Tafuta

Vatican News
Papa Francisko ameridhia uteuzi wa Sinodi ya Maaskofu wa Kanisa la Kikoptiki la Kiorthodox la Upatriaki wa Misri wa Padre Danial Lofty Khella kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Ismaylia, Misri. Papa Francisko ameridhia uteuzi wa Sinodi ya Maaskofu wa Kanisa la Kikoptiki la Kiorthodox la Upatriaki wa Misri wa Padre Danial Lofty Khella kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Ismaylia, Misri.  (ANSA)

Padre Danial Lofty Khella ateuliwa kuwa Askofu Jimbo la Ismaylia

Askofu mteule Danial Lofty Khella alizaliwa mwaka 1969. Baada ya masomo yake, kunako mwaka 1996 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Baadaye alipelekwa nje kwa masomo ya juu kwenye Taasisi ya Ndoa na Familia ya Mtakatifu Yohane Paulo II iliyoko mjini Roma. Baada ya kurejea Misri alitekeleza utume wake kama Paroko-usu Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu huko Qoussieh.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia uteuzi wa Mheshimiwa Padre Danial Lofty Khella, wa Sinodi ya Maaskofu wa Kanisa la Kikoptiki la Kiorthodox la Upatriaki wa Alexandria kuwa Askofu wa Jimbo la Ismaylia, nchini Misri. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Danial Lofty Khella, alikuwa ni Paroko wa Kanisa kuu la Assiut na Mkurugenzi wa Utume wa Familia Upatriaki wa Alexandria, nchini Misri. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Danial Lofty Khella alizaliwa tarehe 4 Mei 1969. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 18 Julai 1996 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Baadaye alipelekwa na Jimbo lake kwa masomo ya juu kwenye Taasisi ya Ndoa na Familia ya Mtakatifu Yohane Paulo II iliyoko mjini Roma.

Baada ya kurejea Misri alitekeleza utume wake kama Paroko-usu Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu huko Qoussieh. Askofu mteule Danial Lofty Khella amekuwa ni mwalimu na mlezi wa Seminari kuu na Paroko huko Dronka. Baadaye aliteuliwa kuwa Mratibu mkuu wa Kituo cha familia kinachoendelea kujipambanua kwa kutetea Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo pamoja na kuwasaidia wanandoa watarajiwa kujiandaa kikamilifu kutangaza na kushuhudia tunu msingi za Injili ya familia zinazofumbatwa katika Injili ya uhai, utu na heshima ya binadamu. Amekuwa pia ni Mkurugenzi wa malezi ya kitawa!

Askofu Misri
03 July 2019, 14:20