Askofu Semeraro wa jimbo katoliki la Albano na Katibu wa Baraza la Makardinali,ameandika kitabu:Kusikiliza na kutibu moyo.Mang’amuzi ya maisha ya kichungaji katika Kanisa Askofu Semeraro wa jimbo katoliki la Albano na Katibu wa Baraza la Makardinali,ameandika kitabu:Kusikiliza na kutibu moyo.Mang’amuzi ya maisha ya kichungaji katika Kanisa 

Papa Francisko:Mang’amuzi ya kiinjili kwa hakika ni muhimu katika mwanga wa Roho!

Kimetolewa kitabu chenye mkusanyiko wa barua tatu za kichungaji za Askofu Semeraro wa Jimbo Katoliki Alibano na Katibu wa Baraza la Makardinali.Kichwa chake:Kusikiliza na kutibu moyo.Mang’amuzi ya maisha ya kichungaji katika Kanisa.Utangulizi ni wa Papa akikazia juu ya nyaraka zake:Evangelii gaudium,Amoris laetitia,Gaudete et exsultate na Ratio Fundamentalis kwa ajili ya mafunzo ya kikuhani,waamini wenye uwezo wa kutafsiri hali halisi ya maisha ya kibinadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika fursa ya Siku ya Duka la vitabu Vatican kimetolewa kitabu kilichoandikwa na  Askofu Marcello Semeraro Katibu wa Baraza la Makardinali chenye kichwa: “Kusikiliza na kutibu moyo. Mang’amuzi ya maisha ya kichungaji katika Kanisa”. Utangulizi wa kitabu hiki umeandikwa na Baba Matakatifu Francisko. Kitabu hiki kimetolewa mapema wiki hiki na ambacho ni mkusanyiko wa barua tatu za Askofu Semeraro kwa  Jimbo katoliki la Albano, Italia ambapo ameweza kukabiliana na mada ya kufanya  mang’amuzi ya kiroho katika maisha ya ukuhani, iwe kwa ngazi binafsi, hata katika mazoezi kamili ya utoaji wa  huduma ya kikuhani. Mang’amuzi kwa mujibu wa Askofu Semeraro, yanaweza kufikiriwa kama mstari mwekundu unaounganisha uzoefu tofauti wa maisha ya kuhani.

Kitabu kinaonesha kwa jinsi gani mahitaji ya Kanisa yanaongezeka pia kuhitaji mang'amuzi

Baba Mtakatifu Fracisko katika utangulizi wa kitabu hiki anaonesha kuwa, kukua kwa Kanisa mara nyingi una mahitaji ya kuwa na uwezo wa kufanya mang’amuzi  na ndiyo kiukweli yeye binafsi amekuwa akikazia mara kwa mara kwa kuonesha katika mitindo mbalimbali. Kwa mfano katika fursa nyingi za mikutano ameweza kukumbusha na  zaidi katika mada  ya Wosia wa “Evangelii gaudium”, ambapo unahusisha sana na  uhusiano wa kufanya uchaguzi wa kichungaji. Mang’amuzi ya kiinjili kwa hakika ni muhimu, ni mahali ambapo katika mwanga wa Roho unajikita unakusaidia kutafuta na kujua kila aina ya wito ambao Mungu anautaka katika Kanisa na kwa kila mtu katika hali halisi ya kihistoria.

Kusoma Amoris laetitia,Gaudete et exultate 

Baba Mtakatifu aidha ameandika kwamba: katika kusoma kurasa za Amoris laetitia, kwa hakika zitakuwa zimeeleweka kwamba. mang’amuzi yanahitajika  kwa namna ya pekee ya kichungaji. Lakini hata hivyo, haihusishi huduma ya wachungaji tu,  bali hata huduma katika mahitaji ya maisha ya kikristo  na ambayo ni ukweli wa imani ya kizamani. Baba Mtakatifu akinukuu neno kutoka kwa watu wa zamani wa Misri wa karene ya ukristo, amemtaja Antonio Mkuu anaye sema hivi: “Kuna watu ambao wamevaa miili yao kwa kujikata katika kusali, bila kuwa hata hivyo kuwa na  mang’amuzi na   wakaishia kwenda mbali na Mungu”. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko anaandika: Na ndivyo  hivyo njia ya utakatifu wenyewe ambayo inahitaji kufanya mang’amuzi;  “hata hivyo ndiyo maisha kama hayo, hasa hasa  katika siku zetu ikiwa kama nilivyo andika katika Gaudete et exsultate, na kidogo kila mtu, lakini hasa vijana, ambao wanajikuta katika kuchat mara kwa mara”. amebainisha Baba Mtakatifu. 

