Tafuta

Vatican News
Tarehe 22 Julai Kardinali Turkison akiambatana na wajumbe wengine wawili amekutana na Rais wa Siria na kumkabidhi Barua ya Papa Rais Asaad Tarehe 22 Julai Kardinali Turkison akiambatana na wajumbe wengine wawili amekutana na Rais wa Siria na kumkabidhi Barua ya Papa Rais Asaad  (ANSA)

Parolin:Papa anaomba Al-Assad matendo ya dhati kwa ajili ya watu!

Vita vinaendelea na mabomu yamesababisha majanga makubwa kwa watu wengi.Uharibifu au kufungwa kwa majengo ya afya huko Idlib.Kwa maana hiyo Papa ametuma barua kwa Rais wa Siria kwa njia ya mikono ya Kardinali Turkson.Kardinali Pietro Parolin,Katibu wa Vatican anaelezea yaliyomo ndani ya barua hiyo akihojiana na Vatican News!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kulinda maisha ya raia, kusitisha majanga ya kibinadamu katika kanda ya Idlib ndiyo mambo muhimu na ya dhati kwa ajili ya kuweza kuingia kwa usalama watu walio rundikana, kuwaachia huru wafungwa na kuachia familia ziweze kuwa na mawasiliano na wapendwa wao, hali za kibindamu kwa wafungwa wa kisiasa. Pamoja  na upyaisho wa tamko la ujmbe kwa ajili ya kurudia mazungumzo na mchakato wa ushiriki wa jumyia ya kimataifa. Haya yote ndiyo wasiwasi mkubwa na maombi ya dhati ambayo yamo ndani ya Barua ya Baba Mtakatifu Francisko aliyependelea kumwandikia Rais wa Siria, Bwana Bashar Hafez al-Assad.

Kardinali Turkson amemkabidhi Rais Assad barua ya Papa

 

Sahihi ya barua ya Papa inaonesha kuandikwa tarehe 28 Juni 2019 na  ambayo imeweza kufikishwa na Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson, Rais wa Braza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya Watu. Kardinali Turkison akiwa na Barua iliyo andikwa kwa lugha ya kingereza alikuwa amesindikizwa na  Padre Nicola Riccardi, O.F.M., Katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya Watu na Kardinali Mario Zenari, Balozi wa Vatican nchini Siria. Na kuhusiana na yote yaliyomo ndani ya Barua hiyo, Vatican News imehojiana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican ambaye ndiye mhudumu wa kwanza wa Papa Francisko!

Kwanini Papa ameamua kumwandikia Rais Assad?

Chimbuko la kuanzishwa suala hili jipya ni kutokana na wasiwasi mkubwa wa Baba Mtakatifu Francisko na Vatican kwa ujumla  kutokana na hali halisi ya dharura ya kibinadamu nchini Siria kwa namna ya pekee katika wilaya ya Idlib, anasema Kardinali Parolin. Katika eneo ambalo wanaishi watu zaidi ya milioni 3 na kati yao milioni 1,3 wamerundikana ndani, huku wakilazimika kuishi kwa muda mrefu na migogoro nchini Siria; na wakati huo huo wakitafuta mahali pa kukimbilia sehemu ambayo ilikuwa imethibitishwa kuwa imekombolewa mwaka jana. Hivi karibuni anasema, wanajeshi wameelezea kuwa hali ya maisha ni ya kutisha katika makambi na kulazimisha wengi wao kukimbia. Papa anafuatilia kwa uangalifu mkubwa, akiwa na uchungu juu ya janga hili la kutisha la raia, hasa watoto ambao wameona umwagaji wa damu kutokana na mapigano. Kwa bahati mbaya vita vinaendelea na wala havisimami, mabomu yanaendelea, majengo yameharibiwa katika maeneo mengi hata yale ya afya, wakati wengine wamelazimika kusimamisha kila kitu au karibu shughuli zao.

Papa anaomba nini kwa Rais Assad katika barua aliyokabidhiwa?

