Tafuta

Vatican News
Ziara ya Papa katika Kitivo cha Taalimungu huko Napoli Italia Kusini tarehe 21 Juni 2019 Ziara ya Papa katika Kitivo cha Taalimungu huko Napoli Italia Kusini tarehe 21 Juni 2019  (Vatican Media)

Hija ya Papa Francisko Napoli:Ni furaha kubwa na shukrani!

Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko huko Napoli ni fupi lakini ya kina.Amewasili majira ya saa 3.00 asubuhi na kupelekwa na Gari huko Possilipo mahali palipo na Taasisi ya Kitaalimungu huko Napoli,Italia Kusini kwa ajili ya kuanza mkutano.Baada ya hotuba yake atawasalimia wawakilishi wa walimu na wanafunzi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Karibu tena Francesco ndiyo kichwa cha habari katika magezeti yote ya Napoli katika siku ambayo Baba Mtakatifu Francisko merudi katika mji huo, lakini hata matarajio ya kwamba anaweza kusimama kati ya watu kwa ajili ya salam katika masaa 6 yaliyoko katika ratiba ya siku. Baba Mtakatifu Francisko amefikia mjini Napoli kwa mara ya pili baada ya miaka minne na amefika katika siku ambayo kiliturujia ni sikukuu ya Mtakatifu Alois Gonzaga, kijana mjesuiti ambaye alikuwa anawaka moto wa upendo kwa ajili ya walio wa mwisho.

Amechagua kwa mara nyingine tena hali halisi ndogo na ya pembezoni ile ya Taasisi ya Kitaalimungu katika ukanda wa Mediterranea, inayo wajumuisha wanafunzi 400 na maprofesa 80 ambapo chuo  kwa sasa kinapata nguvu zake na kuwa ishara ya Papa mwenyewe kutokana na maombi yake ya Katiba yake Kitume ya Veritatis gaudium yaani furaha ya ukweli iliyotolewa kwa ajili ya mafunzo ya kikanisa kwa mantiki zote, yaani hatua mpya ya utume wa Kanisa wa kimisionari unaojikita katika kushuhudia furaha ambayo inatokana na kukutana na Yesu na kutangaza Injili yake.

Hata hivyo kabla ya kufika kwa Baba Mtakatifu  Askofu  Mkuu wa Napoli pia ni Kansela wa Taasisi ya Kitaalimungu ya Kipapa huko Italia kusini Kardinali Crescenzio Sepe alikuwa ameelezea kuhusu roho ya maandalizi yaliyofanywa ili kumpokea Papa Francisko katika Taasisi hiyo ya kipapa na pia hata mujukumu ya mji wa Napoli waliyojikita nayo kwa kipindi cha miaka minne tangu ziara ya kwanza ya Baba Mtakatifu Francisko.

21 June 2019, 09:38