Tafuta

Jimbo Katoliki la Malakal nchini Sudan Kusini  limepata askofu mpya Padre Stephen Nyodho Ador MAJWOK Jimbo Katoliki la Malakal nchini Sudan Kusini limepata askofu mpya Padre Stephen Nyodho Ador MAJWOK  

Papa amemteua Padre Ador MAJWOK kuwa Askofu wa Malakal Sudan Kusini!

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu wa Jimbo la Malakal nchini Sudan Kusini mheshimiwa Padre Stephen Nyodho Ador MAJWOK,wa jimbo hilo,ambaye hadi uteuzi wake alikuwa ni katibu Mkuu wa Jimbo.Alizaliwa kunako tarehe 1 Januari 1973 katika kijiji cha Andong jimbo la Malakal na tarehe 15 Mei 2005 alipewa daraja Takatifu la upadre.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 23 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu wa Jimbo la Malakal nchini Sudan Kusini mheshimiwa Padre Stephen Nyodho Ador MAJWOK wa jimbo hilo na ambaye hadi uteuzi wake alikuwa ni katibu Mkuu wa Jimbo hilo. Padre Stephen Nyodho Ador MAJWOK alizaliwa kunako tarehe 1 Januari 1973 katika kijiji cha Andong jimbo la Malakal. Baada ya mafunzo ya elimu ya Msingi huko Adong na Thawrat Malakal (1982-1989), baadaye katika Taasisi ya Mtakatifu Lwanga (1990-1997). Aliendelea na mafunzo ya Falsafa katika Seminari Kuu ya Kitaifa ya Mtakatifu Paulo huko Khartoum tangu mwaka 1997 hadi 2000, baadaye Taalimungu tangu 2000 hadi 2005. Tarehe 15 Mei 2005 alipewa daraja Takatifu la upadre akiwa ni wa jimbo la Malakal.

Shughuli za kijimbo na masomo ya juu

Padre mteule Nyodho Ador MAJWOK baada ya kupewa daraja la upadre ameweza kujikita katika masomo  na shughuli mbalimbali ya kijimbo kama vile: 2005-2008:  Msaidizi paroko wa Kanisa kuu la Kristo Mfalme Malakal; 2008-2009: Paroko na Mkurugenzi wa kituo cha kichungaji Kijimbo; 2009-2013:  Paroko wa Kanisa Kuu na  Mratibu wa kozi ya kichungaji na msimamizi wa vijana , mjumbe wa baraza la ushauri la  kijimbo na mwanachama wa kundi la uwekezaji kijimbo.  2013-2016: Masomo ya taalimungu maadili Katika Chuo Kikuu cha Kipapa Uribaniano: 2016-2018: Masomo ya udaktari katika kitivo cha Taalimungu Maadili katika Chuo Kikuu cha Kipapa  Gregoriana na 2019, Katibu Mkuu wa Jimbo la Malakal.

23 May 2019, 15:56