Wosia wa "Laudato Si" wa Baba Mtakatifu Francisko umefikisha miaka 4 tangu kutangazwa kwake 2015 Wosia wa "Laudato Si" wa Baba Mtakatifu Francisko umefikisha miaka 4 tangu kutangazwa kwake 2015 

Wosia wa Laudato Si' umefikisha miaka 4:Ni lazima kujibu kipeo cha mabadiliko ya tabianchi!

Tarehe 24 Mei 2019 umetolewa ujumbe kutoka Baraza la Kipapa la maendeleo fungamani ya watu katika fursa ya mwaka wa 4 tangu kutangazwa kwa Wosia wa Baba Mtakatifu Francisko wa Laudato Si'.Wanasayanasi wanatoa taadhari ya kuchukua hatua ya kutunza nyumba yetu ya pamoja ambayo imegawanyika vipande vipande;inasaidia kutoa wito wa nguvu kwa kizazi cha vijana kinachotishiwa maisha yao endelevu!

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ujumbe wa  Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya kibanadamu, umeandikwa kwa ajili ya Jumuiya ya Kisayansi katika fursa ya kutimiza mwaka 4 tangu kutangazwa kwa Wosia wa Laudato Si' wa Baba Mtakatifu Francisko ukihamasisha “kujibu kipeo kinacho sababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Katika ujumbe huo, unaonesha kwamba, siku chache zilizo piata Baba Mtakatifu alikutana na baadhi ya wasayansi wakiongozwa na mtabili wa hali ya hewa kutoka nchini Ufarasa Jean Jouzel, na mjumbe wa muda mrefu katika Jopo la Serikali za Mitaa juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa (IPCC). Akiwa nao Baba Mtakatifu Francisko ameweza kushirikisha kwa kina wasiwasi mkubwa wa wataalam wa kisayansi katika kambi inayotazama kipeo cha sasa kuhusu tabianchi hasa kilicho sababishwa na mtu kuingilia kati  asili ya mazingira. 

Ujumbe huo unathibtisha kuwa, kunako mwaka 2015 ulitangazwa Wosia wa Laudato Si' kwa kuonesha bayana wasiwasi  wa nyufa za sayari tumoishi (LS 163)  na kuwa na matarajio ya kuingia katika majadiliano na kila mtu kuhusu nyumba yetu ya pamoja (Ls 3).  Ujumbe huo unasisitiza kuwa, kwa kutangazwa kwa wosia huo ulikuwa unataka kutia moyo juhudi za kazi ya Wakuu wa nchi COP 21, ambao wangeweza kufikia Mkataba wa kihistoria wa Paris kuhusu tabianchi, kwa lengo la kudumisha joto la wastani katika uso wa sayari hasa  chini ya nyuzi 2 ° na kuimarisha juhudi hata za kupunguza joto kufikia hata kikomo cha nyuzi  1.5 °.  Ripoti maalum ya  IPCC 2018, yaani  Jopo la Serikali za Mitaa juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa  kuhusu mantiki  hiyo na uwezekano wa kuweka kikomo cha nyuzi  1.5 ° , ulionya kuwa, "tuna karibu miaka kumi tu ya kuweza kusimamisha na kupunguza joto hili la kimataifa.

Kiwango cha nyuzi 1.5 ° ni kiwango pia cha kimwili na kikubwa kwani bado kinaweza kuepusha athari nyingi za uharibifu za mabadiliko ya tabia nchi, zilizosababishwa na binadamu kama vile kuyeyuka kwa barafu na  uharibifu wa miamba ya matumbawe ya kitropiki. Na zaidi hasa ambayo ingeweza kulinda nyumba yetu ya pamoja badala ya kuigezea kuwa chafu! Pamoja na joto la dunia  karibu  la nyuzi 1 ° iliyothibitishwa tangu mapinduzi ya viwanda, ni kutazama sasa  na kuona athari kubwa za mabadiliko ya hali ya hewa kwa watu, kwa maana kuna hali  mbaya ya mabadiliko ya tabianchi, kama vile ukame, mafuriko, kupanda kwa usawa wa bahari, dhoruba kali, vimbuka , matetemeko ya ardhi na moto mkali. Mgogoro wa hali ya hewa unafikia idadi isiyokuwa ya kawaida. Kwa maana hiyo ni dharura kukabiliana na kipeo hicho katika kutoa jibu linalo stahili.

