Katika mahojiano na Vatican News Askofu Mkuu Gallagher anaelezea kwa ufupi kuhusiana na shughuli za Kanisa kuhusu suala la uhamiaji na ukimbizi kimataifa Katika mahojiano na Vatican News Askofu Mkuu Gallagher anaelezea kwa ufupi kuhusiana na shughuli za Kanisa kuhusu suala la uhamiaji na ukimbizi kimataifa 

Askofu Mkuu Gallagher anasema ni lazima kutoa majibu ya kibinadamu!

Katika kuekelea siku ya Wakimbizi duniani,umefanyika mkutano katika makao ya Radio Vatican ukiongozwa na mada ya wahamiaji na wakimbizi.Mchango na changamoto za wakati.Ni mkutano uliojadili kwa mapana kuhusu mazungumzo na namna ya kutafuta suluhisho la maswali mengi kuhusu tukio la uhamiaji.Katika mahojiano na Askofu Mkuu Gallagher anaelezea kwa ufupi shughuli za Kanisa kuhusu suala hili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Familia ya Nazaret ni ya kutoka, Yesu Maria na Yosefu ni wahamiaji wa Misri ambao ni mfano wa kuigwa kwa msaada wa wahamiaji na wakimbizi wa kila rika na kila nchi na kwa wakimbizi wa kila hali ambao wanateswa na kunyanyaswa au wanahitaji, wanalazimika kuacha nchi zao na kwenda nchi za kigeni.  Katika maneno ya Papa Pio XII yaliyomo katika Hati ya Exsul Familia iliyotangzwa kunako 1952 na kuzungumziwa na mara nyingi na Baba Mtakatifu Francisko, ndiyo imefunguliwa katika  mkutano katika Makao makuu ya Radio Vatican, kwa kuongozwa na mada ya “wahamiaji na wakatimbizi”. Mchango na changamoto za wakati”,ulio andaliwa na Balozi wa Argentina mjini  Vatican( makao ya MERCOSUR).

Tarehe 20 Juni, Siku ya Kimataifa ya wakimbizi

Tarehe 19 Juni 2019 ulikuwa ni mkutano uliojaa mambo mengi na taarifa mbali mbali rasimi, maoni na mategemeo mema ikiwa na  maana ya ukarimu wa makalibisho ambapo mabalozi waliweza kubadilishana  mawazo na viongozi wengine wa Kanisa, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Afya na mashirika mengine kama vile ya Caritas internationalis na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ikiwa pia ni fursa ya kumbukumbu ya Siku ya ya kimataifa ya uhamiaji ambayo inafanyika kila mwaka tarehe 20 Juni. Kuna haja kwa hakika ya kushirikiana kidunia na uwajibikaji wa kushirikisha, ili kukabiliana zaidi na tendo la wimbi la watu kuhama katika historia za hivi karibuni. Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Wakimbizi duniani UNHCR iliyotangazwa katika fursa ya Siku ya Wakimbizi inasema ni Milioni 260 za wahamiaji kimataifa, Milioni 760 za watu wa ndani na zaidi ya milioni 70 za wakimbizi wanaomba hifadhi wakati wakilazimika kuacha nyumba zao chini ya hatari za mabomu, hofu na kuteswa kisiasa na kidini.

Mchango unaotolewa na Vatican

Katika kinasaba cha Kanisa, katika hisotria yake ina tabia ya ukaribu, ya mshikiamano na kutunza kila mtu anayekimbia. Inajikita katika kishirikiana na Jumuiya za Kimataifa ili kukuza na kuchukua vipimo vya dhati vyenye malengo mafupi , kati na muda mrefu  kwa ajili ya kulinda hadhi, haki na uhuru wa watu ambao wanalazika kuhama. Ndiyo uthibitisho Katibu Mkuu Mkuu wa Mahusiano Vatican na ushirikiano na nchi, Askofu Mkuu Richard Gallagher, wakati wa kutoa hotuba yake katika mkutano huo. Na akihojiana na mwandishi wa habari wa Vatican News kuhusu tema ya mkutano huo yeye anaamini Ujumbe wa Vatican katika kipindi hiki ambacho kila mmoja anatambua kuwa siyo kirahisi kwa ajili ya uendesheaji wa hali halisi ya uhamiaji katika nchi,  hivyo kwa pamoja ni lazima kukabiliana na hali halisi ngumu. Ni hali ambayo haitoweki kwa usiku mmoja tu anabainisha, bali ni mgogoro ambao upo kwa kipindi cha sasa kama Baba Mtakatifu Francisko alivyo sema kuwa, lazima kutoa jibu kwa namna ya kibinadamu, kwa namna ya kikristo na lazima kutafuta kuwatendea vema watu na si kuwatendea vibaya.

Ushirikiano wa Vatican na suala la wakimbizi

Kwa upande wa ushirikiano wa Vatican na nchi nyingine mbele ya uhamiaji huo, Askofu Mkuu Gallagher amesema wanashiriki kwa uhai hata kwa mbali na katika mikutano ya kimataifa; wanatafua kuchangia katika mafunzo ya Mikataba ya kimataifa, hata shughuli nyingine  za lazima na zaidi kuhamasisha mashirika katoliki duniani kote ili wawe wakarimu wa kupokea. Hata hivyo amekumbusha juu ya kazi ya Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu ambao wanajikita kwa namna ya dhati katika matukio hayo ya uhamiaji na wakimbizi, baraza ambalo Baba Mtakatifu alipendelea liweze kuongoza sekta hiyo.Katika hotuba ya Askofu Mkuu Gallagher ametaja maneno manne ya Papa Franciso ya kupokea , kuhamasisha, kulinda na kufungamanisha, licha ya hayo bado kuna majibu hasi ya sera za kisiasa katika kuamsha kuta.

Matendo ya mshikamano wa kweli ni muhimu ili kukabiliana tukio la uhamiaji

Askofu Mkuu Gallagher amethibtisha kuwa  Vatican bado inaendelea kuzungumza zaidi na marafiki wa Ulaya, kuwatia moyo kwa dhati ili bkuweza kutoa majibu ambayo yanaweza kuleta suluhisho la mgogoro huo kwa matend na hasa yaele  yanayo heshimu ukuu wa nchi, lakini wakati huo huo kwa kuzingatia  akilini kwamba, hali halisi ndiyo hiyo na ambayo lazima kukabiliana nayo, lazima kusaidia, ni hali  hali ambayo haitabadiliki kwa siku moja; Ni lazima kuendelea zaidi labda itakuwa miaka na miaka kuwa na matendo ya mshikamano kwa upendo kidugu katika mtazamo wa watu hao. Hata hivyo katika kilel cha siku ya Kimataifa ya wakimbizi  tarehe 20 Juni, naye  katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amehimiza mshikamano akiomba jamii zote kushirikiana katika usaidizi kwa wasiojiweza  ambao ni wanawake na watoto katika migogoro duniani.

20 June 2019, 15:06