Kardinali George Pell atiwa hatiani na Mahakama ya Victoria, lakini akata rufaa Mahakama Kuu ya Australia. Kardinali George Pell atiwa hatiani na Mahakama ya Victoria, lakini akata rufaa Mahakama Kuu ya Australia. 

Kardinali George Pell, atiwa hatiani, akata rufaa Mahakama kuu

Kardinali Pell, daima amekuwa akijitetea kuwa hana hatia katika shutuma zote zinazoelekezwa dhidi yake na kwamba, kwa wakati huu, ameamua kukata rufaa kwenda kwenye Mahakama kuu nchini Australia. Vatican inaungana na Kanisa mahalia nchini Australia kuonesha uwepo wake wa karibu kwa wahanga wa nyanyaso za kijinsia pamoja na familia zao. Wakleri wanapaswa kuwajibika.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Mahakama ya Victoria nchini Australia imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imetolewa na Kardinali George Pell aliyekuwa anatuhumiwa kwa kesi ya nyanyaso za kijinsia dhidi ya watoto wadogo na hivyo kupatikana na hatia. Kardinali Pell ataendelea kutumikia kifungo cha miaka sita jela, ambacho alikianza tangu tarehe 27 Februari 2019 kwenye gereza lenye ulinzi mkali nchini Australia. Dr. Matteo Bruni Msemaji mkuu wa Vatican katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amebainisha kwamba, Vatican inaheshimu na kuthamini hukumu iliyotolewa na Mahakama nchini humo. Kardinali Pell, daima amekuwa akijitetea kuwa hana hatia katika shutuma zote zinazoelekezwa dhidi yake na kwamba, kwa wakati huu, ameamua kukata rufaa kwenda kwenye Mahakama kuu nchini Australia. Vatican inaungana na Kanisa mahalia nchini Australia kuonesha uwepo wake wa karibu kwa wahanga wa nyanyaso za kijinsia pamoja na familia zao.

Vatican inawataka viongozi wa Kanisa kuhakikisha kwamba, wakleri wao wanawajibika barabara. Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa linasubiri kukamilika kwa kesi hii na hatimaye liweze kutoa maamuzi mintarafu Sheria, kanuni na taratibu za Kanisa. Baba Mtakatifu Francisko amekwisha kutoa maelekezo kwamba, kadiri ya Sheria, taratibu na kanuni za Kanisa, Kardinali George Pell haruhusiwi tena kuadhimisha Mafumbo ya Kanisa hadharani wala kukaribiana na watoto wadogo. Dr. Matteo Bruni Msemaji mkuu wa Vatican katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amebainisha kwamba, Kardinali George Pell amesikitishwa sana na hukumu iliyotolewa dhidi yake, kati ya Majaji watu, wawili peke yao ndio waliomkuta na hatia. Kardinali George Pell anaendelea kukiri kwamba, hana hatia dhidi ya shutuma na hatimaye, hukumu iliyotolewa dhidi yake.

Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Australia linasema, kwa hakika kila mtu ni sawa mbele ya sheria za nchi, lakini hukumu iliyotolewa dhidi ya Kardinali Pell imewashangaza wengi. Kumekuwepo na utata mkubwa katika kutafuta, ili kuweza kuupata ukweli wenyewe. Mawazo na sala zao, zinaelekezwa kwa wale waliopeleka shitaka hili mahakamani. Kanisa litaendelea kumpatia Kardinali Pell huduma za maisha ya kiroho na kichungaji kama ilivyo hata kwa wafungwa na maabusu wengine nchini Australia.

Kardinali Pell

 

22 August 2019, 10:42