Kardinali Parolin amesema kuwa, katika barua, Baba Mtakatifu Francisko, anarudia kutoa wito wake  ili uweze kuwapo ulinzi wa maisha ya raia na wakati huohuo kuweza kuimarisha misingi ya majengo, kama vile mashule, hospitali na majengo ya vituo vya Afya. Kiukweli, kile kinacho endelea kutokea, siyo kitu cha kibinadamu na hakikubaliki. Baba Mtakatifu anaomba Rais afanye kila iwezekanavyo ili kusimamisha majanga haya ya kibinadamu na zaidi kuwalinda watu wengi mno kwa namna ya pekee walio wadhaifu zaidi kulingana na Haki za kibinadamu kimataifa.

Kile ulichokieleza,inaonesha kuwa nia ya kuanzisha hatua hii mpya ya kipapa  siyo suala la kisiasa. Ndiyo hivyo?

Kardinali Parolin akijibu juu ya nia ya kipapa siyo sula la Kisiasa na  hivyo anasema: Ndiyo hivyo kwamba, kuwa kama  ambavyo nimekwisha elezea, wasiwasi ni ule wa kibinadamu. Papa anaendelea kusali ili nchi ya Siria iweze kupata hali halisi ya kidugu mara baada ya miaka mingi hii ya vita na kwamba mapatano yaweze kushinda migawanyo na chuki. Katika barua yake, Baba Mtakatifu analitumia neno upatanisho kwa mara tatu. Na hilo ndilo longo lake kwa ajili ya wema wa nchi na watu wake wengi. Baba Mtakatifu Francisko anamtia moyo Rais Bashar al-Assad ili aweze kutimiza ishara yanye maana katika mchakato muhimu wa mapatano na kuwa mfano wa hatua hiyo. Anataja kwa mfano, hali halisi kwa ajili ya kuweza kuingia kwa salama watu wanaoteseka na wale ambao wamerundikana ndani; kwa ajili ya wale ambao wanataka kurudi katika nchi yao mara baada ya kulazimika kuikimbia. Aidha anataja pia kuwachiwa huru wafungwa na familia ziweza kupata mawasiliano na habari juu ya wapendwa wao.

Mada nyingine muhimu ni ile ya wafungwa wa kisiasa. Papa anasemea kidogo hilo?

Kardinali Parolin anajibu kuwa: Ndiyo Papa Francisko kwa namna ya pekee suala la hali ya wafungwa wa kisiasa, lipo rohoni mwake na ambapo anathibitisha kwamba, haiwezekani kukataa hali za kibinadamu. Kunako mwezi Machi 2018, Tume ya Kimataifa ya Uchunguzi inayo egemea katika Jamhuri ya Kiarabu ya Siria ilichapisha ripoti juu ya suala hili, ikizungumzia makumi ya maelfu ya watu waliowekwa kizuizini. Wakati mwingine katika magereza isiyo rasmi na katika sehemu zisizojulikana, na wengi wao waliweza kuteswa kwa aina tofauti za mateso bila kuwa na msaada wowote wa kisheria au kuwasiliana na familia zao. Ripoti hiyo inabaini kuwa wengi wao kwa bahati mbaya wanakufa gerezani na wengine huwawa kwa muda mfupi.

Je! Nini madhumuni ya mpango huu mpya wa Papa Francisko ?

Kardinali Pietro Parolin anajibu kwamba, Vatican  imeendelea kusisitiza juu ya hitaji la kutafuta suluhisho la kisiasa linalofaa kumaliza mzozo, kushinda na kuweka pembeni masilahi binafsi. Na hii lazima ifanyike na zana za kidiplomasia, majadiliano na mazungumzo, kwa msaada wa jumuiya  ya kimataifa. Aidha amesema ilibidi tujifunze tena kuwa vita inaita vita na vurugu huita vurugu, kama vile Papa alivyosema mara nyingi na kama anavyorudia katika barua hiyo. Kwa bahati mbaya, Kardinali Parolini amesema: tuna wasiwasi juu ya kusitishwa kwa mchakato wa mazungumzo, hasa ule wa Geneva, kwa ajli ya  suluhisho la mzozo huo  wa kisiasa. Kwa sababu hii, katika barua iliyotumwa kwa Rais Assad, Baba Mtakatifu anamtia moyo ili kuonyesha nia njema na kufanya kila liwezekanalo ili kupata suluhisho linalowezekana, kukomesha mzozo ambao umechukua muda mrefu sana na umesababisha upotezaji wa idadi kubwa ya maisha yasiyokuwa na hatia.

22 July 2019, 16:14