Tafuta

Itifaki ya Mkataba wa makubaliano kati ya Vatican na Serikali ya Watu wa Congo-Brazzaville imeanza kutumika rasmi baada ya nchi hizi mbili kubadilishana nyaraka za kutendea kazi! Itifaki ya Mkataba wa makubaliano kati ya Vatican na Serikali ya Watu wa Congo-Brazzaville imeanza kutumika rasmi baada ya nchi hizi mbili kubadilishana nyaraka za kutendea kazi! 

Itifaki ya Makubaliano: Vatican & Congo Brazzavile yaanza rasmi

Kardinali Pietro Parolin na Jean-Claude Gakosso, Siku ya Jumanne, tarehe 2 Julai 2019 wameshuhudia mwanzo wa utekelezaji wa Itifaki ya Makubaliano kati ya Vatican na Serikali ya Congo Brazzaville, uliotiwa sahihi tarehe 3 Februari 2017. Tukio hili limehudhuriwa pia na Bwana Jean-Claude Gakosso, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Congo Brazzaville.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kardinali Pietro Parolin Katibu mkuu wa Vatican akiwa ameambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican, Jumanne, tarehe 2 Julai 2019 wameshuhudia mwanzo wa utekelezaji wa Itifaki ya Makubaliano kati ya Vatican na Serikali ya CongoBrazzaville, iliotiwa sahihi tarehe 3 Februari 2017. Tukio hili limehudhuriwa pia na Bwana Jean-Claude Gakosso, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Congo Brazzaville.

Viongozi hawa wamebadilisha nyaraka za utekelezaji wa makubaliano kati ya Vatican na Serikali ya Congo Brazzavile kuhusu uhusiano wa Kanisa Katoliki na Serikali ya Congo Brazzavile. Katika muktadha huu, Serikali kwa sasa inawatambua kisheria viongozi wa Kanisa pamoja na taasisi zake pamoja na kutoa nafasi kwa Kanisa kuweza kutekeleza dhamana na utume wake nchini humo. Pande hizi mbili zitashirikiana kwa kuzingatia mipaka yake kisheria kwa ajili ya: utu, heshima, haki msingi za binadamu, ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Congo Brazzavile.

Congo Brazzaville
03 July 2019, 15:27