazishi ya Kardinali Achille Silvestrini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican Ijumaa tarehe 30 Agosti 2019 yamefanyika mazishi ya Kardinali Achille Silvestrini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican   (Vatican Media)

Mazishi ya Kard.Silvestrini:alikuwa mtu wa mazungumzo na huduma ya kweli ya Papa,Vatican na Jamii!

Ijumaa tarehe 30 Agosti 2019 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vaticani,misa ya mazishi ya Kardinali Achille Sivestrini imeongozwa na Kardinali Giovanni Battista Re,makamu rais wa Baraza la makardinali na mwisho wa misa hiyo Baba Mtakatifu Francisko ameongoza ibada ya mwisho ya kumpa buriani marehemu.Baada ya Ibada hiyo Baba Mtakatifu amesalimiana na Waziri Mkuu wa Italia Bwana Conte.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican News

Kufuatia na kifo cha aliyekuwa Rais Mstaafu wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki,Kardinali Achille Silvestrini, kilichotokea tarehe 29 Agosti 2019 katika Hospitali Katoliki ya Gemelli Roma, yamefanyika mazishi yake mchana siku ya Ijumaa tarehe 30 Agosti 2019, katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, na kuongozwa na  Kardinali Giovanni Battisa Re makamu rais wa Baraza la makardinali na hatimaye  Baba Mtakatifu Francisko ameongoza ibada fupi ya mwisho ya kumpa buriani marehemu (Commendatio na  Valedictio). Katika mahubiri ya Kardinali Re, kwenye misa hiyo amesema kuwa  mbele ya kifo na mbele ya kila kitu cha mwisho kati ya kutengenisha maisha haya katika ardhi hii, ni neno moja tu kutoka kwa Mungu ambalo linafariji. Somo la kwanza kutoka katika kitabu cha Ayubu, anasema, "nami menyewe ninajua vema kwamba mkombozi wangu yuko hai….. baada ya ngozi yangu kuharibika nitamwaona Mungu… na ambaye macho yangu yatamtafakari kwa hakika, wala sitokuwa mgeni ( Ay 19,I.23-27).

Mungu anatoa ahadi ya kuona utukufu wake 

Kardinali Re aliekiendelea na mahubiri yake amesema, vile vile Mtakatifu Paulo anatoa uhakika  wa uhai huo kwa wakati ujao aksema: "Ndugu kwa maana tunajua kwamba utakapo haribiwa mwili huu, nyumba yetu ya kidunia, tutapata makao kutoka kwa Mungu, nyumba ya milele ambayo haijajengwa kwa mikono ya mwanadamu mbinguni (2 Kor.5,1). Na maneno ya Injili yamethibitisha kuwa, mapenzi ya Kristo ya kuwa na utukufu wake kwa wote ambao wamekuwa wake katika ardhi hii. Katika maneno ya Yesu anasema: "Baba, ninataka wale ambao umenipa wawe pamoja nami mahali nilipo ili waone na kutafakari utukufu wangu" ( Yh 17,24). Katika kufafanua hilo Kardinali Re amethibitisha kwamba, katika mwanga wa ukweli huo na uhakika wa imani,ni kumuaga kwa sala za mwisho Kardinali Achille Silvestrini, ambaye Bwana amemwita kwake akiwa na umri wa miaka 95.

Maisha yake marefu katika huduma ya Kanisa,Papa Vatican na jamii

Maisha yake marefu na kazi yake ilikuwa kwa hakika kijitosa katika Curia ya Roma katika huduma ya Kanisa, ya Papa na Vatican kwa ujumla, lakini hata kwa ajili ya jamii nzima, kwa maana ya kushika nafasi mbalimbali na alizozifunika na kupelekea katika kuhamasisha amani, haki za binadamu na sababu mbalimbali za kibinadamu katika nyanja ya kimataifa. Tabia yake daima ilikuwa na roho kubwa ya kikuhani kwa macho maalum ya kujikita kwa kina katika mafunzo ya vijana. Aidha Karidnali Re, ameweze kupitia maisha yake yote tangu kuzaliwa huko Bisighella Faebza Italia kunako mwaka 1923, daraja la upadre Faenza kunako 1946. Masomo yake na shahada za Fasihi na Falsafa katika Chuo Kikuu cha Bologna na baadaye Utroque iure katika Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano na wakati huo huo alikuwa pia mwanafunzi wa Taasisi ya Kipapa ya Kanisa. Kwa miaka 36 amefanya kazi katika Ukatibu wa Vatican na  heshima yake iliendelea kukua. Alikuwa na umakini sana kwa watu, utamaduni wake, ufahamu wa watu, matukio na uwezo wake wa kuchunguza na kuingia kwa kina shida za watu ziliwapatia matumaini  ya mambo yanayowezekana, kwa faida ya Kanisa lakini pia kwa jamii nzima.

Salam za Baba Mtakatifu Francisko kwa Waziri Mkuu Conte wa Italia 

Baada ya Misa Takatifu Baba Mtakatifu Francisko amesalimiana na Waziri Mkuu aliyepewa mamlaka na Rais kwa sasa, Bwana Giseppe Conte. Haya ni kwa mujibu  wa Msemaji Mkuu wa Vatican, Bwana Matteo Bruni akijibu maswali ya waandishi wa habari jioni. Katika utuhibitisho wake amesema: “ Mchana huu  kandoni kabia baada ya mazishi ya Kardinali Achille Silvestrini, Baba Mtakatifu Francisko kwa muda mfupi ameweza kumsalimia Waziri Mkuu  wa Italia, Giuseppe Conte, na pamoja naye amekumbuka kwa upendo mkuu sura ya Kardinali Silvestrini.”

31 August 2019, 09:21