Kiwango cha nyuzi 1.5 ° pia ni kizingiti cha maadili. Ujumbe unaendelea kuonesha kuwa hii ni fursa ya mwisho ya kuokoa nchi zote hizo na mamilioni ya watu wanaoishi katika mazingira magumu katika kanda za pwani. Hawa ni maskini wanaolipa gharama kubwa zaidi ya mabadiliko ya tabiachi.  Hii ikiwa ni uzoefu wa maisha ya kawaida lakini hata katika utafiti wa kisayansi unaonyesha kwamba, matokeo yote na madhara makubwa ya vurugu za mazingira yanawakumba zaidi masikini (Ls 48). Kwa maana hiyo tunapaswa kujibu kwa ujasiri kilio cha huzuni daima wa dunia hii na masikini wake.

Aidha ni ujumbe huo unaendelea kwamba:ni vizuri kuzingatia kwamba nyuzi 1.5 ° ni mantiki ya kidini. Dunia tunayoharibu ni zawadi ya Mungu kwa wanadamu, hasa nyumba hiyo iliyotakaswa na Roho ya Mungu (Ruah) tangu mwanzo wa uumbaji, mahali ambapo Mungu alisimika hema lake katikati yetu (tazama Yh 1,14). Kama alivyoandika Baba MtakatifuMstaafu Benedikto XVI kwamba: “Dunia siyo hali halisi  ambayo itumiwe kulingana na kiumbe binadamu anavyotaka yeye, bali ni kazi ya  uumbaji wa Mungu! Kwa mwaka wa 2001, Maaskofu wa Marekani walikazia kuwa, “ikiwa tunaleta madhara ya hali ya mazingira, tunadharau pia Muumba wetu na zawadi ya uumbaji”. Ni ukweli wa kina kujifunza hasa kutoka kwa ndugu kaka na dada wa asilia. Kwa upande wao wanafikiri kwamba, dunia siyo nzuri kwa sababu ya ustawi wa kiuchumi, bali ni zawadi ya Mungu na ya mababu wanaopumzika ndani yake, katika nafasi takatifu ambayo wanahitaji kushirikishana na ili kudumisha na kuendeleza utambulisho wao, thamani yao na  maadili yao "(Ls 146).

Wito wa taadhari kutoka kwa wanasayansi hasa wakihimiza  kuchukua hatua ili kutunza nyumba yetu ya pamoja ambayo inagawanyika vipande vipande pia inasaidia kutoa wito wa nguvu inayotoka kwa kizazi cha sasa cha  vijana, ambacho kinatishiwa  maisha yao ya baadaye. Vijana wanataka mabadiliko kutoka kwetu (Ls 13) na kuna harakati ya vyama vya wanafunzi ambavyo wamekuwa na mwamko mkuu ulimwenguni kote. Katika Siku ya Vijana ya Dunia huko Panama, mwaka huu, vijana walizindua mkakati uitwao: “Kizazi cha  Laudato Si" na kuoneshwa kwa nguvu zaidi ambayo inachangamotisha jumuiya ya imani na mashirika ya kiraia hasa kujikita katika mzizi wa uongofu mkubwa wa mazingira na zaidi kwa matendo ya dhati. Vijana wanaomba hutekelezwaji wa mabadiliko ya haraka, hasa katika  vyanzo vya nishati mbadala kulingana na Mkataba wa Paris na kukomesha zile nyakati za  uchimbaji wa mafuta baharini, kwa kukumbusha  wito wa Maaskofu kutoka duniani kote.

