Tafuta

Vatican News
Tarehe 19 Juni katika hitimisho la Kongamano la Ekaristi Takatifu Jimboni Oppido Mamertina-Palmila Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican aliongoza Misa Takatifu Tarehe 19 Juni katika hitimisho la Kongamano la Ekaristi Takatifu Jimboni Oppido Mamertina-Palmila Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican aliongoza Misa Takatifu  (Vatican Media)

Kard.Parolin:Ekaristi ni rasilimali ili dunia iweze kuwa bora!

Ili upate ushiriki mkamilifu wa maadhimisho matakatifu… nenda ujipatanishe na baadaye urudi (Mt. 5:23-24), ndiyo mada iliyoongoza Kongamano la Pili la Ekaristi katika Jimbo la Oppido Mamertina-Palmi,(Reggio Calabria)Italia, kuanzia tarehe 14-19 Juni kwa hitimisho la Misa Takatifu iliyoongozwa na Kardinali Pietro Parolin Katibu mkuu wa Vatican.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Kuanzia tarehe 14-19 Juni limefanyika Kongamano la Ekaristi katika Jimbo la Oppido Mamrrtina-Palmi huko Reggio Calabria, kwa kuongozwa na tema “ ndugu ili kwenda kuadhimisha mafumbo matakatifu… nenda kwanza ujipatanishe, baadaye urudi (rej.  Mt 5,23-24). Tarehe 19 Juni 2019 saa 12 jioni masaa ya Ulaya, katika Parokia ya Mtakatifu Gaetano Catanoso wa Gioa Tauro yamefanyika maadhimisho ya Ekaristi Takatifu iliyoongozwa na Kardinali Petro Parolin Katibu wa Vatican. Akianza mahubiri yake ameonesha furaha yake yake kusali nao katika maadhimisho hayo makuu na wakati huo huo ya dhati katika Misa Takatifu. Hiyo ina maana kwamba ni mikutano wa upendo wa Mungu kwa njia ya Neno lake na Mwili na Damu ya Yesu. Ni mkutano na Bwana (Katekesi ya Papa Francisko 15 Novemba 2017). Ni maneno hayo ambayo pia ametumia fursa ya kuwasalimia kwa niaba yake, akionesha ukaribu kuroho katika ardhi yao. Kardinali Parolin amesema kuwa Papa anatambua vema mahangaiko  maswali na matatizo ndani ya roho zao lakini pia hata imani yao kubwa waliyo nayo.

Amemshukuru Mchungaji wao wa Jimbo kwa maneno yake na mwaliko wa kuadhimisha Misa hiyo ikiwa ni kuhitimisho la Kongamano la II la Ekaristi Kijimbo, iliyoongozwa na mada msingi wa Ndugu yangu ili kuweza kuadhimisha kwa hadhi mafumbo matakatifu, Nende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi. Kwa hakika mada hii anasema Kardinali Parolin inawakilisha kipindi muhimu kwa ajili ya safari yao ya Kanisa. Juma walio maliza limekuwa na utajiri wa mikutano na vipindi vya tafakari kuhusu fumbo la Ekaristi na juu ya uhusiano wake na maisha. Ni fursa ya kukutana kwa pamoja na kuweka kiini cha yote na kushirikishana mkate wa mbingu na walio wengi wenye njaa ya matumaini na furaha. “Kuadhimisha Ekaristi hii kwa shauku, furaha na shukurani ni kwa sababu zawadi ambayo ni Sakramenti ya Ekaristi tuliyo pewa inaweza kweli kukaribishwa katika maisha yetu na inaweza kuleta matunda mengi ya neema”.

Hatuwezi kuishi bila Ekaristi

Kardinali Parolin anasema mara nyingi tumesikia kwamba hatuwezi kuishi bila Ekaristi. Bila Ekaristi hatuwezi kuishi, kwenda hata kuhudumia maskini, kama alivyokuwa akisema Mama Teresa wa Kalcutta na Padre Pio alipendelea kutumia picha hiii ni rahisi sana dunia kuishi bila jua kuliko kuishi bila Misa. Ili kuweza kukubaliana na ukweli huu ya kwamba si rahisi kuishi bila Ekaristi, inatosha kukumbuka  amri ya Bwana isemayo “ Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu” (Lk 22,19). Anayekita kwa dhati anajikuta amefungamana na Yeye kwa namna ya ajabu na kuhisi kuwa mdeni katika maisha yake na hawezi kuacha kutopokea neno na kuwa na shukrani na upole. Ni lazima kutambua kama mastahili la uaminifu wa Kanisa ambalo kwa miaka 2000 kwa njia ya amri ya Bwana inaendelea kuhifadhi bado uhai wake na nguvu yake.

Sababu ya kina ambayo sisi hatuwezi kuishi bila Ekaristi anaonesha kwamba ipo katika maneno ya Yesu Mwenyewe aliyo tamka juu ya kumega mkate na divai. “huu ni mwili wangu uliotlewa kwa ajili yenu… hiki ni kikombe cha aga jipya la damu yangu iliyo mwagika kwa ajili yenu” (Lc 22,19-20). Hatuwezi kubaki na sintofahamu mbele ya Maajabu ya Sakramenti ya Yesu aliyotoa maisha yake kama zawadi kwa ajili yetu. Tunapo karibia Ekaristi yake ni kufafanua ishara ya uwezekano wa kupokea zawadi ya Yesu kwa ajili yetu na mapendo yake na upendo wa sadaka ya mapatano. Kutokana na hiyo ndiyo zawadi ambayo Bwana anatoa maisha yake na inatoka katika upendo, ukarimu, msamaha, huduma ya pamoja na ambayoo inapanuka bila kuwa na kikomo hadi kuwafikia watu wote ili wote wahusike katika mzunguko wa karama!