Ikikosekana hekima ya mang’amuzi kuna hatari ya kubadilishwa wenyewe na kuwa bidhaa

Baba Mtakatifu anaandika, ikiwa basi, inakosekana  hekima ya mang’amuzi, kuna hatari kubwa ya kubadilishwa, au hata ya kujibadilika wenyewe na kuwa kama bidhaa za tabia ya sasa. Kwa njia hiyo mang’amuzi kiukweli ni muhimu. Kwetu sisi sote. Wakati mwingine, kwa sababu ya huduma yao, makuhani wanahitaji hasa kufanya mang'amuzi hayo. Na ndiyo sababu aliona na kupongeza jitihada za Askofu wa Albano hasa katika kugusia mara kwa mara na makuhani pamoja na waseminari wa Jimbo. Hatimaye katika utangulizi wa kitabu  hicho, Baba Mtakatifu Francisko anasema, lengo la mafunzo ya makuhani na waseminari kwa hakika ikiwa ni yale ya mwanzo na ya kudumu ni kuwafanya kila mmoja awe imara,  mtu aweze kuwa na  mang’amuzi. Na katika kufanya mikutano na mapadre na waseminari ndipo nyaraka hizi tatu zimezaliwa na ambazo zimekusanywa kwa pamoja. Asili yake zilikuwa barua za kichungaji. Baba Mtakatifu anaamini kwmba kutangazwa kwa katika mtindo wa kitbu nyaraka hizi, zinaweza kuwasaidia hata mapadre na waseminari wengine ili kuendelea kuwa bora zaidi kama inavyo someka katika Hati ya hivi  karibuni ya Ratio Fundamentalis n. 43, kwa ajili ya mafunzo ya kikuhani, waamini wenye uwezo wa kutafsiri hali halisi ya maisha ya kibinadamu katika mwanga wa Roho, kwa maana ya  kutambua kuchagua, kuamua na kutenda kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu.

Mang’amuzi yatakiwa kuchagua na kuamua

Mchakato wa kufanya mang’amuzi unajikita katika matendo mawili muhimu ambayo yanakamilishana yaani kuchagua na kuamua. Ndivyo anavysisitiza Askofu Semeraro katika Kitabu chake, “kusikiliza na kutibu Moyo. Inahitaji kufanya uchaguzi kwa sababu mang’amuzi hayawezi kubaki katika kichwa tu, bali lazima yapitie katika mwili mzima. Aidha katika uchaguzi wa dhati, mwenendo, uhusiano na matendo ni vitu msingi ambavyo vinafuatia hatua ya kufanya maamuzi. Hautaweza kuingia katika hali halisi anasema Askofu,  iwapo hautakamilisha hatua  hizo za dhati kwamna  matokeo yake unaweza kujikata katika njia kipofu. Vile vile Askofu Semeraro ameonesha kuwa  kila uamuzi daima unahitaji hata majaribu ya dhati ili baadaye kuwa na uhakika wa ukweli! Kutokana na hilo  anasisitiza kuwa mchanganyiko wa mambo mawili ya kuchagua na kuamua ina maana  msingi wa kufanya mang’amuzi, ambayo ni mazoezi ya uhuru halisi wa kibinadamu na uwajibikaji binafsi.

Kwa mujibu wa Askofu Semeraro katika kitabu hiki anasema, lazima kuchagua wema iwezanavyo yaani ule ambao ni kwa ajili yangu leo hii. Hii ina maana ya kuchagua kwa hakika na hiyo ni kwa mara moja katika kujua nini cha kufanya leo hii,  ikiwa na maana ya kwenda sambamba na mapenzi ya Mungu.  Kwa  hakika hili ni jambo muhimu ikiwa tangu hatua ya kuamua na  kustahili kufanya mang’amuzi  inakuwa sahihi na kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu. Lakini hii ikiwa haina maana ya kucheza uwanja wa mchezo au kugundua na kutekeleza mpango iliyoanzishwa, bali ni kuwa na uhakika wa kile ambacho umefanya, umeng’amua na kuwa na uamuzi!

