Tafuta

  Dk.Cristiane Murray ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Msemaji mkuu msaidizi wa Vatican Dk.Cristiane Murray ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Msemaji mkuu msaidizi wa Vatican  

Papa amemteua Dk.Cristiane Murray kuwa Msemaji mkuu msaidizi wa Vatican!

Tarehe 25 Julai 2019 Baba Mtakatifu Francisko amemteua Cristiane Murray kuwa Msemaji Mkuu msaidizi wa Vatican.Alizaliwa huko Rio de Janeiro,nchini Brazil kunako 1962.Ni mama mwenye familia ya watoto wawili.Tangu mwaka 1995 anafanyakazi Radio Vatican.Na kuanzia Aprili 2018 anashiriki katika maandalizi ya Sinodi maalum kwa ajili ya Amazoni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Dk. Cristiane Murray kuwa Msemaji Mkuu msaidizi wa Vatican. Alizaliwa tarehe 10 Machi 1962 huko Rio de Janeiro (Brasili). Amepata shahada ya Utawala wa Biashara na Uuzaji katika Chuo Kikuu Katoliki cha Kipapa cha Rio de Janeiro.Tangu Novemba 1995 anafanya kazi Radio Vatican. Kunano  2018 anashirikiana na Sekretarieti Kuu ya Sinodi Maaskofu kuandaa Sinodi Maalum ya Kanda ya Amazoni ijayo.

Dk. Murray anashukuru Baba Mtakatifu,viongozi na wafanyakazi wenzake

Naye Dk. Cristiane Murray katika tamko lake la kwanza mara baada ya uteuzi huo amesema kwamba amepokea habari hiyo kwa mshangao mkubwa! Na kwa waandishi wa habari wenzake wa Baraza la Mawasiliano Vatican, ni furaha kubwa ya utambuzi huu wa kazi yake ya kila siku ya kupeleka Injili duniani kwa njia ya ujumbe wa Papa na Kanisa. Aidha akitoa shukurani zaidi kwa Baba Mtakatifu Francisko Bi Murray awali ya yote anatoa shukrani zake, kadhalika anawataja wanawake waliomchagua katika nafasi hii muhimu. Anamshukuru Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasilinao Dk. Paolo Ruffini, Mkurugenzi  wa uhariri Vatican, Dk. Andrea Tornielli na Katibu Mkuu wa Sinodi inayo ongozwa na Kardinali Lorenzo Baldisseri ambaye amefanya kazi naye karibu mwaka mzima kwa kuandaa shughuli ya Sinodi ya Amazoni ijayo. Anatoa ahadi ya kufanya kila jitihada na shauku yake kwa Msemaji Mkuu wa wa Vatican, Dk. Matteo Bruni na kikundi chote cha Ofisi ya  Waandishi katika  huduma mjini Vatican.  

Uthibitisho wa Dk. Paolo Ruffini:uchaguzi wa mwanamke na mzizi kutoka Brazili ni ufunguzi katika dunia

Naye Dk. Paulo Ruffini Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano anasema,“kufuatia na Baba Mtakatifu Francisko kumteua Cristiane Murray kuwa Msemaji mkuu msaidizi wa Vatican, unatimizwa mchakato mzima wa viongozi wakuu katika muundo  kwa ujumla wa Baraza la kipapa la Mawasiliano. Uchaguzi wa mwanamke na mzizi kutoka Brazil na mtazamo wa ufunguzi wazi katika dunia, unashuhudia ule utashi wa kujenga na mapenzi ya kutambua kuzungumza lugha kwa yule anaye tusikiliza”. Aidha Dk. Ruffini ameongeza kusema: "Ninao uhakika kuwa Cristiane ambaye kwa miaka mingi anafanya kazi katika vyombo vya habari Vatican na ambaye taaluma na ubinadamu zimethaminiwa kila wakati, zitatoa mchango ulio msingi wa akili, usikivu, kumbukumbu na mipango katika huduma ambayo sisi sote tunajaribu kuitoa katika Kanisa”.

Uthibitisho wa Mhariri Mkuu wa Matangazo Dk. Andrea Tornielli

Naye Mhariri Mkuu wa Matangazo ya Radio Vatican, Dk. Andrea Tornielli anasema, “Ninamshukuru Baba Mtakatifu kwa kumchagua  Braziliani Cristiane Murray kuwa msemaji mkuu msaidizi wa Vatican. Hadi leo hii Cristiane amekuwa rasilimali muhimu kwa ajili ya gazeti la  Radio Vatican, (Vatican News), pia anathaminiwa na Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu,mahali ambapo ametoa huduma zaidi ya mwaka mmoja akishirikiana kuandaa Sinodi kwa ajili ya Kanda ya Amazoni. Ni kwa mara nyingine taaluma ya ndani inatambulikana katika vyombo vya habari vya Vatican, nina uhakika kuwa uwezo wa Cristiane utathaminiwa sana kwa ajili ya  kazi ya Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican”. amesema Dk Tornielli.

Uthibitisho wa Msemaji Mkuu wa Vatican Dk. Matteo Bruni

Naye Msemaji Mkuu  wa Vatican Vatican  Dk. Matteo Bruni kufuatia na kuteuliwa kwa makamu wake amethibitisha:"Ofisi ya vyombo vya habari inapokea kwa shukrani na utambuzi wa Baba Mtakatifu kumteua Cristiane Murray  kuwa msemaji msaidizi wa Vatican. Nina uhakika kuwa taaluma yake na uzoefu uliokomaa katika miaka hii ya huduma kwa ajili ya Kanisa na Vatican, vitakuwa na thamani kubwa katika jukumu jipya hili. Na pia kwa niaba ya Wafanyikazi wa Ofisi ya Vyombo vya Habari, nina mkaribishwa kwa furaha kubwa wakati huo huo nikimtakia ufanisi wa kazi nzuri”. Amesema Dk.Bruni.

25 July 2019, 13:27