Ekaristi inafanya Kanisa

Kardinali Parolin amesema kuwa awali ya yote Ekaristi inafanya Kanisa na kwa maana ya mujibu wa maneno anayorudia Mtakatifu Paulo kwamba Kanisa ni mwili wa Kristo (Ef 1,22-23; Kol 1,24). Ni muhimu kukumbuka kuwa Kanisa ni mwili, yaani hali halisi ya kijamii inayo onekana na wala siyo ya mawazo tu. Kanisa halifanywi uzoefu kwa njia ya undani bali ni hali halisi ya nje, inayo onekana na ambayo inajikita kwa dhati na uhalisia wake wa historia katika dunia. Neno ambalo Kanisa litangaza siyo lake  bali ni la Kristo, Sakramenti ambayo Kanisa inaadhimisha siyo za Kanisa bali za Kristo. Upendo ambao Kanisa unatafua kuuishi siyo upendo ambao unatokana na Kanisa bali na upendo wa  Kristo Bwana. Kwa maana hiyo anayekutana na Kania anaweza na kwa njia yake kukutana na Kristo, licha ya udhaifu, vikwazo ambavyo hawezi kuzuilika katika watu ambao wanaunda Kanisa hilo, amesema Kardinali Parolin.

Ekaristi ni rasilimali iliyotolewa ya maisha katika dunia

Ekaristi ni rasilimali iliyotolewa katika maisha katika dunia. Dunia yenyewe inakuwa bora. Je ni kitu gani kinawekwa katika miundo ya dunia, kwa njia ya Ekaristi iwapo siyo nguvu ya upendo, ya msamaha na mapatano? Vitu ambavyo kwa dhati vinashikiria dunia iweze kuwa na ngvu? Mara nyingi kuna anayefikiria kwamba dunia inashikiriwa na misukano mingi na ubinafsi tofauti. Kila mmoja anatafua faida yake binafsi, na jamuiya kwa sababu ya mafao na misukano ya wengine. Mtazamo huo lakini ni mbaya na usio kamilika uwapo hauzingatiwi na ni  wa kuharibu. Dunia imesisima kwa sababu wapo watu ambao wanapenda kweli na wanachukua si tu, uzito wa maisha yao lakini pia uzito wa maisha ya wengine na kukataa mambo ya anasa, ukuu, kwa kuacha nafasi kwa ajili ya wema wa wengine. Iwapo tunatoa hilo, dunia inageuka kuwa jehanamu; na iwapo dunia inakuwa jehanamu hata shauku ya kuwapatia wengine maisha haipo. Kwa maana hiyo Kardinali Parolin anasema kuna haja ya Ekaristi ambayo ni kisima cha upendo wa dunia na kwa hakika Mungu ametoa uwezo  na kutamani kwa kila moyo na uzoefu wenyewe wa kuishi, wa kupokelewa na mwingine wakati huo wa kusukumwa kupenda!

Hatuwezi kuishi bila Ekaristi

Hatuwezi kuishi bila ekaristi ikiwa na maana ya kwamba hatuwezi kuishi kama wakristo, hatuwezi kupata sehemu nyingine nguvu ya upendo ambao tunahitaji. Maisha yetu ni yale ambayo yameandikwa katika Injili iliyosomwa. Kwa njia ya rasimali zetu tunaweza kuhesabu kwa hakika mikate mitano na samaki wawili (Lk9,13); ambayo haikutupwa katu. Na japokuwa Bwana anataka zile rasilimali zetu ndogo za mikate mitano na samaki wawili ziweze kuongezeka maradufu kwa namna ya kwamba inaweza kutosheleza njaa zetu na za umati mkubwa pamoja nasi.

Ni jambo muhimu kukutana na umasikini wetu tunao wakilisha hasa wa mkate kidogo na divai kidogo. Lakini kile  kidogo ambacho tunakiweka mikononi mwa  Bwana kinatimiza miujiza. Huu ni mwili wangu kwa ajili yenu na kwa ajili ya agano jipya. Ekarisiti imewekwa katika mchakato wa mzunguko wa upendo na utambuzi wa yule anayependa kujipanua kwa upendo upeo.  Hatua ya asili ni kwamba, Kristo alinipenda na kujitoa mwenyewe kwa ajili yangu (Ga 2,20). Siyo rahisi kumrudishia Kristo kile ambacho alitoa kwa ajili yetu sisi, lakini tunaweza kumrudishia wale ambao Kristo anawapenda yaani ndugu zetu. Na ili kuwa na utambuzi huo, Kardinali Parolin anashauri kuwapenda wengine na kuwasaidia wale ambao mara nyingi hawewezi kurudisha upendo huo na kwa kufanya hivyo ni kuruhusu upendo upanuke na ndiyo sheria ya Ekaristi! Ni matarajio yake kwamba wanaweza kutumia nguvu za akili na moyo kwa ajili ya ujenzi wa jamii iliyo bora, hali na yenye mpangilio na wakati huohuo ikiwa ya kibinadamu, jamii yenye kuwa na hadhi ya utamaduni  wa kikristo katika ardhi yao!

20 June 2019, 14:59