Tafuta

Jubilei ya dhahabu ya SECAM Jubilei ya dhahabu ya SECAM 

Askofu Mkuu Rugambwa:Furaha na matumaini kwa miaka 50 ya SECAM!

Askofu Mkuu Protace Rugambwa,Katibu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu amekazia juu ya furaha na matumaini ya miaka 50 tangu kuundwa kwa Shirikisho la SECAM.Ni matashi yake kwa wote waweze kuchota na kuendeleza kazi ya utume kwa kufuata miongozo ya maneno ya Mtakatifu Paulo VI;ya Wosi wa Ecclesia in Africa wa Mtakatifu Yohane Paulo II kunako 1994 na ule wa Africae Munus,2009 wa Papa Papa Benedikto XVI.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wakati wa kutoa hotuba yake Askofu Mkuu Protase Rugambwa, Katibu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishi wa watu mjini akiwa mjini Kampala, tarehe 21 Julai 2019 katika fursa ya Mkutano Mkuu 18 wa SECAM na ambao unahimitimisha maadhimisho ya Jubilei ya dhahabu tangu kuanza kwa shirikisho hilo amesema kuwa, “Jubilei hii ni sababu ya furaha na matumaini. Furaha kwa ajili ya zawadi na neema iliyopokelewa kwa miaka 50 hii na matumaini kwa ajili ya kazi ya kutimiza na neena ya Mungu katika miaka mingine ijayo”.

Kuundwa kwa SECAM ni ishara ya dhati ya Mungu kwa Kanisa barani Afrika

Kuundwa kwa SECAM  anasema Askofu Mkuu Ryugambwa kuwa ilikuwa ni, na inabaki kuwa  ishara ya dhati ya Mungu kwa ajili ya Kanisa barani Afrika. Na Shirikisho linaweza kuwa lenye nguvu kubwa kwa ajili ya wakati ujao wa Kanisa katika bara na kwa maana hiyo,  anapendelea kwa moyo wake wote kwamba, maadhimisho ya miaka hiyo iwe ishara kwa ajili yao na kwa ajili ya Kanisa zima  la Afrika katika  kutafakari juu ya upyaisho wa kiroho na kichungaji. Na kwa katika kuchota kutoka katika visima vya waanzilishi wa SECAM, leo hii wafanye kuwa Injili ya Kanisa  iwe kisima cha matumaini kwa ajili ya watu wa Afrika.

Kanisa, familia ya Mungu Afrika

Kauli mbiu ya maadhimisho ya Jubulei ni, “Kanisa, familia ya Mungu Barani Afrika; Sherehekea Jubilei yako!Mtangaze Kristo Yesu Mkombozi wako, ambapo ameongeza kusema hii inakwenda sambamba na Mkutano maalum kwa ajili ya Afrika wa Sinodi  ya maaskofu iliyofanyika mjini Roma  kunako 1994 na  ya mwaka  2009, kwa kuhitimishwa na tangazo la Wosia wa  Kitume wa Kanisa la Afrika (Ecclesia in Africa) wa Mtakatifu Yohane Paulo II   na Africae Munus 2009 wa  Papa Benedikto XVI.

Kauli mbiu ya jubilei amesisitiza, inadumisha uhusiano maalum kati ya wakati uliopita na wakati uliopo  kwa kutoa mwaliko wa utume wa Kanisa katika bara la Afrika. Kwa kuzingatia sura ya Kanisa, familia ya Mungu kwa namna ya pekee inayostahiki katika  uinjilishaji wa Afrika, Askofu Mkuu Rugambwa ametaja mtazamo wa Mtakatifu Yohane Paulo II ambapo alitoa matashi mema ya ushirikiano wa kitaalimungu wa Kanisa  na familia katika utajiri wake wote kwa namna ya mantiki hiyo. Na kwa upande wa Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI , alisema, inahitahi jitihada za kuonesha thamani za muumba alizoziweka katika mioyo ya waafrika katika usiku wa nyakati.

Kumbukumbu ya ziara ya Papa Paulo VI kunako 1969

Askofu Mkuu Rugambwa amekumbusha pia  juu ya ziara ya kwanza ya Papa  Barani Afrika kunako mwaka 1969, wakati Mtakatifu  Paulo VI aliweza kushuhudia hitimisho la Mkutano wa Shirikisho la Maaskofu wa Afrika na kuwaweka wakfu maaskofu wazalendo, wakati huo huo na kutoa heshima kwa Wafiadini wa Uganda ambao yeye mwenyewe alikuwa amewatangaza kuwa watakatifu kunako mwaka 1964 na kutoa sakrameti ya ubatizo na kipaimara kwa wakristo wapya 22 wa Afrika. Katika tukio hilo Mtakatifu  Paulo VI alitoa ujumbe wake wa nguvu na ambao ulitakiwa kupelekwa katika Kanisa lote la Afrika na kuwa na dhamiri yake nyoofu na kazi yake ndani ya bara, ambapo alisema: “ ninyi waafrika kwa sasa mko tayari, ni wamisionari wenyewe”.

Umuhimu wa utamadunisho

Kuthamanisha utamaduni wa Afrika amba leo hii unajikita katika mantiki ya utamadunisho ndiyo ulikuwa kiini msingi cha shughuli za kuchungaji za Mtakatifu Paulo VI na siyo kwa Afrika tu,  lakini hasa hasa kwa ajili ya Afrika amebainisha Askofu Mkuu Rugambwa. Mtakatifu Paulo VI aliandika kwamba kati ya wali msitari wa mbele wa utamaduni ni waafrika kwa maana maana ya udhati wa kujieleza imani yao kikristo. Lengo la utamadunisho kama ilivyo jana kama leo hii ni kutaka kuonesha Kanisa la kweli la Afrika na daima kuonesha wakristo wa kina na wakatoliki ambao ni  ishara ya uwepo wa wokovu wa Mungu katika moyo wa hali halisi ya Afrika amesisitiza Askofu Mkuu Rugambwa.

Kanisa la Afrika linaalikwa kuwa na dhamiri nyoofu

Akiendelea na hotuba yake, Askofu Mkuu Rugambwa katika mtazamo wa ushauri wa Mtakatifu  Paulo VI ameshauri kwamba SECAM iweze kuishi upendo wa kweli wa kikundi au kwa maana nyingine kuwa na ushiriki wa mahusiano mema, ambao unapata msukumo wa maaskofu kwa ajili ya Makanisa mengine, na  kwa namna ya pekee amesema Askofu Mkuu kuwa, Kanisa la Afrika linaitwa kutengeneza dhamiri nyoofu  za kusikiliza  dharura za  madai ya haki na ili wanaume na wanawake waweze kukomaa na kuwa na uwezo wa kutambua utaratibu wa kijamii katika  mwenendo wao wa kuwajibika!

Kwa kuhitimisha Askofu Mkuu Rugambwa ametoa ushauri huku akikumbuka yale ambayo SECAM imeweza kutimiza kwa ajili ya kukua na maendeleo ya Kanisa barani Afrika na kufanya maneno ya Baba Mtakatifu Francisko yawe yake, wakati akizingumza juu ya ulazima wa mabadiliko na uongofu wa Kanisa. Ni imani ya Askofu Mkuu Rugambwa kwamba kwa msaada wa SECAM, Kanisa la Afrika, katika vipengele na miundo yake, linaitwa kuwa na mageuzi yake na  ya kudumu kwa ajili ya uaminifu kwa Kristo.

22 July 2019, 15:30