Tafuta

Vatican News
Kardinali Turikosno amkabidhi barua ya Papa Rais wa Siria Kardinali Turikosno amkabidhi barua ya Papa Rais wa Siria   (ANSA)

Uthibitisho wa barua ya Papa kwa Rais Bashar Hafez al-Assad

Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa vyombo vya habari Vatican Dk Bruni amethibitisha juu ya barua ya Papa Francisiko kwa Rais Bashar Hafez al-Assad iliyokabidhiwa asubuhi ya tarehe 22 Julai 2019 huko Damasco na Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma kwa Rais wa Siria.

Katika kuanza rasmi kazi ya Msemaji Mkuu wa vyombo vya habari Dk. Bruni amethibitisha juu ya barua ya Papa Francisiko kwa Rais Bashar Hafez al-Assad iliyokabidhiwa asubuhi ya tarehe 22 Julai 2019 huko Damasko katika mikono ya Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya maendeleo Fungamani ya Binadamu,akisindikizwa na Padre Nicola Riccardi,Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Kardinali Mario Zenari, Balozi wa Vatican nchini Siria mara baada ya kukutana na Rais Bashar Hafez al-Assad.

Dk. Bruni amesema kuwa wakati wa mkutano wao Kardinali Turkson amewza kumkabidhi Mkuu wa nchi ya Siria barua iliyoandikwa na Baba Mtakatifu na ambayo inaonesha juu ya wasiwasi wake wa kina kwa ajili ya hali halisi ya kibinadamu nchini Siria, kwa namna ya pekee hali halisi ya kutisha ya raia huko Idlib.

Shukrani kutoka kwa msemaji Mkuu mpya wa vyombo vya habari Vatican 

Aidha uthibitisho wa msemaji mkuu wa vyombo vya habari Dk. Matteo Bruni wakati wa kuanza rasmi majukumu yake, kama ilivyo kuwa imesema tarehe 22 Julai 2019 amesema: "Leo ninaendelea kutoa huduma kwa miaka hii kumi katika roho ya huduma ya Papa na Vatican, kwa uzoefu na jitihada zangu.” "Ninawashukuru wafanyazi wengine na rafiki Alessandro Gisotti, kwa ajili ya kuongoza kwa ukarimu na hekima kama msemaji wa vyombo vya habari katika miezi hii. Ninao utambuzi wa kazi nyeti  na maamuzi ya zoezi la  mawasiliano na kwa utambuzi kuwa, kwa hakika nitapata msaada kutoka kwa wafanyakzi wenzangu ambao nimejifunza taratibu kutambua thamani na taaluma zao  katika miaka hii ya kazi Vatican. Ninamshukuru Baba Mtakatifu kwa imani yake aliyo nipatia, pia Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Bwana Paulo Ruffini na msaada wa Baraza lote".

 

22 July 2019, 14:19