Tafuta

Vatican News
Baraza la Makardinali Washauri chini ya Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 25-27 Juni wanafanya mkutano wao wa XXX. Baraza la Makardinali Washauri chini ya Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 25-27 Juni wanafanya mkutano wao wa XXX. 

Baraza la Makardinali Washauri: Mkutano XXX: 25-27 Juni 2019

Baba Mtakatifu Francisko pamoja na Makardinali washauri, kuanzia tarehe 25 Juni hadi tarehe 27 Juni 2019 wanafanya mkutano wa XXX wa Baraza la Makardinali Washauri. Alhamisi, tarehe 27 Juni 2019, Dr. Alessandro Gisoti, Msemaji mkuu wa muda wa Vatican na Askofu Marcello Semeraro, Katibu wa Baraza la Makardinali Washauri, watazungumza na waandishi wa habari na kutoa TAMKO!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baraza la Makardinali Washauri tayari limekwisha wasilisha Muswada wa Katiba mpya ya Kitume inayojulikana kama “Predicate evangelium” yaani “Hubirini Injili. Muswada huu unaendelea kupitiwa na Mabaraza ya Kipapa, Mabaraza ya Maaskofu Katoliki na Sinodi za Makanisa ya Mashariki, kama sehemu ya utekelezaji wa dhana ya Sinodi katika maisha na utume wa Kanisa. Baba Mtakatifu Francisko pamoja na Makardinali washauri, kuanzia tarehe 25 Juni hadi tarehe 27 Juni 2019 wanafanya mkutano wa XXX wa Baraza la Makardinali Washauri.

Alhamisi, tarehe 27 Juni 2019, Dr. Alessandro Gisoti, Msemaji mkuu wa muda wa Vatican, akiwa ameandamana na Askofu Marcello Semeraro, Katibu wa Baraza la Makardinali Washauri, watazungumza na waandishi wa habari, ili kufafanua yale yatakayokuwa yamejiri katika mkutano huu. Mazungumzo hayo yatatangazwa na kurushwa moja kwa moja na vyombo vya mawasiliano vya Vatican kwa kushirikiana na wamiliki wa vyombo vingine vya mawasiliano ya jamii ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi! Baraza la Makardinali Washauri ni chombo kilichoundwa na Baba Mtakatifu Francisko, kama sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyokuwa yametolewa na Baraza la Makardinali kunako mwaka 2013.

Baraza la Makardinali

 

25 June 2019, 14:52