Tafuta

Vatican News
Kardinali Filoni akiwa nchini Thailand katika maadhimisho ya miaka 350 ya kuanzishwa kwa umisionari nchini humo Kardinali Filoni akiwa nchini Thailand katika maadhimisho ya miaka 350 ya kuanzishwa kwa umisionari nchini humo 

Kard.Filoni:Miaka 350 ya Kanisa la Thailand ni kipindi cha shukrani

Katika maadhimisho ni matokeo chanya ya miaka 350 ya kazi ya uinjilishaji katika taifa la Thailand.Katika sikukuu hiyo ni furaha na kwa maana nyingine ni kipindi cha jitihada ya kuwa wafuasi wa kimisionari. Hayo yamesisitizwa katika mahubiri ya Kardinali Fernando Filoni Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu tarehe 18 Mei 2019 huko Sampran (Bangkok).

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kardinali Ferdinando Filoni Rais wa Baraza la Kipapa la unjilishaji wa watu akiwa Thailand katika maadhismisho ya Miaka 350 ya kuanzishwa kwa Kanisa nchini humo amesema tukio hili ni kipindi cha neema. Katika maadhimisho hayo ni matokeo chanya ya miaka 350 ya kazi ya uinjilishaji katika taifa hilo. Katika sikukuu hiyo ni furaha ya  maadhimisho kwa maana nyingine ni kipindi cha jitihada ya kuwa wafuasi wa kimisionari. Amesisitiza hayo katika mahubiri yake tarehe 18 Mei 2019 huko Sampran (Bangkok), ikiwa ni mwaka wa 350 kwa Kanisa la Kitume huko Siam na ndiyo ulikuwa mwanzo wa Kanisa mahalia la Thailand

Kanisa linakua

Kardinali Filoni amekumbusha kuwa Makao ya kitume huko Siam yalizinduliwa kunako mwaka 1669 na kupitia vipindi hatua mbalimbali za maisha yake. Leo hii kuna majimbo katoliki 11 nchini Thailand, ambayo ni ishara ya kukua kwa Kanisa. Amekumbuka kwa shukrani jitihada za unjilishaji ulioanzisha na wamisionari wa Utume wa Nje kutoka Paris (MEP). Baada ya hawa walifuata wamisionari wengine wa kike na kiume kutoka katika taasisi nyingine. Wakiwa na shauku ya kitume hawa walijikita katika shughuli ya kupanua kanisa hili katika taifa kubwa.

Kuendeleza shughuli za uinjilishaji

Akiendelea na tafakari yake, Kardinali Filoni amewaalika kuishi tukio hili kwa moyo wa shukrani kwa Mungu na kupyaisha jitihada kwa ajili ya wakati endelevu kwani anasema shughuli za uinjilishaji hai wa wamisionari lazima uendelee. Shughuli ya kupeleka Injili na wokovu kwa watu wote iliyoanzishwa na Yesu na kukabidhiwa Kanisa, bado ni kubwa na liko mbali kufikia ukamilifu wake. Kwa mtazamo huo, ni kuonesha kuwa utume bado huko mwanzo kabisa na hivyo wote lazima kujitahidi kwa moyo wote kwa ajili ya utume wa uinjilishaji.

Kuunganika na Yesu

Akitafakari katika masomo ya Biblia yaliyokuwa yamesomwa, Kardinali Filoni amesisitiza: katika Injili ya Yesu mfufuka anaalika kubaki naye na ndipo wanaweza kuzaa matunda mengi na mema.  Kubaki ndani mwake maana yake ni kungana na Yesu. Ni kuwa na urafiki wa kina na Kristo. Wote tunaalikwa kuwa marafiki wa Yesu na zaidi kuwa washiriki. Kama wakristo wabatizwa, sisi sote ni washiriki katika Yesu. Ushiriki huo una maana ya kushirikishana na kushiriki utume wa Yesu. Sisi sote tunaalikwa kwa namna hiyo kutangaza Injili na kuishuhudia.

Mfano wa  padre Nitbamrung   

Aidha amesema maadhimisho hayo ni mwaliko kwa wote kubaki na muungano na Yesu kama walivyo fanya mitume wake. Na ili kuweza kufanya zoezi la kutangaza Injili, lazima kuwa karibu na Yesu. Ni lazima kukua katika familia ya Yesu. Ni lazima mmoja kugeukwa kuwa rafiki wa kweli wa Yesu. Na hatimaye ni lazima kugeuka kuwa wafuasi wa Kristo. Kuna haja kubwa ya kazi ya kuinjilisha katika taifa hilo amesema. Katika mantiki kubwa ya dunia na tamaduni za kiroho, kazi ya ushuhuda wao wa kikristo unaweza kutoa mchango mkubwa wa uelewa wa imani ya kikristo. Kila mbatizwa anao uwajibu na kwa maana hiyo, wanaweza kufanya kama alivyofanya  Padre Nicholas Bunkerd Nitbamrung, aliyetengazwa kuwa mwenyeheri kunako mwaka 2000. Padre Nicolas (1895-1944), wa Thailand alifungwa jela kwa tuhuma za kuwa mpelelezi wakati yeye katika maisha yake yote alikuwa anajikita kutumikia Kristo na kutangaza Injili.

Kushuhudia umoja

Kardinali Filoni aidha amekumbuka Mkutano Mkuu wa Kanisa la Thailand kunako mwaka 2015 uliokuwa unaongozwa na kauli mbiu “wafuasi wa Kristo walio hai katika uinjilishaji mpya” na kuwambia kwamba: “ ninyi mnaitwa kuonesha ushuhudwa wa umoja wa wafuasi ambao wanamtazama Yesu ili wakristo wote waweze kuwa chumvi na ambao wanaangazwa  na mwanga wa kweli wa Kristo, mwanga wa Mungu ambaye ni upendo na alio utoa katika dunia”. Hatimaye Kardinali Filoni amewatia moyo wote wawe wafuasi wa kimisionari: “katika mantiki ya Thailand anasema inajitaji uhusishwaji wa watu wote wenye mapenzi mema kwa maana bado kuna nafasi kubwa ya uinjilshai katika nchi yenye kupendwa” amesisitiza.

21 May 2019, 13:05