Askofu Ayuso Guixot: Matunda ya Hati ya Udugu wa Kibinadamu yaanza kuonekana! Kiu ya amani!
Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Wakati wa mahojiano na Vatican News Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya majadiliano kidini Askofu Mkuu Miguel Ángel Ayuso Guixot,amejaribu kuelezea juu ya tathmini ya matunda ya kwanza ya Azimio la pamoja kuhusu Udugu wa kibinadamu uliotiwa sahini mwezi februari mwaka huu huko Abu Dhabi na Baba Mtakatifu Francisko akiwa na Imam mkuu wa di Al Azhar. Askofu Mkuu Guixot amesema mazungumzo ya ukidini ndiyo njia bora ya kuweza kukabiliana na uovu wa itikadi kali. Hata hivyo amesisitiza juu ya kuanzishwa hivi karibuni Kamati kuu mpya kwa ajili ya utekelezwaji wa Hati ya Udugu wa kibinadamu na ambayo ni hatua ya kwanza ya mchakato mzima wa utekelezaji. Kwa upande wake amesema Kamati hiyo na ambapo ametiwa moyo na Baba Mtakatifu Francisko ni mfano wa dhati katika jitihada za viongozi wa kidini ili waweze kujenga madaraja, ujenzi wa mazungumzo na kishinda vishawishi vya kujifungia binafsi ambavyo pia vinafafanua katika malumbano dhidi ya maendeleo.
Kuundwa kwa Kamati kuu ni tendo lenye maana
Kuundwa kwa Kamati kuu ni tendo la maana sana amebainisha, na hii ni kama inavyosomeka katika maelezo yaliyo andikwa wakati wa kuzaliwa hati hiyo na kwamba ni kuhamasisha mawazo yaliyomo kwenye hati ya Udugu kibinadamu kwa sababu ni tamko la pamoja katika jitihada za kuunganisha binadamu na kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya amani duniani na mwisho ili kuweza kuhakikisha kuwa, vizazi vijavyo vinaweza kuishi katika hali ya kuheshimiana na kuishi vema pamoja. Lengo hili ni bora! Aidha anamshukuru mrithi wa Abu Dhabi, Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan ambaye amefanya kazi ili kuwa na maendeleo ya mpango na kutekeleza malengo ya hati ya Udugu wa Kibinadamu ya Abu Dhabi. Aidha anamshukuru Baba Mtakatifu Francisko na Imam Mkuu wa Al- Azhar kwa sababu ya maneno na ushuhuda wao ambao umewezesha kile alichosema mrithi katika dibaji ya Kamati kuu.
Nini kilimvutia katika ziara ya Baba Mtakatifu katika nchi za uarabuni
Kuhusiana na suala la kile kinacho mvutia zaidi katika utashi wa mazungumzo ya Baba Mtakatifu kwenye ziara katika nchi za Uarabuni awali ya yote anatoa shukrani kwa ajili ya jitihada za uhamasishaji wa mazungumzo! Na kwa hakika amabainisha kwamba ni kwa mapapa wote waliomtangulia Baba Mtakatifu Francisko kuhusiana na mazungumzo yao ya heshima na urafiki, kwa maneno na matendo. Zaidi ameongeza kusema hawakosi kamwe kutoa ushauri katika dunia nzima na kwa watu wote wenye mapenzi mema na hasa katika kuhamasisha mambo matatu:udugu, amani na kuishi vizuri. Ameongeza kusema kuwa watu wote hawapaswa kusahau kuwa mambo haya matati ndiyo nguzo msingi iwapo tunataka kweli kupona majeraha ya dunia yetu. na ndiyo kitabu cha mwanzi kama ABC na cha wakati endelevu. Ni wengi walioshirikiana katika mpango wa kuandaa hati hiyo amesema, na kwa hakika wanakukwa katika sehemu ya mwisho ya Hati hiyo.
Kamati kama tamko inazaliwa na kutokana na mazungumzo kati ya waislam na wakristo, kuna uwezekano wa kufikiria upanuzi wa dini nyingine
Askofu Mkuu Guixot akielezea muktadha kuhusu kamati iliyozaliwa kutokana na tamko amesema, Tamko linazaliwa na mazungumzo kati ya waislam na wakristo kwa mantiki ya mkutano mkuu juu ya Udugu wa Kibinadamu. Na ndiyo mantiki ya ulimwengu ambayo ndiyo ujumbe wa tamko lililo enea dunia kote na ambalo ni dirisha jipya linalojifungua kwa mantiki ya Roho ya Assisi. Kwa matokeo zaidi ya nani, wapi na lini, katika ujumbe wa ulimwengu kuhusu udugu wa amani na kuishi pamoja ni jumuishi na kushirikishwa kwa wote waamini wa dini zote, pamoja na watu wote wenye mapenzi mema. Kwa mfano amesema, mwezi ujao Septemba, ataudhuria mkutano wa kimataifa huko Madrid, Spain mkutano kuhusu watu na dini, ulioandaliwa na Jimbo Kuu Katoliki la Madiri na Jumuia ya Mtakatifu Egidio. Katika meza ya mduara ya Mkutano huo watazungumzia kwa dhati juu ya tema hii ya udugu wa kibinadamu pamoja na wahusika wa dini mbalimbali.
Dini zinazokiri Mungu mmoja lazima kufanya kazi pamoja na nyingine zote
Jambo pia muhimu ambalo amekazia amesema dini zinazomkiri Mungu mmoja pamoja na zingine zote zitatakiwa kufanya kazi pamoja kwa sababu ndicho kilichosainiwa na Baba Mtakatifu Francisko na Imam Mkuu, kwamba kila sehemu iweze kuenea ile hali ya kuishi kwa amani na wema wa kibinadamu. Kutokana na hili Kamati mpya itakuwa chombo muhimu sana amesema. Na kwa sababu hii ametumia fursa hiyo kusasisha shukrani zake binafsi kwa tathmini yenye thamani ambayo Imamu Mkuu, ndugu yao wa Al Azhar amefanya katika vyombo vya habari na ambayo anaungana nao kwa niaba ya Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini na Yeye akiwa kama rais wake.