Tafuta

Vatican News
Radio Vatican inakuletea habari za Papa na Vatican kwa lugha ya kilatino kila siku ya Jumamosi saa 6.32 masaa ya Ulaya na marudio siku ya Jumapili saa 11. 30 masaa ya Ulaya kuanzia 8 Juni 2019 Radio Vatican inakuletea habari za Papa na Vatican kwa lugha ya kilatino kila siku ya Jumamosi saa 6.32 masaa ya Ulaya na marudio siku ya Jumapili saa 11. 30 masaa ya Ulaya kuanzia 8 Juni 2019  

Hebdomada Papae: Radio Vatican inakuletea Matangazo kwa lugha ya kilatino

Radio Vatican inakuletea habari za Papa kila siku ya Jumamosi saa 6.32 masaa ya Ulaya na marudio siku ya Jumapili saa 11. 30jioni kuanzia 8 Juni 2019. Kipindi rasmi kiitwacho “Hebdomada Papae, notitiae vaticanae latine redditae” yaani “Habari za Radio Vatican katika Lugha ya kilatino”. kipindi kipya kabisa cha habari za wiki kwa lugha ya kilatino kwa dakika 5,ambazo zitawekwa katika podcast ya Vatican News.Hii imeundwa kwa ushirikiano na Ofisi ya Katibu Vatican kwenye kitengo tafsiri ya barua za Kilatino.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 8 Juni 2019, masafa mapya ya Radio Vatican itatangazwa  kipindo kiitwacho Hebdomada Papae, notitiae vaticanae latine redditae’, yaani  habari za wiki za shughuli za Baba Mtakatifu na Vatican kwa lugha ya kilatino. Hiki ni kipindi kipya kabisa cha habari za wiki kwa lugha ya kilatino kwa dakika 5, ambazo zitawekwa pia katika podcast ya Vatican News. Hii imeundwa kwa ushirikiano wa uhairiri wa Radio Vatican na Ofisi ya Katibu wa Vatican kwenye kitengo cha  tafsiri za barua za Kilatino na Tweet za Acount ya @Pontifex_ln.

Matangazo ya  kila Jumamosi kwa dak 5 saa 6.32 na marudio Jumapili jioni

Habari mpya za  matangazo ya radio kwa lugha ya kilatino ambayo yatadumu kwa dakika tano, yatahaririwa na Alessandro De Carolis,  ambayo yatatangazwa kila Jumamosi kwenye masafa ya Radio Vatican (kwa upande wa wa Italia ni saa 6.32 na kurudiwa tena kila Jumapili  saa 11.30 jioni masaa ya Ulaya).

Tornielli: ni habari halisi za radio halisi; changamoto kwa siku zijazo

Naye amkurugenzi wa uhariri wa Radio Vatican, Bwana Andrea Tornielli akifafanua juu ya kuanzishwa kwa matangazo haya  amesema:  “kwa kuanzishwa kipindi hiki cha kila wiki, tunataka pia kufufua hata habari  katika lugha rasmi ya Kanisa Katoliki ambayo tayari ipo kila siku katika mzunguko wa Radio Vatican hasa wakati maadhimisho ya misa takatifu ya kila asubuhi kwa lugha ya kilatino”. Vilevile amethibitisha: "hii ni huduma ya habari na halisi. Hatukufikiria kama ni kufanya kumbukumbu ya wakati uliopita, bali ni kama changamoto kwa siku zijazo”.

06 June 2019, 12:12