Tafuta

Ujumbe wa uwakilishi wa Marais washirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya(Comece) wamekutana na Papa Francisko mjini Vatican tarehe 6 Juni 2019 Ujumbe wa uwakilishi wa Marais washirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya(Comece) wamekutana na Papa Francisko mjini Vatican tarehe 6 Juni 2019  

Papa na wakuu wa Comece:Ask.Mkuu Hollerich amesema Papa anaipenda kweli Ulaya!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na Tume ya maskofu wa Shirikisho la mabaraza ya Maaskofu Ulaya(Comece).Katika mzungumzo yao na waandishi wa habari viongozi hao mara baada ya mkutano wao,wamethibitisha juu ya wasiwasi alio nao Papa kwa ajili ya Ulaya,nafasi ya Kanisa,wahamiaji na ulinzi wa kazi ya uumbaji.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko anaipenda kweli Ulaya na kuwa na  wasiwasi kwa ajili ya Ulaya na kwa ajili ya amani akitazama historia ya bara la kizamani kwa yote yaliyotukia kuanzia miaka ya 30 na kwa sababu labda kuna ulinganifu. Haya na mengine ndiyo yaliyojitokeza katika mkutano wa Papa Francisko na wajumbe kutoka katika Tume ya Mabaraza ya Maaskofu wa Muungano wa Ulaya (COMECE) kwa mujubu wa maneno ya Askofu Mkuu Jean-Claude Hollerich wa Jimbo Kuu Lussemburg na Rais wa Comece akihojiwa na waandishi wa habari mara tu baada ya Mkutano huo.

Mkutano na viongozi hao na Papa umewatia moyo

Askofu Mkuu Hollerich anathibitisha kutiwa moyo wakati wa kukutana na  Papa  katika mkutano uliodumu kwa nusu saa na hata mawazo ya Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa ni muhimu hasa hasa aliyosema wakati yuko ziara ya kitume nchini Romania kwamba “siasa hazipaswi kamwe kupanda chuki na kuogopesha, bali kutoa matumaini”. Na Askofu Mkuu Hollerich anathibitisha kuunga mkono  amaneno hayo ya Papa kwa sababu, “ni kweli  watu wa kisiasa mara nyingi wako mbali na mahangaiko ya watu, katika maisha yao  ya kila siku ambayo yanatazama watoto bila kujua kama watafikia mwisho wa mwezi. Ni lazima wanasiasa wajikite  kwa kina zaidi kuhusu maisha ya watu na siyo kutumia mitindo ya kuogopesha.

Akitazama Lussemburg anasema, hata Kanisa lina  matatizo hayo ya wanasiasa, mara nyingi wako mbali na watu na  hata wasiwasi wao. Na ili kupelekea neno la Injili katika Ulaya ni lazima kuwa wanyenyekevu na kuwa karibu na watu.  Kuna vyama na labda vile vya upyaisho wa kiroho anabainisha Askofu Mkuu ambapo ni vizuri,  labda ni lazima kuweka mambo yote kwa pamoja kama ambavyo anavyosisitiza Baba Mtakatifu juu ya umasikini na jitihada kwa ajili ya masikini. Na kwa kufanya hivyo itaonesha kwa hakika  kuzaliwa kwa upya Kanisa katika nchi ya Umoja wa Ulaya!

Wahamiaji na nyumba yetu ya pamoja

Miongoni mwa masuala  mengini amabyo wamejikta nayo na Baba Mtakatifu  Francisko pia ni suala ya uhamiaji na ekolojia kwa mujibu wa Wosia wa Laudato Si wa kutunza nyumba yetu ya pamoja na umakini juu ya Sinodi ijayo ya Amazon , ambayo amezungumzia  Makamu Rais wa Comece, Askofu Franz-Josef Overbeck, wa jimbo la  Essen, Ujerumani. Katika kuelezea suala hili amesema kwamba Askofu Mkuu Hollerich, hivi karibuni ametoka ziara ya kitume kwa mujibu wa Baba Mtakatifu Francisko ya kwenda katikati ya wahamiaji katika kisiwa cha kigiriki huko Lesvos. Katika ziara hiyo amesisitiza kuona ni kwa jinsi gani gani katika bara la Ulaya, Makanisa yake yanapaswa kuwa na ukarimu wa kupokea, ikiwa ni  pamoja na majimbo, vyama na kwa njia ya mikondo ya kibinadamu.Wahamiaji walioko katika kisiwa cha Lesvos kwa hakika amesema wanaishi katika umasikini wa kutisha, japokuwa suala hili kwa baadhi ya maelfu ya watu wa Ulaya ingewezekana kabisa kuwapokea na kuwakaribisha.

Fursa na kipaumbele kwa vijana

Vile vile katika mantiki inayofanana na hiyo ya umasikini, pia suala la vijana limezungumziwa na Askofu Crociata wa Jimbo la Latina Italia  hasa katika mwanga wa uchaguzi wa hivi karibuni barani Ulaya na mabapo kwa ujumbala amethibtisha kwamba vijana waliopiga kura wameonesha mwamko chanya. Na Shirikisho la Mabaraza  ya Maaskofu Ulaya ( COMECE) kwa sasa wanajikita katika kuhamasisha kwa njia ya ujenzi wa jukwaa katika mashirikana na vyama vya vijana Ulaya. Hii siyo tu kwa wakristo bali kwa wote na  ili kuweza kuwapatia kipaumbele vijana wa Ulaya ambao wanahitaji. Na wakati huo huo, wakati endelevu unategemea na uwezo tulio nao yaani wa watu wazima wa kuwapatia nafsi na kipaumbele ili waendelee kuwa mstari wa mbele kwa ngazi ya Ulaya na katika maisha ya Kanisa. Huu ni  wito kwa wote ili kuweza kukuza nguvu ya sauti moja  katika Bunge la Ulaya na katika taasisi mpya za Ulaya kwa kukusanya dharura zote hasa kwa kujikita kutafuta kujibu ule  wema wa pamoja na kwa ajili ya wema wa watu wote!

07 June 2019, 10:10