Katika miezi ya hivi karibuni, vijana wamezidi kuwa wazi, kama inavyoonekana, kwa mfano, katika mgomo wa mazingira. Kuchanganyikiwa na hasira kwa kizazi chetu ni dhahiri unasema hujumbe huo. Tunahusika na kuhatarisha kuwaibia wakati wao endelevu ikiwa pia ni kuwaachia kizazi kijacho magofu mengi ,  jangwa na uchafu (Ls 161). Ni wakati wa kujiandaa ili kuingilia kati. Kama inavyoelezwa katika Laudato Si ', katika kupunguza uharibifu wa kutofautiana kwa sasa kulingana na kile tunachofanya sasa” (Ls 161). Sisi sote tunapaswa kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yetu, matumizi ya nishati, matumizi, usafiri, uzalishaji wa viwanda, ujenzi, kilimo, nk. Kila mmoja wetu anaitwa kutenda kwa dhati. Lakini pia tunapaswa kuchukua hatua ya pamoja, kuanzia na serikali na taasisi, familia na watu. Tunahitaji mikono yote tuliyo nayo, unasisitiza ujumbe. Tunahitaji talanta na ushirikishwaji wa wote (Ls 14) ili kukabiliana na mgogoro huu na kushinda maslahi yenye nguvu ambayo yanazuia majibu yetu muhimu ya pamoja kwa tishio hili lisilo la kawaida dhidi ya ustaarabu wetu.

Ni vyema kuungana na wanasayansi na vijana katika kuhamasisha familia yetu ya kibinadamu, hasa wale walio katika nafasi za mamlaka ya  kisiasa na kiuchumi, kuchukua  hatua kubwa za kubadilisha. Tunapaswa kufikiria ulimwengu mmoja, mpango wa pamoja (Ls 164). Tunahitaji kutoa wito kwa  viongozi wa kisiasa ili wawe jasiri zaidi na kusikiliza kilio kikubwa kilichotabiliwa na Jumuiya  ya kisayansi na harakati za vijana kuhusiana na hali ya hewa. Serikali zina wajibu wa kuheshimu ahadi walizojiwekea mwaka 2015. Viongozi wakuu wa Umoja wa Mataifa watakaohudhuria Mkutano kuhusu Hali ya Hewa mwezi Septemba 2019 ni lazima wawe na mipango imara ya kitaifa ya utekelezaji wa Mkataba wa Paris, hasa nchi zenye nguvu zaidi na  zilizochafuka (Ls 169). Ili kukabiliana na mgogoro huu wa kutisha wa hali ya hewa, tunahitaji kuhamasisha utashi na uamuzi, pamoja na rasilimali za kiuchumi kwa kiwango kikubwa.  Hiyo ilifanyika wakati wa fursa ya mgogoro wa kifedha wa mwaka 2007-2008 ili kuokoa mabenki na sasa je haiwezekani kufanya hivyo sasa  ili kuokoa nyumba yetu ya pamoja, siku zijazo za watoto wetu na vizazi vijavyo?

Na hatimaye ujumbe huo unahitimishwa ukisisitiza kuwa: bado kuna matumaini, tumaini kubwa, bado kuna wakati wa kujikita katika  matendo na kuepuka athari mbaya zaidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Binadamu, wenye uwezo wa kujiharibuwenyewe,  hadi mwisho wanaweza pia kushinda wenyewe, kurudi kuchagua mema na kujitengeneza wenyewe (Ls 205). Lazima tupyaishe rasilimali bora za asili yetu ya kibinadamu, sifa nzuri za upendo, huruma, ukarimu na shauku. Rasilimali kubwa zaidi ya mwanadamu ni ile ya utambuzi kwamba Bwana Mungu  wa uzima hamwachi binadamu na hamwachi mtu peke yake, kwa sababu ameungana kabisa na yeye na kwa dunia nzima na upendo wake daima unaongoza kutafuta njia mpya ( Ls 245).

28 May 2019, 14:46