Kard.Parolin anakumbusha wajibu wa kulinda daima maisha katika juhudi za Hospitali ya Bambino Gesù!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Inawezakana kutenda wema na kuutenda vema. Hii inajionesha katika idadi kubwa ya shughuli za afya na kisayansi kwenye takwimu za ripoti ya mwaka 2018 ya Hospitali ya kipapa ya Watoto “Bambino Gesu”, iliyowakilishwa tarehe 24 Julai 2019 katika makao ya Mtakatifu Paulo jijini Roma. Mkutano huo umefunguliwa na Rais wa Hospitali hiyo Bi Mariella Enoc ambaye baada ya utambulisho imefuatia hotuba ya Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican.
Hotuba ya Kardinali Pietro Parolin
Katika hotuba yake Kardinali Pietro Parolin anasema, matokeo yaliyopatikana yako mbele ya macho ya wote na kuwapongeza wale wote ambao wametoa mchango wao kutimiza ufanisi huo. Katika fursa ya maadhimisho ya miaka 150 tangu kuanzishwa kwa Hospitali ya Bambino Gesù, Baba Mtakatifu Francisko katika barua yake alionesha kuwa “anayekita kutoa matibabu kwa walio wadogo zaidi yuko katika sehemu ya Mungu na anashinda utamaduni wa kibaguzi”. Katibu wa Vatican amekumbuka maneno ya Baba Mtakatifu huku akitafakari matokeo ya ufanisi wa jengo la Afya la Vatican. Ni ripoti bora zaidi inayohusu shughuli za afya, shughuli za kisayansi na ripoti ya kijamii ikiwa na mipango yake ya kibinadamu katika nchi 10. Kardinali Parolin amewaalika wasisimame kamwe! “Ni muhimu kwamba lengo hili bora lisijikunjike na tusisahau kamwe kuwa thamani ya mafanikio yaliyopatikana hupimwa katika uwezo wa kuboresha ubora wa utunzaji na usaidizi. Watoto, vijana na familia zao wako na lazima wabaki katika mioyo ya kila shughuli, kila mchakato na kila hatua inayofanywa”.
Wazo kwa ajili ya Vincent Lambert: kulinda maisha daima
Hata hivyo katika hotuba yake, Kardinali Parolin amewaalika “kushinda hatari ya migawanyiko na ukimbele mbele na kuwashauri kila mmoja ajikite katika nafasi yake kwa utambuzi na unyenyekevu”. Na akigusia juu jambo la Vincent Lambert amekumbusha kuwa ndani ya usimamizi imara na busara, inawezekana kukuza uendeshaji. Aidha , “Ninafikiri kazi iliyoanzishwa kwa ajili ya Taasisi ya Saratani na Upandikizaji wa viungo au kubuni chumba cha kukaa watoto wachanga; ni kwa jinsi gani katika siku hizi kuwa muhimu sana na zaidi baada ya kifo cha Vincent Lambert, ambaye ameamsha tena ndani mwetu kumbukumbu ya watoto Alfie Evans na Charlie Gard. Kwa maana hiyo ameongeza kusema”,kutokana na hiyo ameongeza kusema: “ tunalo jukumu la kuthibitisha kuwa kuna magonjwa ambayo hayaponi, lakini hakuna magonjwa yasiyoweza kutibika. Na ili kuweza kutibu haina maana tu ya kuponyesha lakini hata ile ya kusindikiza na kulinda. Na kama alivyothibitisha Baba Mtakatifu Francisko wakati akionesha uchungu wake wa tukio hilo alisema: “ Ni mungu peke yake mkuu wa maisha kuanzia mwanzo hadi kifo cha kawaida, ni wajibu wetu kuyalinda maisha daima”.
Kuhusiana na wasiwasi wa kibinadamu nchini Siria
Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin akijibu swali kando ya mkutano huo kwa mwandishi wa habari kuhusiana na mada ya Siria na barua ya Baba Mtakatifu iliyomfikia Rais wa Siria Assad, amerudia kusema yale ambayo tayari alikuwa amethibitisha katika mahojiano na Vatican news, kuhusu wasiwasi wa Vatican ambao ni mkubwa kwa ajili ya maisha ya kibinadam nchini humo.
Shughuli za kliniki na kisayansi
Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Afya Massimiliano Rapon na Mkurugenzi wa Kisayansi Bruno Dallapiccola na Murugenzi Mkuu Ruggero Parrotto wakati wa uwakilishaji wa shughuli zao, wamewekwa mwanga zaidi kuhusu matokeo mema ya Hospitali ya Vatican. Bambino Gesù kwa hakika imepiga hatua kubwa hasa kuwa karibu na milioni mbili ya vituo nje vya kutoa huduma na wakati huo huo wagonjwa wa kulala ni 29,000. Kwa kuongezea zaidi kile kitengo cha kupandikiza viungo. Kwa hakika hii ni hospitali pekee katika bara la Ulaya yenye uwezo wa kujibu hitaji la aina yoyote ya kupandikiza viungo na ambayo imejitofautisha na shughuli za operesheni 324 za seli na tishu.
Hata hivyo pia imejihusisha kuonesha matokeo katika matibabu ya magonjwa nadra au adimu, kwa kesi za magonjwa mapya 21 adimu yaliyotambuliwa na zaidi ya wagonjwa 13,000 wenye magonjwa yasiyo ya kawaida waliyo fuatilia. Katika jitihada hizi inaongezeka hata kazi kubwa ya utafiti na ambayo imewezesha kutoa uchapishaji wa makala 679, kwa kukadiriwa na vidokezo vya 2968 vya Impact Factor Raw (IFG), yaani njia ya kupima thamani ya masomo ya kisayansi yaliyozalishwa. Kwa maana hiyo ni Shukrani kwa Taasisi yenye kushika nafasi ya tatu katika mtandao wa Taasisi za Hopitali za kulala na utunzaji zenye kuwa na tabia ya Hospitali ya kisayansi (IRCCS) na ni ya kwanza kati ya hospitali za watoto nchini Italia.
Ni Hospitali ya makaribisho
Hospitali ya watoto Bambino Gesù inakaribisha karibia familia zenye wagonjwa wa kulala 4,500 na 2,100 wa familia zinazofuatiliwa na huduma ya kijamii. Ni wagonjwa 62 wa msaada wa kibinadamu walio karibishwa kutoka nchi 68. Hii ni ishara ya kuwa hospitali hiyo ni wazi, inayokaribisha na kuwa na mshikamano. Na katika kusheherekea mafanikio hayo na miaka 150 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo, tarehe 20 Novemba ijayo, wanatarajia kuandaa tukio liitwalo: usiku wa nyota za mtoto Yesu (le stelle del Bambino Gesu’) katika Ukumbi wa Paulo VI , kwa lengo la kukusanya fedha za ujenzi wa Taasisi mpya ya Saratani na upandikizaji wa viungo.