Tarehe 21 Juni 2019 Papa atakwenda Napoli katika mkutano kuhusu taalimungu baada ya Varitatis gaudiumu katika mantiki ya kimediterranea Tarehe 21 Juni 2019 Papa atakwenda Napoli katika mkutano kuhusu taalimungu baada ya Varitatis gaudiumu katika mantiki ya kimediterranea  

Papa katika mkutano Napoli:Kiini cha taalimungu ya Papa Francisko!

Ijumaa tarehe 21 Juni 2019 Baba Mtakatifu Francisko atakwenda Napoli katika mkutano kuhusu tema ya Taalimungu baada ya Veritatis Gadium katika mantiki ya Kimediterranea”ulioandaliwa na Taasisi ya Kipapa ya Taalimungu huko Italia Kusini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 21 Juni 2019 Baba Mtakatifu anatarajia kwenda Napoli ikiwa ni kwa mara ya pili baada ya kukubali mwaliko wa kuudhuria mkutano ulioandaliwa na Wajesuiti wa Taasisi ya Kipapa ya kitivo cha Taalimungu nchini Italia Kusini, kwa lengo la kuhimiza taalimungu inayo jikita katika hali halisi ya wakati wa sasa ili kuweza kujipyaisha kwa namna ya pekee katika mantiki inayotazama hali ya kimeditrannea na kujifafanua hasa katika mazungumzo, kubadilishana mawazo, suala la umbali na ambalo limegeuka kuwa janga la kifo na migogoro. Huu ni mkutano unaoongoza na tema ya "taalimungu baada ya Varitatis gaudium katika mantiki ya kimediterranea". Ni tema ambayo pia iliongoza mwaka 2018.

Taalimungu inayoanzia kwa kina katika imani ya kikristo

Naye Dk. Fabrizo Mandreoli Profesa cha Taalimungu msingi na Historia ya mawazo ya Taalimungu katika Kitivo cha Taalimungu huko Emilia Romagna Italia, akifafanua kwa ufupi kile ambacho ni mapendekezo ya Taalimungu ya Baba Mtakatififu Francisko anasisitiza kwamba hii ni taalimungu ambayo inaanzia na imani ya kikristo kwa kina na kuelekeza kwenye hali halisi ambayo inatuzunguka. Na ndilo lengo na msukumo wa Baba Mtakatifu Francisko katika kuikuza na  yeye kuiwakilisha kama msingi wa  mantiki ya taalimungu na katika maisha ya Kanisa kwa ujumla.

Taalimungu katika mantiki zake, inahitaji kupyaishwa

Hata hivyo kwa uhakika wa upyaisho wa mafunzo katika  vitivo vya taalimungu Profesa Mandreoli ambaye  pia atazungumza katika mkutano huo akiwakilisha  mada yake “ni taalimungu ipi katika mantiki ya Mediterranea" anathibitisha kuwa ni muhimu kwa maana  ni ujumbe unaojikita ndani ya Hati ya Kitume ya Veritatis gaudium na ambayo inafanya kuzungumza taalimungu katika mantiki tunamoishi! Na ndiyo  maana ya mkutano wa Napoli wa unaochota umuhimu wake na mada inayoongozwa na mkutano huo,utakaoitimishwa na tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 21 Juni. Mkutano huo hata hivyo unaanza siku ya Alhamsi 20 Juni  2019 kwa kujikita awali ya yote na mada zenye changamoto mbalimbali kama vile: mipaka mipya ya Bahari yetu, (Mare nostrum), uhamiaji, utamaduni, mazungumzo na baadaye watatoa mapendekezo yanayowezekana kutoa suluhisho  la mantiki ya kisanaa, ya makutano, ya mazungumzo ya kidini na mang’amuzi.

Swali kuhusu Taalimungu inayopendekezwa na Papa

Katika swali ni namna gani ya kuweza kufanya taalimungu mpya inayopendekezwa Baba Mtakatifu hasa inayojikita katika hali halisi ya Mediterranea. Na  Je kuna nini katika asili ya ujumbe wa Baba Mtakatifu alio ukabidhi katika Hati ya Veritatis gaudium na ambayo ni sambamba  na huduma yake yote hasa katika utume wa kimisionari, wa makutano, wa mazungumzo na kambi zake zote, ya kufungua mikono bila kujibagua. Profesa Fabrizio katika kufafanaua hili anaanzia na mapendekezo ya taalimungu moja kwa moja  ya Baba Mtakatifu Francisko. Yeye anasema haya  ni mapendekezo makubwa aliyotoa Baba Mtakatifu. Ndiyo ya kutafakari ndani ya utamaduni na ndani ya maisha ya Kanisa, japokuwa Profesa anaongeza kusema, ni lazima kwanza kuacha kujiuliza maswali binafsi yatokanayo na hali halisi ya mazingira.

Katika Taalimungu ya Baba Mtakatifu inasisitiza kwamba: ili taalimungu iweze kupyaishwa inahitaji kwanza kusikiliza, kuchunguza kwa makini kila aina ya uzoefu ambapo watu wa Mungu wanafanya na wanaishi, ikiwa na maana ya kuishi kati kati ya tamaduni za watu, maisha yao yaliyo magumu na utangazaji wa Injili. Na katika  kusikiliza uzoefu ambao kwa dhati Injili inagusa maisha ya binadamu, inawezekana kabisa kupata suluhisho na   matarajio hata kuwa na chachu ya kuweza kusaidia kupyaisha taalimungu kwa ujumla.

Changamoto ya kwanza ni ile ya kuwa na utajiti wa taalimungu ya kuunganisha

Aidha Profesa Fabrizo anazungumza kwamba changamoto ya kwanza ni ile ya kuweza kuweka utajiri wa Taalimungu ambayo imeungana daima katika imani, lakini kwa wingi wa hali halisi na unyeti wake. Pili taasisi zote zinahitaji kuwa na wanafunzi wataalimungu na maprofesa, watafiti ambao wanakaa katikati ya mantiki hizi. Ni wazi kwamba katika Mediterranea, dunia yenye wingi wa tamaduni, kuna haja ya watu waliokomaa kwa hakika  kitaalimungu! Vile vile kuna haja ya kile ambacho Baba Mtakatifu Francisko  anakiita "mazungumzo yote katika kambi". Hii ina maana ya kuwa makini kwa walio wa mwisho na kuwasikiliza wao wanasemaje. Na ndiyo hiyo  Profesa anafikiri kwamba ni muhimu suala la kutafuta walio wa mwisho.

18 June 2019, 14:15