Tafuta

Tarehe 18 waemwakilisha Jukwaa la vijana ambalo limezinduliwa tarehe 19-22 Juni 2019,huko Sassone ya Champino Roma kwa kuongozwa na mada "vijana katika matendo ndani ya Sinodi ya Kanisa” Tarehe 18 waemwakilisha Jukwaa la vijana ambalo limezinduliwa tarehe 19-22 Juni 2019,huko Sassone ya Champino Roma kwa kuongozwa na mada "vijana katika matendo ndani ya Sinodi ya Kanisa”  

Uzinduzi wa Jukwa la vijana kimataifa katika mwendelezo wa wazo la Sinodi iliyopita!

Tarehe 18 Juni 2019,wamewakilisha Baraza la kipapa la Walei Familia na Maisha,limewakilisha kwa waandishi wa habari juu ya siku tatu za Jukwaa la vijana,katika mwendelezo wa wazo la Sinodi ya Maaskofu Oktoba mwaka jana.Padre Mello kutoka Baraza hilo amesema Jukwaa hili ni fursa ya kutoa kipaumbele cha maisha ya vijana katika Kanisa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika uwakilishi wa Jukwaa la vijana la siku tatu kuanzia 19-22 Juni 2019,  huko Sassone ya Champino Roma, uliowakilishwa tarehe 18 Juni 2019 kwa waandishi wa habari Padre Alexandre Awi Mello, Katibu wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha amesema: Sinodi ya vijana bado haijaisha. Ipo katika hatua za michakato yake na kwamba  ni muhimu sasa kuwasaidia vijana wenyewe waweza kupeleka katika Mabaraza yao ya Maaskofu na katika vyama vyao wanamoshiriki, iwe hitimisho la Sinodi yenyewe ya mwaka jana,  iwe Wosia wa Christus Vivit, ambao ni tunda komavu la mchakato wa Sinodi ambao Baba Mtakatifu Francisko anautoa kwa Kanisa! 

Wawakilishi kutoka nchi 109 duniani

Jukwaa hili linaongozwa na tema vijana katika matendao ndani ya Sinodi ya Kanisa lililoandaliwa na Baraza hili na kwa maana hiyo ni mwendelezo wa mawazo ya maaskofu ya mwezi oktoba mwaka jana, uliokuwa unaongozwa na mada ya vijana, imani na mang’amuzi ya miito.  Kwa sasa ni Vijana 246 kati ya umri wa miaka 18- 29 ambao wanashiriki mkutano wa siku tatu, na wanao wakilisha nchi 109 na Jumuiya na vyama vya Kanisa 37. Vijana 18 ni wale waliokuwa wameshiriki Sinodi iliyopita mwezi Oktoba kama wasikilizaji, na wengine 15 ambao ni  wahusika viongozi katika masuala ya kichungaji ya  vijana kitaifa.

Fursa ya kuwa msitari wa mbele

Vijana anasema Padre Mello wanahisi kuwa kweli na furaha kwa sababu wanatambua kuwa Kanisa limejikita kwa dhati katika shughuli, siyo tu  katika kuwasikiliza vijana, lakini kwa namna ya kuwasindikiza na kuwasaidia ili waweze kuwa mstari wa mbele. Matendo ya  Sinodi yanategemea moja kwa moja na vijana. Wao wanapaswa kupeleka mbele hali halisi, katika makanisa yao maalum, katika vyuo vikuu , katika shule  na mahali popote pale ujumbe wa Sinodi, Ujumbe wa Papa wa Christus Vivit. Na wanahisi kuwa sehemu yao ambayo ni fursa ya kuwa na mstari wa mbele katika Kanisa.

Sinodi ya dhati isibaki katika karatasi

Lengo la kweli la Padre Mello amethibitisha kwamba  ni la kutaka kujua ni kitu gani kimefanyuka baada ya Sinodi  na baada ya Christus vivit, katika nchi za vijana  wanakotoka na katika vyama vyao. Baadaye ni kutafakari ujumbe wa Christus Vivit na kujikita kwa kina katika ujumbe huo wa Baba Mtakatifu. Je Papa anasema nini kwa vijana na jinsi gani wao wanapokea ujumbe huo? 

Siku ya tatu  ya Jukwaa na hitimisho litakuwa ni kuonesha hili: Je ni kitu gani kinaweza kutolewa leo hii na baadaye na sisi kama wawakilishi wa hali halisi ya makanisa yetu. Je ni kitu gani tunaweza kufanya mbele ya maaskofu, mbele ya mabaraza ya maaskofu na  ili Sinodi isibaki katika maandishi tu, bali  iweze kukita katika maisha ya kila siku ya Kanisa!

 

 

19 June 2019, 14:42