Tafuta

Papa Francisko amewateua Dr. Sergio Centofanti na Dr. Alessandro Gisotti kuwa Wahariri wakuu wasaidizi, Idara ya Uchapaji ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Papa Francisko amewateua Dr. Sergio Centofanti na Dr. Alessandro Gisotti kuwa Wahariri wakuu wasaidizi, Idara ya Uchapaji ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano. 

Dr. S. Centofanti & Dr. A. Gisotti: Wateuliwa kuwa Wahariri wakuu wasaidizi

Papa Francisko amewateua Dr. Sergio Centofanti na Dr. Alessandro Gisotti kuwa ni Wahariri wakuu wasaidizi, Idara ya Uchapaji ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Uteuzi huu unaanza tarehe 22 Julai 2019. Dr. Paolo Ruffini pamoja na Wafanyakazi wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano wanawatakia heri na baraka katika utume huu mpya waliokabidhiwa na Baba Mtakatifu Francisko.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Dr. Sergio Centofanti na Dr. Alessandro Gisotti kuwa ni Wahariri wakuu wasaidizi, Idara ya Uchapaji ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Uteuzi huu unaanza tarehe 22 Julai 2019. Wafanyakazi wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano wanawatakia heri na baraka katika utume huu mpya waliokabidhiwa na Baba Mtakatifu Francisko. Dr. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano katika tamko lake baada ya uteuzi huu wa Baba Mtakatifu Francisko anasema kwamba, Baba Mtakatifu ameonesha kuthamini mchango mkubwa wa rasilimali watu iliyoko kwenye Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii, hatua kubwa katika mchakato wa mageuzi ndani ya Baraza hili. Baba Mtakatifu amemteua Dr.  Matteo Bruni, kuwa Msemaji mkuu wa Vatican. Huyu ni kiongozi anayefahamu kikamilifu shughuli na utendaji wa Ofisi ya Msemaji mkuu wa Vatican.

Ni kiongozi ambaye amebahatika kupata ujuzi na uzoefu mahali pa kazi. Ni kiongozi ambaye pia amebahatika kuwa na karama za kibinadamu, weledi, ujuzi na maarifa ya kazi zake. Ofisi hii itaweza kukamilika baada ya Baba Mtakatifu kumteua Msemaji mkuu msaidizi wa Vatican. Hata hivyo Dr. Paolo Ruffini ana matumaini makubwa kwamba, Dr. Matteo Bruni ataweza kutekeleza vyema dhamana na majukumu yake, akiendelea kutumia: uzoezi, mang’amuzi, busara, mwono mpana pamoja na kuthamini umoja katika utekelezaji wa shughuli za Vatican kwa kuhakikisha kwamba, daima anajitahidi kutoa habari za kweli na zenye uhakika!

Itakumbukwa kwamba, mwezi Desemba 2018, Baba Mtakatifu Francisko alimteuwa Dr. Andrea Tornielli kuwa Mhariri Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Ili kuweza kuratibu vyema shughuli zinazotekelezwa na Idara ya Uchapaji ya Vatican, LEV, Gazeti la L’Osservatore Romano pamoja na Vatican Media, Baba Mtakatifu amewateua Dr. Sergio Centofanti na Dr. Alessandro Gisotti kuwa ni Wahariri wakuu wasaidizi, Idara ya Uchapaji ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Lengo kuu ni kuendelea kuboresha huduma ya mawasiliano ya jamii inayotolewa na vyombo vinavyomilikiwa na kusimamiwa na Vatican. Itakumbukwa kwamba, Dr. Alessandro Gisoti, kwa muda wa miezi sita amekuwa Msemaji mkuu wa muda wa Vatican. Lakini hata katika kipindi hiki kifupi, ameweza kutekeleza majukumu makubwa yaliyohitaji nguvu ya ziada ili kuweza kutekeleza kwa ufanisi mkubwa, kwa kujisadaka bila ya kujibakiza na kuhakikisha kwamba, weledi na uzoefu unafanyiwa kazi kikamilifu. Dr. Alessandro Gisoti, amechangia kwa kiasi kikubwa katika maboresho ya Ofisi ya Msemaji mkuu wa Vatican.

Dr. Ruffini

 

18 July 2019, 15:25