Tafuta

Vatican News
Taasisi ya Kitaalimungu ya Yohane Paulo II ilipendekezwa na  Baba Mtakatifu Francisko na Motu Prorio yake “Summa familiae cura". Taasisi ya Kitaalimungu ya Yohane Paulo II ilipendekezwa na Baba Mtakatifu Francisko na Motu Prorio yake “Summa familiae cura". 

Ask.Mkuu Paglia:Mkutano wa Wataalam kuhusu familia katika Taasisi ya Yohane Paulo II

Utafiti kimataifa kuhusu familia umeanzishwa kutokana na dharura ambayo inaoneshwa wazi na Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake wa Kitume wa Amoris Laetitia kwa kutazama familia zote duniani katika maisha yao halisi.Ndiyo lengo la Mkutano wa Wataalam kimataifa uliozinduliwa tarehe 13-15 Mei 2019 katika Taasisi ya Kitaalimungu Yohane Paulo II,Roma.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 13 Mei 2019, umezinduliwa mkutano wa wataalam ikiwa ni hatua ya kwanza ya kisayansi  ya watafiti kimataifa kuhusu familia. Mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Kitaalimungu ya Yohane Paulo II kwa ajili ya Sayansi ya Ndoa na Familia kwa kushirikiana na  Chuo Kikuu Katoliki cha Murcia na Cisf ya Milano Italia. Aliyezindua Mkutano huo wa Wataalam  ni  Askofu Mkuu Vincenzo Paglia Kansela wa Taasisi hiyo na ambapo amesema kuwa, shughuli ya utafiti huo ilianzishwa kunako Desemba 2018 kwa lengo la kuendeleza utafiti wa kisayansi kwa ngazi ya kimataifa juu ya hali halisi za familia katika mantiki zake zote yaani kijamii, kiutamaduni na kiuchumi.

Utafiti wa wataalam kuhusu familia utafanywa kwa miaka mitatu 2019-2021

Askofu Mkuu Paglia akifafanua zaidi kuhusu sababu ya mkutano huo (expert meeting) amesema, utafiti huo utafanywa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2019-2021 na ambapo utajikita kwa kina katika kutoa ripoti mbili juu ya familia na uhusiano wa umasikini, familia na umasikini kiuchumi, ambayo ni miongozo msingi itakayoongoza utafiti wote  kuhusu mada hiyo.  Uchunguzi kimataifa kuhusu familia umeanzishwa kutokana na dharura ambayo imeoneshwa wazi na Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wa kitume wa Amoris Laetitia, katika kutazama familia zote duniani hasa maisha yao halisi, amesisitiza Askofu Mkuu Paglia. Aidha amasema "kazi hiyo ya utafiti ambao leo hii tunaiishi pamoja ni hatua msingi hata ndani ya upyaisho wa Taasisi ya Kitaalimungu ya Yohane Paulo II iliyopendekezwa na Baba Mtakatifu Francisko na Motu Prorio yake  “Summa familiae cura” amethibitisha Askofu Mkuu Paglia.

Vigezo msingi alivyotoa Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mkutano wa hivi karibuni jimbo Kuu Roma

Askofu Mkuu akiendelea kufafanua zaidi amesisitizia hata baadhi ya vigezo ambavyo Baba Mtakatifu Francisko amevionesha  wakati wa Mkutano wa Jimbo la Roma hivi karibuni. Awali ya yote kuwa na “mtazamo wa kutafakari juu ya maisha ya watu wanaoishi katika mji”. Kuchunguzwa kwa makini dunia ya maisha na ili kuweza kupokea historia ya maisha ambayo inasaidia akili zetu ziweze kweli  kupokea hali halisi na  ukarimu wa hekima yetu ya Imani". Kwa maana hiyo Askofu Mkuu Paglia amesema: hayo ndiyo matarajio, ambayo wanatarajiawataalam  kuanza hatua hizo. Pili hata katika maelekezo ambayo yaonesha  ulazima wa kuhesabu “tamaduni mpya ambazo zinazaliwa katika mji” kwa mujibu wa Baba Mtakatifu Francisko. "Tamaduni hizi mpya hazijiwakilishi kuwa na ulazima wa kutengeneza nadharia inayoelezeka  na mpango uliokamilika, badala yake zinapaswa kutambuliwa katika mienendo halisi, katika mabadiliko yanayo tokea hata  kama ni madhara yatokanayo na miji ya jumuiya", amesema Askofu mkuu.

Washiriki wa mkutano huo waudhuria katekesi ya Baba Mtakatifu Siku ya Kimataifa ya Familia

Katika kazi hiyo na ya utambuzi, kwa mujibu wa Askofu Mkuu Paglia anathibitisha kwamba ndiyo kwa hakika watatifi  watafanya ikiwa ni kama mpango wao ambao wana utengeneza na ambao unaonesha kuwa mwafaka. Na akihitimisha amekumbusha kuwa Mwezi mmoja uliopita Baba Mtakatifu Francisko katika Karatasi aliyomwakilishia mapendekezo ya kuanzishwa kwa Utafiti huo wa familia, yeye binafsi aliandika kwa mkono wake na kutoa Baraka. Karatasi hiyo inahifadhiwa vizuri na wametiwa moyo  kwa mtazamo wa familia yote duniani hasa wale ambao ni maskini na ukosefu wa rasilimali na kwa hakika leo hii ni kazi kubwa yenye ugumu wake amesema. Washiriki wa Mkutano wa "wataalam" watashiriki Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 15 Mei 2019 katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya Familia inayo adhimisha kila ifikapo tarehe 15 ya kila mwaka. Siku hii ilianzishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kunako 1989 na kumbe mwaka huu ni mwaka wa 20 tangu kuanzishwa kwa siku hii.

14 May 2019, 10:36