Tafuta

Vatican News
Tarehe 24 JuniAskofu Mkuu Fisichella amewakilishwa video ya Katekisimu ya Kanisa  Katoliki Tarehe 24 JuniAskofu Mkuu Fisichella amewakilishwa video ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki  

Video ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki ni kichocheo cha nyakati zetu!

Tarehe 24 Juni 2019 imewakilishwa Video ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki,ambapo Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji mpya Askofu Mkuu Rino Fischella anasisitizia juu ya video hiyo kuwa ni kichocheo cha nyakati zetu.Ni jibu zaidi ambalo limesasishwa kuhusu swali la vyombo vya habari kwamba vinaweza kufanya nini ili viweze kuwa katika huduma ya uinjilishaji mpya.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Askofu Mkuu  Rino Fischella, Rais wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa uinjilishaji mpya, wakati wa kuwakilisha video ya Katekisimu ya Kanisa katoliki katika Jumba la picha mjini Vatican, amesema kuwa video hiyo ni kichocheo cha nyakati zetu.  Amesema hayo mara baada ya utangulizi kwa jumla kutoka  Chuo Kikuu ca Kipapa cha  Gregoriana Roma. Hii ni katika siku chache  kufikia miaka 9 tangu Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI alipotangaza juu ya kuundwa kwa baraza la kipapa la uinjilisha mpya akiwa katika Kanisa Kuu la Mtakatofu Paulo nje ya Ukuta Roma. Na kutokana na hilo Askofu Mkuu Fischella pia amekumbusha jinsi gani shughuli hiyo ilivyoweza kukabidhiwa  na kusimamia uhamasishaji wa Katekisimu ya Kanisa Katoliki na ambayo inafuatilia kiutaalam zaidi juu ya katekesi katoliki itumikayo duniani kote. Katika Video ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki yapo matarajio mawili, ambayo lazima kwenda sambamba. Awali ya yote shughuli  kubwa inatazama zana mpya kama ile ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki na ambayo leo hii imetafsiriwa kwa lugha 70 ikiwemo hata lugha ya kikurdi na pia video ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki.

Video ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki inatoa jibu kwa vyombo vya habari

Video ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki ambayo kwa mujibu wa Askofu Mkuu Fischella anasema ni kutoa zaidi ambalo limesasishwa kuhusu swali la vyombo vya habari vinaweza kufanya nini ili viweze kuwa katika huduma ya uinjilishaji mpya. Hii ina maana ya nini kile ambacho Kanisa liliamini, linaamini,linaadhimisha na kushuhudia na kama kweli kichochezi kwa ajili ya mtu wa sasa. Na kwa kufanya hivyo Askofu Mkuu Fischella ametaja hata maneno ya hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kumbukumbu ya miaka 25 tangu kutangazwa kwa Katekisimu ya Kanisa Katoliki na ambapo yeye aliomba kubadili kifungu cha maandiko yanayohusu adhabu ya kifo.

Video ya Katekisimu ni fursa ya kusoma ndani ya Kanisa historia na utamaduni

Video ya Katekisimu katika mantiki hiyo Askofu Mkuu Fisichella  anahitimisha kwamba, ni fursa ya kuweza kulisoma Kanisa kwa undani dhana ya kihistoria na kiutamaduni lakini pia ni ndani ya Kanisa ambamo tunaishi, licha ya  kuwa hazina iliyowekwa katika mazoezi ya mamilioni ya makatekisti  duniani kote; kwa ajili ya katekesi ya watu wazima wenye hamu ya kukutana zana mpya ya mawasiliano.

25 June 2019, 13:17