Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amemteua Askofu mkuu Giorgio Lingua kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Croatia. Papa Francisko amemteua Askofu mkuu Giorgio Lingua kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Croatia. 

Askofu mkuu Giorgio Lingua ateuliwa kuwa Balozi, Croatia!

Askofu mkuu Giorgio Lingua alizaliwa tarehe 23 Machi 1960 huko Fossano, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 10 Novemba 1984 akapewa Daraja takatifu ya Upadre. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu na hatimaye kuwekwa wakfu tarehe 9 Oktoba 2010 na Kardinali Tarcisio Berteno aliyekuwa Katibu mkuu wa Vatican wakati ule.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Giorgio Lingua kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Croatia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Lingua alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Cuba. Amewahi pia kuwa Balozi wa Vatican nchini Iraq na Yordan ambako ameshuhudia mateso na mahangaiko ya Wakristo kutokana na nyanyaso na dhuluma za kidini na kiimani, lakini wakati wote amejitahidi kuwa ni rejea ya matumaini kwa wale waliokata tamaa.  Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Lingua alizaliwa tarehe 23 Machi 1960 huko Fossano, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 10 Novemba 1984 akapewa Daraja takatifu ya Upadre.

Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu na hatimaye kuwekwa wakfu tarehe 9 Oktoba 2010 na Kardinali Tarcisio Berteno aliyekuwa Katibu mkuu wa Vatican wakati ule. Kimsingi Askofu mkuu Lingua alianza huduma ya kidiplomasia mjini Vatican kunako mwaka 1992. Tangu wakati huo ametekeleza utume wake sehemu mbali mbali za dunia kama vile: Pwani ya Pembe, Marekani, Serbia na Italia. Amewahi kufanya kazi katika Sekretarieti ya Vatican kwenye idara ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican na alijikita zaidi kwa masuala yaliyokuwa yanazihusu nchi za Amerika ya Kusini na Caribbeani.

Askofu mkuu Lingua
24 July 2019, 09:56