Tafuta

Askofu mkuu Peter Rajic, Balozi wa Vatican nchini Angola  na São Tomé Askofu mkuu Peter Rajic, Balozi wa Vatican nchini Angola na São Tomé 

Askofu mkuu Petar Rajic, Balozi mpya wa Vatican nchini Lithuania

Askofu mkuu Rajic alizaliwa kunako tarehe 12 Juni 1957. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa hapo tarehe 29 Juni 1987. Tarehe 2 Desemba 2009 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu hapo tarehe 23 Januari 2010. Na Mwaka 2019 amehamishiwa Angola na Sao Tome.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Petar Antun Rajic kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Lithuania. Kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Angola, Sao Tome na Principe. Askofu mkuu Petar Rajic amewahi pia kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Kuwait, Bahrein, Yemen, Qatar na Falme za Kiarabu pamoja na kuwa ni mwalikishi wa Kisiwa cha Kiarabu.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Rajic alizaliwa kunako tarehe 12 Juni 1957. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa hapo tarehe 29 Juni 1987. Tarehe 2 Desemba 2009 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu hapo tarehe 23 Januari 2010. Na Mwaka 2019 ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Lithuania! Utume mwema!

Papa: Lithuania
17 June 2019, 10:17