Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Petar Antun Rajic kuwa Balozi wa Vatican nchini Estonia, Latvia pamoja na Lithuania. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Petar Antun Rajic kuwa Balozi wa Vatican nchini Estonia, Latvia pamoja na Lithuania. 

Askofu mkuu Petar Rajic ateuliwa kuwa Balozi: Estonia & Latvia

Askofu mkuu Rajič alizaliwa kunako tarehe 12 Juni 1957. Alipadrishwa kunako tarehe 29 Juni 1987. Tarehe 2 Desemba 2009 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu hapo tarehe 23 Januari 2010. Na Mwaka 2019 ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Lithuania, Estonia na Latvia!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Petar Antun Rajič kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini: Estonia na Latvia ataendelea pia kuwa Balozi wa Vatican nchini Lithuania. Kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Angola, Sao Tome na Principe. Askofu mkuu Petar Rajič amewahi pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Kuwait, Bahrein, Yemen, Qatar na Falme za Kiarabu pamoja na kuwa ni mwalikishi wa Kisiwa cha Kiarabu.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Rajič alizaliwa kunako tarehe 12 Juni 1957. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa hapo tarehe 29 Juni 1987. Tarehe 2 Desemba 2009 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu hapo tarehe 23 Januari 2010. Na Mwaka 2019 ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Lithuania, Estonia na Latvia! Utume mwema kwa watu wa Mungu katika nchi hizi tatu!

Askofu Mkuu Rajic
06 August 2019, 11:56