Kardinali Peter Turkson katika ujumbe wake katika fursa ya Siku ya Utalii Duniani 2019 unaofikia kilele chake 27 Septemba anakazia  juu ya kazi ya hadi haza katika kizazi kipya cha vijana Kardinali Peter Turkson katika ujumbe wake katika fursa ya Siku ya Utalii Duniani 2019 unaofikia kilele chake 27 Septemba anakazia juu ya kazi ya hadi haza katika kizazi kipya cha vijana 

Siku ya Utalii Duniani 2019:Utalii na kazi hali bora ya baadaye!

Tarehe 24 Julai 2019 Kardinali Turkson Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu ametoa Ujumbe wake kufuatia na fursa ya maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani 2019, inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 27 Septemba ya kila mwaka.Katika ujumbe huo anakazia juu ya kazi yenye hadhi,hasa kwa vijana.Papa Francisko anasema mahali ambapo hakuna kazi, haiwezekani kupata wakati endelevu ulio bora

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kuelekea fursa ya kilele cha Siku ya Utalii duniani 2019, ambayo inaadhimishwa kila ifikapo tarehe 27 Septemba  ya kila mwaka kwa kuandaliwa na Shirika la Utalii duniania (UNWTO), Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu ametoa ujumbe wake ukiangazia Kauli mbiu ya siku isemayo: “Utalii na kazi:hali bora ya baadaye kwa wote”. Ujumbe huo unaonesha kuandikwa tarehe 23 Julai 2019 ambapo  Kardinali Turkson anajikita kufafanua zaidi maana ya mada inayoongoza siku hiyo na ujumbe mbalimbali kutoka kwa mababa watakatifu katika kukazia juu ya kazi kwa ujumla katika ngazi zake zote, lakini zaidi hasa kwa vijana kizazi kipya.

Mada hii ni mapendekezo ya Shirika la Kazi duniani ILO

Kardinali Turkson amesema kuwa mada hii ni wito wa kazi ya baadaye kwa mujibu wa mapendekezo ya Shirika la Kazi  duniani ILO ambalo kwa mwaka huu linaadhimisha miaka 100 tangu kuanza kwake. Uchaguzi wa mada ya utalii kwa mantiki ya kazi, unajionesha kwa namna ya pekee katika fursa mbele ya ugumu unasimika mizizi na kuongezeka katika  tabia ya kufanya kazi ya maisha ya watu wengi kila kona. Lengo la matarajio  ya amani, usalama, uhamasishaji na upamoja kijamii haviwezi kufikiwa iwapo kuna dharau ya kufanya jitiha za pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kazi yenye hadhi, usawa, uhuru na ambao unajengwa kumzungukia mtu na mahitaji yake msingi ya maendelo fungamani, anaandika Kardinali Turkson. “Kufanya kazi ndiyo hali sawa kwa mwanadamu. Kazi inaelezea hadhi yake ya kuumbwa kwa sura na mfano wa Mungu”, alisema Baba Mtakatifu Francisko. Mahali ambapo hakuna kazi, haiwezekani kuwa na wakati endelevu ulio bora. Na ni kazi ambayo sio ya ajira tu, lakini ni njia ambayo mwanadamu anajitambua katika jamii na katika ulimwengu; kazi  ni sehemu muhimu katika kuamua maendeleo ya pamoja ya mtu na jamuiya anamoishi.

