Tafuta

Papa amepokea watoto waliofika na treni kutoka Genova na wengine kwa Meli kutoka Sardegna Papa amepokea watoto waliofika na treni kutoka Genova na wengine kwa Meli kutoka Sardegna 

Treni ya watoto imefikia Papa ili kushinda hofu na upweke!

Kisiwa-daraja-bahari ni mada inayoongoza katika toleo la saba la “Treni ya Watoto” iliyoandaliwa na Cortile Gentile.Tarehe 8 Juni 2019 Baba Mtakatifu Francisko amewapokea makundi ya shule za watoto kutoka Genova na Sardegna nchini Italia walioathiriwa na matukio makubwa yatokanayo na uzembe na mengine ya asili pia vijana wengine kutoka mitaa ya hatari katika mji wa Napoli.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 8 Juni 2019 Baba Mtakatifu Francisko amewapokea makundi ya shule ya Genova na Sardegna nchini Italia walioathiriwa na matukio makubwa kama vile uzembe wa kibinadamu na nyingine majanga ya asili, na pia  vijana kutoka mitaa iliyo ya hatari katika mji wa Napoli. Vijana hawa wamefika na treni ya mwendo kasi kutoka Genova na wengine na njia ya Meli ya Moby Tommy kutoka kisiwa cha Sardegna. Ni watoto na vijana ambao wamekumbwa na matukio, kwanza kuanguka kwa daraja la Morandi huko Genova mwaka jana tarehe 14 Agosti na mafuriko katika Kisiwa cha Sardegna kunako mwaka 2013 na pia kuwahusisha shule ya Vela - Mascalzone Latino, iliyoundwa na Armatore Vincenzo Onorato kwa ajili ya kusaidia kwa dhati mafunzo ya watoto wanaoishi katika mitaa migumu sana ya mji wa Napoli. Kutokana na hiyo mwaka huu "Kisiwa, daraja la dhahabu na bahari ya mwanga"  kuwa  mada inayoongoza katika  toleo la saba la “Treni ya Watoto” iliyoandaliwa na Cortile Gentile, kitengo cha Baraza la Kipapa la Utamaduni kwa ushirikiano na Kampuni ya  Treni za Taifa na Kampuni ya Meli. Lengo la kujenga madaraja kwa ajili ya kushinda kila aina ya upweke ndiyo msingi na sababu ya watoto wengi ambao wameshirikishwa kwa kuwakumbusha mada msingi  wa mambo hayo matatu: daraja, kisiwa na bahari.  

Maswali ya watoto; Sijawahi kuchukia mwenzangu shuleni

Baada ya hotuba na salam na uwakilishi wa wahusika wa taasisi za  shule za Sardegna na Genova, watoto wamekuwa na fursa ya kuuliza maswali Baba Mtakatifu Francisko  ambaye amezungumza nao kwa hali ya utulivu kwa kumpatia akumbuke uzoefu wa utoto wake na kutoa baadhi ya tafakari. Baba Mtakatifu akijibu swali la watoto waliotaka kujua kama alikuwa anapenda shule, amesema kuwa, yaye hakuwa anapenda kusoma ... lakini alitakiwa ajifunze. Inatakiwa kijifunza kwa maana  mafunzo yanafungua milango na kusaidia sana kwenda mbele. Kadhalika amekumbuka mafunzo muhimu aliyopata kutoka kwa mwalimu wake aliyempa onyo la  kuwa makini dhidi ya kuchukia wenzake shuleni, kwa maana Baba Mtakatifu amesema, vita vikubwa vilivyopo sasa ambavyo wanauana katika vita, huanzia katika chuki ndogo ndogo. Kutokana na hilo, amependekeza  jambo rahisi kwamba iwapo mtu anahisi kusengenya wengine, ajaribu kuumwa ulimi wake kwa nguvu!.

Bwana anazungumza katika moyo; Papa na Safari

Baba Mtakatifu Francisko amejibu pia swali kuhusu wito wake juu ya  ukuhani kwamba, Bwana alimfanya ahisi kuwa hiyo ilikuwa ni njia yake. Yeye alikuwa amesomea kemia na alikuwa anafanya kazi katika mahabara, alihisi hili, na kwenda mbele na hisia hiyo. Ni Bwana anayezungumza katika moyo amesisitiza Baba Mtakatifu. Na kwa maana hiyo amewashauri watambue namna ya kuchambua sauti ya Mungu na ile ya shetani. Aidha ameweza kuwaeleza ni kwa jinsi gani hapendelei kusafiri. Amesema hayo kutokana na swali juu ya  ziara gani kati ya zile alizofanya imekuwa ya kipee na kujibu kuwa yeye ni kama watoto watukutu wasio penda supu.... Licha ya vichekesho hivyo amesema katika ziara zake, anapenda uzuri wa mazingira na kukutana na watu na hivi karibuni ametoka nchini Romania. Vile vile amewasimulia wageni waliotoka Sardegna kuwa, katika mji wake wa Buones Aries kuna sehemu inayoitwa jina la Madhabahu ya Mama Yetu wa Bonaria wa Cagliari ambayo walipewa mabahari wa  Sardegna waliofika na meli za Kisipanyola.

Kuishi kwa ajili ya fedha kuna haribu moyo

Hatimaye Baba Mtakatifu Francisko amejikita kutazama juu ya majanga ya asili ambayo yaliikumba Sardegna na juu ya uwajibikaji wa mikono ya binadamu na kusisitiza  kuwa, hasiye heshimu asili ameongozwa na fedha kwa maana shetani anaingia katika mifuko na kuongeza kusema kwamba fedha ndiyo za lazima na zinasaidia kuishi, lakini siyo kuishi kwa ajili ya fedha kwa maana zinaharibu mioyo na kukuharibu! Maandalizi ya mashule haya  kwa ajili ya kukutana na Baba Mtakatifu Francisko yameweza kuelezwa kwa kinagaubaga na Maria Grazia Cugisi, mwalimu wa shule ya Bitti, Orune, Lula, huko Sardegna kwa waandishi wa Vatican News. Katika maelezo yake  ni kwamba mada hii ina maana yake hasa ya kujenga madaraja kwa ajili ya kushinda ule upweke, ikiwa ni njia mwafaka na ya lazima ili kuweza kubomoa kuta mbaya kwa ajili ya kujenga madaraja ya upendo, ambayo yanadumu hata wakati wa mafuriko na pamoja na kuaka zile  kuta ambazo kila wakati zinaleta madhara  ya kila siku hasa kwa watoto.

Mchakato ya elimu kwa ajili ya maandalizi

Kabla ya kuanza safari hii wamefanya maandalizi ya mafunzo ya kisaikolojia ambayo yalifanyika katika mashule yote hasa kwa mwaka huu, na maandalizi ya mwanzo wakati wa kukutana. Taasisi mbali mbali zilizojita tangu  mwaka 2018 ni Shule ya msingi Giuseppe Mazzini, Shule ya Misingi Sampierdarena huko Genova, Taasisi ya Arzachena 1, taasisi ya Olbia, taasisi ya Torpè, taasisi ya  Bitti Onanì‐Lula, taasisi ya Terralba huko Sardegna.  Hata shule ya Msingi ya Vela Mascalzone- Latino, imejihusisha  katika maandalizi na vijana wa mitaa iliyo katika hatari huko Napoli kwa njia ya bahari na michezo wakiishi uzoefu wa mafunzo mbadala hata barabarani.

 

08 June 2019, 17:04