Ziara ya Kardinali Filoni nchini Sri Lanka ambapo amesali kwa ajili ya waathirika wa mashambulizi ya kigaidi na kuwafariji wafiwa wote. Ziara ya Kardinali Filoni nchini Sri Lanka ambapo amesali kwa ajili ya waathirika wa mashambulizi ya kigaidi na kuwafariji wafiwa wote. 

Sri Lanka:Kard Filoni amesali sala ya Papa na ndugu waathirika wa shambulizi la kigaidi!

Tangu tarehe 22-24 Mei Kardinali Fernando Filoni Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu amekuwa nchini Sri Lanka.Amefika nchini humo kwa ajili ya kupeleka mshikamano wa Baba Mtakatifu Francisko.Akiwa nchini humo ametembelea sehemu zote zilizo shambuliwa pia kusali kwa ajili ya waathirika wa mashambulizi ya kigaidi baada ya mwezi mmoja

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Akiwa katika ziara yake nchini Sri Lanka Kardinali Fernando Filoni Rais wa Baraza la Kipapa la Injilishaji wa Watu, ametembelea madhabahu ya Mtakatifu Colombo, Kanisa la Mtakatifu Sebastian huko Nagombo, kukutana na familia za ndugu waathirika wa mashambulizi ya kigaidi na kufanya mazungumzo na  Rais wa nchi pia Waziri Mkuu wa Sri Lanka. Ndiyo zilikuwa hatua zake muhimu katika kijiji hiki kikubwa cha kisiwa hicho, baada ya mwezi mmoja tangu kushambuliwa na magaidi tarehe 21 Aprili 2019 na kusababisha karibia vifo vya watu 258. Kwa mujibu wa mamlaka ya nchini mashambulizi hayo ni kutokana na vikundi vidogo vidogo vyenye mzizi wa Serikali yakiislama katika kisiwa hicho.

Imani ndiyo ngao zaidi dhidi ya hofu zote

Katika ziara yake Kardinali Filoni amesindikizwa na Askofu Mkuu wa Colombo Kardinali Malcolm Ranjith Patabendige Don na ambaye akizungumza na Vatican News amesema kuwa, mashambulizi hayo yaliyo jitokeza katika Sikukuu ya pasaka yameleta wasiwasi mkubwa katika nchi na kusababisha kuyumba kwa namna ya kuishi kwa watu kati ya dini tofauti. Lakini anakumbusha kwamba Kardinali Filoni ameweza kukutana na familia za waathirika na kuwapa mshikamano wa Baba Mtakatifu Francisko na kuwahakikishia maombi yake.

Jiwe la msingi katika kituo cha utoaji wa chakula kwa masikini

Aidha akiwa katika ziara hiyo Kardinali Filoni ameweka jiwe la msingi katika jengo la kituo cha masikini cha Kanisa la Mtakatifu Antonio ambalo liliharibiwa na mabomu ya mashambulizi ya kigaidi. Hiki ni kituo cha kuwapatia masikini chakula na kinakaribishwa watu wote bila kujali dini, bali watu wote  wenye  kuhitaji ambapo kwa kukutana na masikini hao amewafariji na kurudia maneno ya Baba Mtakatifu aliyosema wakati wa sala ya Malaika wa Bwana siku ya Pasaka katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Katika kituo hiki Kanisa mahalia wamaanzisha mshikamano wa nguvu wa kuwasaidia ndugu wa waathirika kwa njia ya zana, kisaikolojia na hata kiroho.

Ni waamini wachache kwa sasa wanaokwenda kanisani japokuwa wakiwa na hofu

Hadi sasa Kanisa la Sri Lanka linaudhuriwa na watu wachache Kanisani.hata hivyo wakatoliki wanajaribu kutoa ushuhuda mkubwa wa imani yao. Sehemu kubwa ya waamini katika kisiwa hicho ni wabudha, lakini pia wahindu na waislam kwa mujibu wa maelezo mahalia wa  Jimbo Kuu la Colombo. Hata hivyo wameshangazwa na waamini wakristo ambao hawakujibu mashambulizi hayo kwa hasira na wala kisasi badala yake kupenda kuwa na majadiliano. Vile vile, ushuhuda wa ushiriki wa ibada takatifu unaendelea, japokuwa na hofu  kutokana na mashambulizi mapya ambayo yaweza kutokea. Kwa hakika katika baadhi ya mashule bado hayajafunguliwa hasa kwa watoto wadogo. Katika jamii ya Sri Lanka  wamekomaa kwa kiasi chake jumuiya nyingi za kikristo na kwa namna ya pekee wakatoliki amethibitisha Askofu Mkuu wa Colombo .

27 May 2019, 11:04