Tumeitwa kufanya kazi tangu kuumbwa kwetu

:“Tumeitwa kufanya kazi tangu kuumbwa kwetu”, anaadika Kardinali Turkson kwamba Baba Mtakatifu Francisko aliandika katika Wosia wake wa  Laudato si', akisisitiza  kwamba “Kazi ni jambo la lazima, ni sehemu ya maana ya maisha hapa duniani, njia ya kukomaa, ya maendeleo ya mwanadamu na kujikamilisha binafsi”, “Bila kazi, hakuna hadhi” aliongeza  tena katika ujumbe kwa njia ya video kwa washiriki wa Wiki ya 48 ya Jumuiya ya Wakatoliki nchini Italia huko Cagliari, Oktoba 2017,  Na kama inavyokumbusha maelezo ya Kitabu cha Mafundisho jamii ya Kanisa katoliki kwamba,  “Mtu ni kipimo cha hadhi ya kazi” na  akinukuu kutoka Wosia wa  Laborem exercens, anasema, “Kiukweli, hakuna shaka kuwa kazi ya mwanadamu ina thamani yake ya maadili, na ambayo bila kuwa na masharti yoyote inabaki moja kwa moja fungamani kwa maana ya kwamba yule anayetimizia hivyo ni mtu”. Na kwa namna ya pekee kuhusiana na Utalii , katika Ujumbe wa Siku ya XXIV ya Utalii duniani, Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa akielezea zaidi kuwa sekta hii “inapaswa kufukiriwa kama kieleleza kwa namna ya maisha ya kijamii, mwa mwamko wa kiuchumi, kifedha, kiutamaduni na kwa matokeo ya uamuzi wa yak ila mmoja na watu”. Aidha “Uhusiano wake wa moja kwa moja wa maendeleo fungamani ya mtu unapaswa kuelekeza huduma kama shughuli nyinginezo za kibinadamu, zinazojenga. ( Katekesi ya Papa Francisko tarehe 15 Agosti 2015).

Matatizo yanayohusiana na kazi katika sekta ya utalii mengi

Hadi leo kuna shida nyingi zinazohusiana na kazi katika sekta ya utalii, ambayo imegawanywa katika taaluma tofauti na kazi maalum. Washauri wa kusafiri na miongozo ya watalii, chef, wapishi na watoa huduma katika ndege , watumbuiza, wataalam wa uuzaji wa utalii na mitandao ya kijamii: wengi wao hufanya kazi kwa hali ya hatari na wakati mwingine kinyume cha sheria, na mishahara isiyofaa, wanalazimika kufanya kazi kwa bidii, na mara nyingi mbali na familia zao,  katika hatari kubwa ya kufadhaika kutokana na kushikilia kwa nguvu  sheria za ushindani mkali. Kufuatia na mambo kama hayo, ipo hali mbaya inayojihusisha na unyonyaji wa wafanyikazi katika nchi masikini na wakati huo  pakiwa na  wito mkubwa wa watalii kwa sababu ya urithi wa tajiri wa mazingira na kihistoria ambao unawatambulisha, na mahali ambapo ni nadra sana kufaidika  watu wa kiasili na utumiaji wa rasilimali mahalia.

Vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wakazi mahalia havikubaliki

Hata hivyo vitendo vya unyanyasaji dhidi ya idadi ya wakazi mahalia pia havikubaliki, hasa kudharauliwa utambulisho wao wa kitamaduni na shughuli zote zinazosababisha udhalilishaji na unyonyaji mkubwa wa mazingira. Katika suala hili, bado kunako mwaka  2003, Mtakatifu Yohane Paulo II, alisema kwamba, “shughuli za watalii zinaweza kuchukua jukumu muhimu katika mapambano dhidi ya umasikini, iwe  kwa mtazamo wa kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Katika kusafiri, anasema, tunajua maeneo na hali tofauti na tunagundua ni kwa jinsi  gani kuna pengo kubwa kati ya nchi tajiri na nchi masikini. Aidha inawezekana  kuthamanisha rasilimali na shughuli mahalia kwa kuhamasisha ushiriki wa sehemu za maskini zaidi ya watu”.Katika mantiki hii, ikiwa tutaangalia kwa karibu uwezo wa maendeleo unao tolewa na na sekta ya utalii, lazima kuzingatiwa iwe suala la fursa za ajira na ambazo zinahamasisha kibinadamu, kijamii na kitamaduni. Fursa ambazo ziko wazi kwa  kufungulia  kwa namna ya pekee vijana na ambazo zinahimiza ushiriki wao kama msatari wa mbele katika maendeleo yao, labda kupitia jitihada za kuanzisha ujasiriamali katika nchi zisizo kuwa na fursa.

