Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI tarehe 25 Juali 2019 amefanya ziara ya ghafla huko Castel Gandolfo,Madhabahu ya Mama Maria wa Tufo, Rocca di Papa na Uasikofuni Frascati Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI tarehe 25 Juali 2019 amefanya ziara ya ghafla huko Castel Gandolfo,Madhabahu ya Mama Maria wa Tufo, Rocca di Papa na Uasikofuni Frascati 

Ziara ya ghafla ya Papa Mstaafu Benedikto XVI katika Majengo ya Kiroma!

Castel Gandolfo,madhabahu ya Mama Maria wa Tufo,Rocca di Papa na Uaskofuni Frascati ndiyo maeneo ambayo siku ya Alhamisi mchana tarehe25 Julai,Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI alifanya ziara yake kufuatia na mwaliko wa Askofu Raffaello Martinelli.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika  kujibu maswali ya waandishi wa habari, Msemaji Mkuu wa Vatican, Dk. Matteo Bruni amethibitisha yafuatayo: “ka,a alivyoelekezwa na Askofu Mkuu Georg Gänswein  msimamizi mkuu wa nyumba ya Kipapa asubuhi tarehe 26 Julai 2019 kwamba,  Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, tarehe 25 Julai mchana saa 10.15  alikwenda  Castel Gandolfo, mahali ambapo aliweza kuzunguka katika bustani hiyo wakati kaizunguka na  kusali rosari, baadaye alikwenda katika madhabahu ya Mama Maria wa Tufo huko Rocca di papa na hatimaye akiwa na Askofu Raffaello Martinelli, Askofu wa Jimbo la Frasicati walikula chakula cha jioni. Na  Saaa 4.30  walirudi katika Manostri ya Mater Ecclesiae. Ziara yake hii ni kujibu mwaliko aliopewa na  Askofu Raffaello Martinelli wa Frascati.

Mahojiano ya Askofu Raffaello Torelli wa Jimbo la Frascati na Vatican News kuhusu ziara ya Baba Mtakatifu Mstaafu  

Katika mahojiano na Askofu Raffallo Torelli, Askofu wa Frasicati kuhusiana na ziara ya  Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuitembelea madhabahu ya Mama Maria wa Tufo huko Rocca di papa amesema  kwa hakika  Baba Mtakatifu msataafu “ni mtu mkarimu sana, mpole sana na mwenye imani kubwa ambaye anaonesha amani kubwa ya kina  kwa njia ya tabasamu na macho yake.

Madhabahu ya Mama wa Tufo

Baba Mtakatifu Mstaafu alifika na kupokelewa huko katika madhabahu ya Mama maria wa  Tufo huko Rocca di papa. Aliwasiri majira  ya  saa 12.30 jioni kwa masaa ya Ulaya akitokea Castel Gandolfo. Askofu kwa haraka alikaribia gari na kuwapokea kwa kwa shangwe. Kati ya Baba Mtakatifu Mstaafu na Askofu huyo kwa hakika kuna uhusianoa wa kifamilia kwa sababu askofu Marnelli alikuwa ni mhudumu wa Josefu Ratzinger wakati akiwa kama Rais wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa.

Na wakati wa kipindi cha kujiunda katika sala, ndani ya Madhabau, Baba Mtakatifu Mstaafu aliingia akisindikizwa kwenye kiti cha wagonjwa na jambo la kwanza alitaka kupiga magoti ili kusali kwa sauti kutokana na wale walio kuwa ndani ya Kanisa la Bikira Maria. Hata hivyo katika madhabah hayo pia Baba Mtakatifu Mstaafu XVI alikuwa amekwisha eleza juu ya kutembelea madhabahu hiyo wakati uliopita. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kwa kupendelea kusali kwake Bikira Askofu amesema “ nimwelekeza mahali penye Tabernakulo iliyo na  Sakramenti Takatifu na Baba Mtakatifu Mstaafu amepiga magoti  mbele ya Yesu.

Historia fupi ya madhabahu hiyo

Kwa mujibu wa utamaduni wa karne ya XVI historia ya madhabahu hiyo inasema ili kuwa ni mpita njia mmoja wakati alikuwa akitembea katika njia hiyo, mara kwa ghafla  aliona jiwe kubwa la mviringo likibomoka katika mwamba mkubwa na lenye karibu kilo 150 hivi. Ilikuwa ni hatari ambapo mtu huyo alimwomba Mama Maria na kwa ghafla kama muujiza jiwe hilo lilibaki limesisima na msafiri huyo akaokoka. Jiwe hili kubwa anaeleza, Askofu Torelli limechongwa sura ya Mama Maria ambaye hadi leo hii anatolewa ibada.

Urahisi wake, unyenyekevu na upole

Mara baada ya ziara yake katika Madhabahu ya Bikira Maria Baba Mtakatifu Msataafu Benedikto XVI amepanda gari kwa upya ili kuelekea katika nyumba ya Askofu wa Fraskati kwa ajili matembezi  na urafiki wake askofu huyo. Ni ziara ambayo anabainisha Askofu Torelli kwamba,“imeacha utulivu mkubwa na imani na  hata kama kilelezo na maoni  ya wale ambao kama mimi nimekuwa mbele ya Benedikto XVI, ni ile ya mtu ambaye anaishi daima na uwepo wa Mungu, mtu mwenye utakatifu na  ambaye anauonesha kwa maana ya  kimungu zaidi katika uwezo wake kimwili. Kwa maana ya kuuonesha kwa njia ya macho na tabasamu, kwa unyenyekevu na urahisi wa utu wake.

26 July 2019, 14:11