Tafuta

Vatican News
Vatican na Burkina Faso wametiliana mkataba wa ushirikiano kati ya serikali na Kanisa kwa aqjili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini humo: kiroho na kimwili! Vatican na Burkina Faso wametiliana mkataba wa ushirikiano kati ya serikali na Kanisa kwa aqjili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini humo: kiroho na kimwili!  (Vatican Media)

Vatican na Burkina Faso watiliana sahihi ya ushirikiano!

Serikali na Kanisa hata katika tofauti zao msingi, zinahamasishwa kujenga umoja, ushirikiano na mshikamano kwa ajili ya kukuza na kudumisha ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Burkina Faso: Katika maisha ya kiroho, kimaadili na kiutu! Utekelezaji wa Itifaki hii ya Makubaliano utaanza mara tu baada ya pande hizi mbili kubadilishana nyenzo za utekelezaji wake.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican, Ijumaa, tarehe 12 Julai 2019 ameongoza ujumbe wa Vatican ili kuwekeana sahihi Mkataba wa Makubaliano kati ya Vatican na Serikali ya Burkina Faso, kuhusu utambuzi wa Kanisa Katoliki kisheria nchini Burkina Faso, ambayo imewakilishwa na Bwana Alpha Barry, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Burkina Faso. Tukio hili limehudhuriwa pamoja na viongozi wakuu kutoka Ubalozi wa Vatican nchini Burkina Faso na alikuwepo pia Kardinali Philippe Ouèdraogo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Ouagadougou.

Na kwa upande wa Serikali ya Burkina Faso alikuwepo Bwana Robert Compaorè, Balozi wa Burkina Faso mjini Vatican. Itifaki ya Mkataba huu umegawanyika katika Sura 19 zinazotoa fursa ya Kanisa Katoliki nchini Burkina Faso kutekeleza dhamana na wajibu wake kikamilifu. Viongozi wa Kanisa na Taasisi zake, watatambulikana kisheria. Serikali na Kanisa hata katika tofauti zao msingi, zinahamasishwa kujenga umoja, ushirikiano na mshikamano kwa ajili ya kukuza na kudumisha ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Burkina Faso: Katika maisha ya kiroho, kimaadili na kiutu! Utekelezaji wa Itifaki hii ya Makubaliano utaanza mara tu baada ya pande hizi mbili kubadilishana nyenzo za utekelezaji wake.

Vatican: Burkina Faso
12 July 2019, 16:19