Kuhani ni mtu wa mang’amuzi iwapo anajitafiti mwenyewe katika mchakato huo

Katika kitabu cha Askofu Marcello Semeraro aidha ameandika: Kuhani kwa hakika ni mtu wa kufanya mang’amuzi na zaidi anapojitafiti mwenyewe katika mchakato huo na iwapo anabaki akiwa wazi na kuwa na uwezekano wa maisha yake yote. Anaye sindikiza wengine katika kufanya mang’amuzo, lazima awe mtu wa mang'amuzi,  maana hawezi kuhudumia saula la mang’amuzi ya wengine, hata kwa mtazamo wa hali halisi ya kibinadamu, au uwe mang’amuzi ya ishara za nyakati , iwapo bado hana hakomaa na manag'amuzi binafsi.

Kwa mujibu wa Askofu Semeraro ni kwamba mtu wa mang’amuzi ni lazima kimaadili awe na uwajibikaji wa kuongoza jumuiya, kuhani kwa maana hiyo lazima awe mhudumu wa mang’amuzi ya maisha yake mwenyewe ikiwa pia na ya wengine. Na hii ina maana Askofu Semeraro anasisitiza, kuwajibika katika maisha binafsi kwa mujibu wa  mapenzi ya Mungu, aliyetambuliwa wakati wa kufanya mang’amuzi ambayo ni mchakato ulio wazi. Katika maisha ya kiroho kwa makuhani, suala la mang’amuzi ni thamani hata ya kuweza kuondokana na uovu wa giza la ubaya ambao ni wivu, unaowakilisha ubaya ambao kila mtu anao. Dalili maalum ya uwepo wake katika maisha ya makuhani ni kuanza kuzungukia utupu, labda kupotelea katika elfu ya mambo ya kufanya kama kibendera na kuishi daima kila mahali, lakini kamwe haishi ndani mwake, badala kuishi mahalia ambamo Mungu anaishi.

Wivu ni tabia inayoendelea, ni mtego hata kwa makuhani

Askofu Semerano katika kitabu chake “Kusikiliza na kutibu moyo” anafafanuua kuwa wivu ni moja ya dhambi saba za mauti. Wivu kwa ujumla unamkumba mtu katika njia za ukuu wake, kuanzia  kimwili, kisaikolojia na kiroho. Wivu inafanana na hali fulani ya uvivu na hukosefu wa uvumilivu, lakini pia ukosefu wa ladha, chuki, uchovu hata roho mbaya ya uharibifu. Waandishi wa vitabu vya koroho, wanazungumzia hata juu usingizi, kwa maana kwamba, binadamu anapenda kulala na kusinzia bila hata ya kuchoka. Hii inatokana na kutoridhika na hali ya kawaida kwa ujumla. Na kwa maana hiyo mtu anayeinamia  na tamaa hii anapoteza ladha ya kila kitu. Katika mtego huu kila mtu anaweza kuanguka, ikiwa ni pamoja na makuhani. Suala la mchungaji aliye  na uchovu ni hatari halisi ambayo inapitia katika maisha ya kuhani leo hii. Kutokana na hiyo, Askofu Semeraro anakumbusha kuwa, hata kuhani lazima atunze na kuwa na makini na shauku yake. Kuhani siyo mwota ndoto, lakini anaacha afundishwe, wakati mwingine hata kujeruhiwa na ndoto za Mungu ambaye  hata kwa ugumu wa kupatana anamwita awe mshiriki wa mazoezi yake. Kwa mujibu wa askofu Semeraro, kuna tiba ya kutibu wivu ambayo inajikita hasa katika kujijali bila kuachia maisha yako yakumbwe katika bidhaa za wakati wetu yaani za kubaki katika mambo ya  marudio, kujali wingi wa marafiki katika Facebook, wafuasi kwenye Instagram na kueneza uvumi na masengenyo.

 

29 May 2019, 10:43