Tafuta

Kambi ya wakimbizi wa Siria nchini Lebanon Kambi ya wakimbizi wa Siria nchini Lebanon 

Vatican:Haiwezekani kubaki viziwi mbele ya ukosefu wa chakula na madawa!

Upo wasiwasi mkubwa wa Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya hali halisi ya kibinadamu nchini Siria ambayo pia imezungumzwa na Askofu Mkuu Bernadito Auza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini New York.Katika hotuba yake ni matashi mema ya kuwa inawezekana kurudia mchakato wa maridhiano kati ya Waisraeli na Wapelestina.Msaada wa kibinadamu ni msingi katu kukosekana;anatazama nchi ya Yemen inahitajika matendo ya dhati.

Na Sr. Angela Rwezaula

Tarehe 23 Julai 2019, Askofu Mkuu Bernadito Auza, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko mjini New York Marekani ametoa hotuba yake katika kikao kinachohusu Nchi za Mashariki na Palestina. Katika hotuba hiyo anamshukuru Rais wa Peru katika ufunguzi wa majadiliano kuhusu nchi za Mashariki pamoja na masuala ya Palestina. Wiki iliyopita katika maelezo mafupi kwenye Kikao cha usalama ambaco kilikuwa kimeandaliwa maalum kwa ajili ya mkachakato wa amani nchi za mashariki, Nickolay Mladenov, alibainisha juu ya hatari ya  kuongezeka kwa vurugu huko Gaza na vurugu zinazoendelea katika Benki ya Magharibi. Aidha alieleza juu ya ukosefu wa umoja pande zote mbili na mgawanyiko ya ndani inayoinamia mazingira ya kutoaminiana.

Migogoro hiyo amesema inachangiwa na itikadi za hatari na zenye msimamo mkali na wakati huo huo ukosefu wa kuaminiana kunaweza kwa haraka kutokeza vitendo vya ukatili ambavyo vinaweka maisha ya Wapalestina wasio na hatia na Israeli kwa pamoja  katika hatari na kuathiri vibaya kanda pana amesisitiza Askofu Mkuu Auza. Na hali kama hii haiwezi kuruhusu mjadala huu kubaki kimya kama mazoezi ya ukweli yanayojulikana na maoni juu ya shida na vizuizi ambavyo vinazuia kufikia matarajio kwa miaka miwili,  mara baada ya mipaka kutambuliwa kimataifa, kwa maana hiyo ni lazima zitekelezwe kwa hatua anabainisha!

Michango ya ukarimu ya UNRWA

Askofu Mkuu Auza aidha amebainisha kwamba kupitia michango wa kutoa kwa ukarimu hasa kwa njia ya UNRWA, jumuiya ya kimataifa inaendelea kuhakikisha kuwa elimu, huduma za afya na huduma zingine za msingi zinaweza kutolewa kwa wakimbizi wa Palestina na hali hiyo iweze kuendelea bila kusitishwa. Hata hivyo ameonesha kwamba, tayari kuna ukosefu wa ajira mkubwa na matarajio madogo kwa vizazi vilivyopo na vijanavyo, kandoni mwa mahitaji ya chakula na maji yanayoongezeka. Lakini wakati huo huo, msaada wa kibinadamu na kiuchumi unabaki kuwa muhimu  hasa katika  kuunda mazingira ya mazungumzo,na ambayo hayawezi kubadilishwa na katu na  mchakato wa mazungumzo. Utashi wa kisiasa na ujenzi wa mazungumzo yanahitajika ili kuweka masharti ya amani ya kudumu na suluhisho kamili na endelevu. Mchango muhimu kwa Nchi Wanachama unaoweza kutolewa kwa wakati huu ni kuhamasisha wote wanarudi kwenye meza ya mazungumzo na kuwapa nafasi na rasilimali ya kujitolea kujadiliana kama wahusika wa mustakabali wao wa Amani ya  pamoja.

Haiwezekani kupuuza hali halisi za nchi ambazo hazina utulivu kama Siria

Askofu Mkuu Auza akiendelea na hotuba yake katika suala la hali halisi ya migogoro anasema, kwa kuzingatia nchi za Mashariki ya Kati, hatuwezi kupuuza maeneo ambayo bado hayana utulivu kama nchini Siria, ambapo hatari ya shida mbaya ya kibinadamu imebaki kuwa ya juu. Hatuwezi kuwa viziwi kwa ajili ya kilio cha wale wanaokosa chakula, huduma ya matibabu na masomo, au wale mayatima, wajane na waliojeruhiwa. Tarehe 22 Julai, Amesema Askofu Mkuu Auza, katika barua yake kwa Rais Bachar El-Assad, Baba Mtakatifu Francisko ameonyesha umakini wake mkubwa juu ya hali ya kibinadamu nchini Siria na hasa, kwa hali kubwa ya wanadamu wanayoyokabili rai wa Idlib. Alisasisha wito wake kwa ajili ya kuwa na linzi wao na kwa heshima ya sheria za kibinadamu za kimataifa.

Aidha, Askofu Mkuu Auza ameongeza kusema, hali inayoongezeka ya kibinadamu nchini Yemen pia ni sababu ya wasiwasi mkubwa, hasa wakati wale wanao hitaji sana wananyimwa chakula na matibabu. Makubaliana ya  Halmashauri kunamo tarehe 15 Julai kwa  Azimio namba  2481 lenye kutaka kurekebisha agizo la Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Kuunga mkono Makubaliano ya Hodeidah, lilikuwa hatua inayohitajika kuimarisha utekelezaji  na kuwezesha upatikanaji wa vifaa na  zana muhimu na kutokana na hiyo kuna haja ya kushikamana, amesisitiza. Kadhalika anauliza swali Je! Tunawezaje kufanya kujikimu vizuri kwa ajili ya amani katika Mashariki ya Kati na hata kujitolea kwa vitendo vya kibinadamu wakati huo huo tukiendelea kubali mauzo  ya silaha katika kanda?

Akigusia nchini Iraq

Hata hivyo Iraq, baada ya uhalifu wa kinyama ambapo ISIL imewanyanyasa wakazi wake, hasa washiriki wa dini ndogo ndogo na za kikabila, inatoa tumaini wakati inasonga mbele katika njia ya maridhiano na ujenzi upya, “kupitia harakati ya amani ya pamoja wema kwa upande ya jumuiya zote. Hata hivyo kwa kuongezea amesema ni  muhimu kwamba jamuiya ya kimataifa iendelee kuhimiza na kutafuta kila fursa inayo wezekana ya mazungumzo na suluhisho la amani katika majanga  ya sasa katika mkoa wa Ghuba. Huu ni wakati muhimu sana ambapo nchi zote hazipaswi kusitisha maendeleo kutafuta amani na badala ya kurudi nyuma katika uhasama unaosababishwa na mizozo inayoingiliana ya nguvu katika mkoa. Badala yake ni muhimu kukuza mazungumzo zaidi ya utamaduni wa uvumilivu, kukubalika ya wengine na ya kuishi pamoja kwa amani; kwa njia hii, wanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza shida nyingi za kiuchumi, kijamii, kisiasa na mazingira ambazo zina uzito sana kwa sehemu kubwa ya ubinadamu.

25 July 2019, 10:54