Takwimu zilizotolewa na Shirika la Utalii Duniani UNWTO

Takwimu zilizotolwa na Shirika la Utalii Duniani I (UNWTO) Kardinali Turkson anathibitisha kuwa kwamba kati ya nafasi kumi na moja ya kazi duniani angalau moja tu  imetokelewa n utalimoo  moja kwa moja au kinyume chek na kuorodhesha tukio la kuongezeka mara kwa moaja ambalo linawahusu miolini ya watu katika kila kona ya ardhi. Hii ina maana ya kuzungumzia mzunguko mkubwa na athari kubwa kwa kiwango cha kijamii, kiuchumi na kiutamaduni, ambacho kimezidi matarajio yake  zaidi. Inatosha kkufikiria kwamba kunako mwaka 1950 watalii wa kimataifa walikuwa karibu zaidi ya milioni 25, wakati katika muongo utakaofuata  inakadiriwa kuwa inawezekana kufikia idadi ya wasafiri bilioni 2 ulimwenguni kote. Mbele ya mtititiko huo unajionesha mwelekeo wa kutiwa moyo katika ukuu wa mkutano  ambao kazi ya utalii inaweza kutoa. Wahudumu wa sekta katika ngazi zote, katika utendaji wa kazi zao za kila siku, katika visa vingi, wanapata fursa yakukabiliana na watu kutoka nchi tofauti zaidi za ulimwenguni, na kuanza mchakato wa kufaafamiana ambao ni hatua ya kwanza kwa kuacha hukumu  na ubaguzi na kwa ajili ya  kujenga uhusiano unaotegemea urafiki.

Baba Mtakatifu anasema, utalii ni kama fursa ya kukutana na kukuza dhamiri na kujenga urafiki

Baba Mtakatifu Francisko akihutubia vijana wa Kituo cha Kitalii cha Vijana mwezi Machi 2019, katika hafla ya kuadhimisha miaka 70 ya kuanzisha Chama hicho, alizungumzia juu ya utalii kama fursa ya kukutana. Alitoa shukrani zake kwa kujitolea kwao katika kukuza “utalii mwepesi”, ambao hauchochewi na kanuni za ununuzi au kutaka tu kukusanya tu uzoefu, lakini wenye uwezo wa kupendelea kukutana  kati ya watu na eneo, na kufanya kukua katika dhamiri ya maarifa na kuheshimiana. Kutokana na hiyo Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu inatoa  wito kwa watawala wote na wale wahusika  wa sera za kisiasa kitaifa na  kiuchumi ili kuhimiza kazi, kwa namna ya pekee miongoni mwa vijana, katika sekta ya utalii. Iwe kazi ambayo inazingatia hadhi ya mtu  kama vile inavyopendekezwa na  Tume ya Dunia juu ya mustakabali wa Kazi endelevu wa Shirika la Kazi duniani (ILO)  na  ambayo ni  chombo cha kukuza maendeleo fungamani ya kila mtu na ya watu wote.  Kwa kufanya hivyo itawezekana kushirikiana na maendeleo ya jumuiya  moja, kila moja kulingana na mantiki yake na ambayo inasaidia kuunda uhusiano wa urafiki na udugu kati ya mtu na watu.

Uhakika wa ukaribu kwa wote wanaojikita kutimiza malengo 

Kardinali Turkson anasema kwamba, “Tunawahakikishia ukaribu wetu na msaada kwa wote ambao wamejikita kutimiza malengo haya na tunawasihi wasimamizi na wadau wa utalii wawe na ufahamu juu ya changamoto na fursa zenye tabia ya kazi katika tasnia ya utalii". Aidha anaongeza kusema, "hatimaye, tunapenda  kuwashukuru wafanyakazi wa kichungaji kwa ajili ya  juhudi zao zote za kila siku za kuhakikisha kwamba Neno la Mungu linaenea na kuangaza na kutoa uhai katika kila uwanja huu wa kipekee wa maisha ya mwanadamu".

24 July 2019, 14:03