Tafuta

Vatican News
Askofu mkuu Ivo Scapolo ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ureno, kabla ya uteuzi huu alikuwa nchini Chile. Askofu mkuu Ivo Scapolo ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ureno, kabla ya uteuzi huu alikuwa nchini Chile.  (ANSA)

Askofu mkuu Ivo Scapolo ateuliwa kuwa Balozi nchini Ureno

Askofu mkuu Ivo Scapolo alizaliwa tarehe 24 Julai 1953 huko Terrassa, Padua, Kaskazini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, tarehe 4 Juni 1978 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 26 Machi 2002, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu mkuu na hatimaye, kuwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu hapo tarehe 12 Mei 2002 na Kardinali Angelo Sodano.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Ivo Scapolo kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ureno. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Ivo Scapolo alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Chile. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Ivo Scapolo alizaliwa tarehe 24 Julai 1953 huko Terrassa, Padua, Kaskazini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, tarehe 4 Juni 1978 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 26 Machi 2002, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu mkuu na hatimaye, kuwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu hapo tarehe 12 Mei 2002 na Kardinali Angelo Sodano, enzi hizo akiwa Katibu mkuu wa Vatican.

Tarehe 17 Januari, 2008 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Rwanda. Na tarehe 15 Januari 2011, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamwamisha na kumtuma kwenda kuwa Balozi wa Vatican nchini Chile. Tarehe 29 Januari 2019, akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Ureno, wakati huu watu wa Mungu nchini humo wanapoendelea na maandalizi ya Siku ya XXXV Vijana Duniani. Itakumbukwa kwamba, maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani ni tukio ambalo linaendelea kupyaisha maisha na utume wa Kanisa kwa kuona tena ufunuo wa Uso wa huruma na upendo wa Mungu katika maisha ya vijana wa kizazi. Maadhimisho ya Siku ya XXXV ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2022 yatafanyika Jimbo kuu la Lisbon, nchini Ureno.

Papa: Ureno
30 August 2019, 13:39