Ilikuwa mwaka 2015 Papa alipokutana kwa mara ya pili na Rais wa Shirikisho la Urusi Bwana Vladimir Putin. Kwa mara ya tatu atakutana naye tarehe 4 Julai 2019 Ilikuwa mwaka 2015 Papa alipokutana kwa mara ya pili na Rais wa Shirikisho la Urusi Bwana Vladimir Putin. Kwa mara ya tatu atakutana naye tarehe 4 Julai 2019 

Baba Mtakatifu atakutana na Rais wa Urusi tarehe 4 Julai 2019

Tarehe 4 Julai 2019 Baba Mtakatifu anatarajia kukuta na Rais wa Putin wa Urusi. Na huu ni mkutano wake kwa mara ya tatu kati ya Papa na Putin. Wa kwanza ulikuwa tarehe 2 Novemba 2013, wa pili ulikuwa tarehe 10 Juni 2015 na sasa wa tatu Julai 2019.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Akijibu maswali ya baadhi ya waandishi wa habari Msemaji wa mpito wa vyombo vya habari Vatican Dk Alessandro Gisotti, amethibitisha kuwa, Baba Mtakatifu Francisko atampokea mjini Vatican Rais wa Shirikiko la nchi ya Urusi, Bwana Vladimir Putin, tarehe 4 Julai 2019. Na hii itakuwa ni kwa mara ya tatu kuwa na mkutano kati ya Papa na Putin. Wa kwanza ulikuwa tarehe 2 Novemba 2013: wa pili ulikuwa tarehe 10 Juni 2015 na sasa wa tatu Julai 2019.

Mkutano wa kwanza wa Papa na Rais wa Urusi

Mwaka 2013 Baba Mtakatifu alipata kuzungumza na Rais wa Urusi kwa faragha dakika 35 na kufuatia utumaduni wa kubadilishana zawadi. Baba Mtakatifu alimzawadia picha  inayoonesha bustani ya Vatican na Bwana Vladim alimzawadia picha ya Mama Maria inayotolewa ibadi sana na watu wa urusi.

Mkutano wa pili ulikuwa ni 2015

Baba Mtakatifu alikutana na Rais wa Urusi kwa mara ya pili kunako mwaka 2015 katika Makataba ya Jumba la kutume mjini Vatican na mazungumzo yao yalidumu kwa dk 50. Na kama kawaida ya utamaduni ilifuatiwa kubadilishana zawadi. Zawadi ya Baba Mtakatifu ilikuwa ni medali iliyowakilisha malaika wa amani ikimwalika katika ujenzi wa dunia ya mshikamano na amani inayojikita juu ya haki na kitabu cha Wosia wake wa Kitume Evangelii gaudium. Katika mazungumzo yao waligusia zaidi juu ya migogoro ya nchi ya Ukrane na hali halisi ya nchi za Mashariki.

Mkutano na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedetto XVI

Hata hivyo pia kunako 2007 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI alikutana na  Rais wa Urusi Valdimir Putin na ambapo katika mazungumzo yao walielezea juu ya uhusiano uliopo kati ya Vatican na Shirikisho la Urusi , vile vile kuonesha utashi wa maendeleo na masuala ya  utamaduni. Hawakukosa kutazama hata hali halisi inayotazama  Kanisa Katoliki na Kanisa la Kirothodox pamoja na  masuala ya kimataifa ya sasa ikiwa ni pamoja na hali halisi ya nchi za Mashariki, ukosefu wa vumilivu ambao hadi leo ni hatari ya  kutokuweza kuishi vema kati ya mataifa. Na kwa maana hiyo walisisitizia juu ya kukuza amani na kutafuta suluhisho la mchakato wa amani katika migogoro.

06 June 2019, 14:39