Tafuta

Kuelimisha kwa ajili ya amani katika dunia ya dini nyingi:mtazamo wa kikristo ni kauli mbiu ya Hati ya pamoja na Baraza la Kipapa la mazungumzo ya kidini na Baraza la Kiekumene la Makanisa duniani Kuelimisha kwa ajili ya amani katika dunia ya dini nyingi:mtazamo wa kikristo ni kauli mbiu ya Hati ya pamoja na Baraza la Kipapa la mazungumzo ya kidini na Baraza la Kiekumene la Makanisa duniani 

Kuelimisha amani katika mtazamo wa amani kikristo

Kuelimisha kwa ajili ya amani katika dunia ya dini nyingi:mtazamo wa kikristo, ndiyo kauli mbiu ya Hati ya pamoja na Baraza la Kipapa la mazungumzo ya kidini (Pcid) na Baraza la Kiekumene la Makanisa (Cec) iliyotangazwa mchana jijini Geneva tarehe 21 Mei 2019

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kutia moyo Makanisa na mashirika ya kikristo katika kutafakari juu ya mzizi ambayo imesababisha kuyumba kwa amani  duniani na ili hatimaye kuweza kuimarisha kwa kiasi kikubwa mijadala na kuwahusisha wafuasi wa dini nyingine kama vile wadau wa kijamii na kisiasa. Ndiyo maelezo yaliyomo katika utangulizi wa lengo la Hati ya pamoja na Baraza la Kipapa la mazungumzo ya kidini (Pcid) na Baraza la Kiekumene la Makanisa duniani (Cec)  inayoongozwa na kauli mbiu: “Kuelimisha kwa ajili ya amani katika dunia ya dini nyingi:mtazamo wa kikristo”, iliyotangazwa huko Geneva mchana tarehe 21 Mei 2019. Kwa mujibu wa waliotia sahini, wanathibitisha kuwa ni muhimu katika jitihada  za kila mara ili kuweza kukuza uhusiano wa kiekumene kwa njia ya kuhamasisha mazungumzo ya kidini.

Hati iliwakilishwa katika mkutano ulio ongozwa na mada:kuhamasisha amani pamoja

Hati hiyo imewakilishwa katika mkutano ulioandaliwa kwa kungozwa na tema ya “ kuhamasisha amani pamoja”.  Mara baada ya tamasha vyombo vya muziki wa kiroho na kuashwa kwa mishumaa kwa upande wa viongozi wa tamaduni nyingi za imani; baadaye  Askofu Miguel Ángel Ayuso Guixot, Katibu wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini na Katibu Mkuu wa Baraza la Kiekumene la Makanisa ulimwenguni, Olav Fykse Tveit, walitoa hotuba zao zilizofuatiwa na salam kutoka kwa Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa, Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, na taasisi maalum mjini Geneva na wawakilishi wa Utume wa kudumu katika nchi za Uarabuni, Aalya Al Shehhi.V. Katika mkutano huo umewakilishwa na vipindi viwili vya kutafakari kwa kina juu ya Hati ya kihistoria ya Udugu wa kibinadamu kwa ajili ya amani duniani na kuishi kwa pamoja, iliyotiwa sahini na Baba Mtakatifu Pamoja na Imam Mkuu  wa Al Azhar huko Abu Dhabi, tarehe 4 Februari 2019. Na kwa upande wa Kanisa Katoliki Katibu wa Pcid, monsinyo  Indunil Kodithuwakku aliweza kutoa tangazo la hati hiyo wakati wa Mkutano.

Ugaidi, mashambulizi ya nguvu dhidi ya  dini, misimamo mikali na itikadi au kujithibitisha kwa njia ya mitandao ya kijamii

Katika uwakilishi wa hotuba yake kwa ufupi, Askofu Ayuso amesema: tunishi katika dunia iliyogawanyikana kwa maana hiyo watu wanazidi kuongezeka. Zaidi ya kipeo cha kiekolojia, ukosefu wa msimamo wa kisiasa, uchumi na kijamii unaoendelea kuhatarisha ustawi wa maisha katika sayari. Ugaidi, mashambulizi ya nguvu dhidi ya  dini, misimamo mikali na itikadi au kujithibitisha kwa njia ya mitandao ya kijamii, uchochezi wa chuki, kama vile mahubiri ya ulaghai, baadhi ya  taasisi za kidini ambazo zinapanda vurugu na katika mitandao ya kijamii ni masuala ambayo ni lazima kuyavalia njuga. Kutokana na hiyo Askofu ameelezea kuwa hati hiyo inajikita juu ya utambuzi wa kushirikishana na ambao elimu ina nafasi kubwa na hai na zaidi inaweza kusaidia kutatua migogoro, kuingilia kati na kuzuia kurudiwa tena, kuponyesha majeraha, kuimarisha haki na kusaidia hadhi ya usawa wa wote.Aidha Askofu Ayuso amesema, Hati ya pamoja imeandikwa na wakristo na ndiyo kwanza inawalenga wakristo wenyewe na inathibitisha kuwa ujenzi wa amani lazima ujihusishe kwa watu wote.

Hati imeundwa  katika sehemu tatu: sehemu ya kwanza inaonesha sababu saba

Hati hiyo inaundwa na sehemu tatu. Katika sehemu ya kwanza inaonesha sababu saba ambazo wakristo wanaalikwa kujibidisha katika elimu ya amani. Kristo ni amani yetu (Ef 2,14; kama walengwa wa zawadi ya amani ya Kristo, wanafunzi wake wanaitwa kuwa wahunzi wa wamani; wao wanapaswa wahusishwe na haki; kuhudumia na tathmini ya elimu ni muhimu kwa utamaduni na mazozi ya kikristo, ambayo yanapaswa kuwa na maana kubwa kwao kwa njia ya hekima ya kibiblia; amani, inaeleka kama marejesho ya mahusiano ya haki, huleta uhusiano  msingi na wa kina kati ya dhambi, msamaha na upatanisho;  mchakato wa amani unahusisha kuzingatia mambo yote yaliyopita na endelevu; Imani ya Kikristo katika utatu wa Mungu mmoja inafundisha kwamba watu wa Mungu ni wakweli na bado wamefungamana kati yao.

Sehemu ya pili: maendeleo, mikakati ya kudumisha amani kwa njia ya elimu

Sehemu ya  pili kwa upande wa Hati hiyo inawakilisha maendeleo mengi na mkakati kwa ajili ya kukukamilisha muundo wa amani kwa njia ya elimu ambayo inaunganisha rika zote na sekta zote za kijamii, baadhi yao ni kama vile zile  maalum zinazo tazama watoto, nyingine kwa ajili ya vijana na nyingine kwa ajili ya watu wazima. Miongoni mwao hizo kuna  haki ya elimu inayofaa, elimu kwa jumla, elimu inayohusu wanadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu, mfano wa Yesu kama mwalimu; mafunzo ya kudumu kwa wote; amani na nguvu; kujua, kulinda na kuthibitisha, nyingine ni  matumizi ya vyombo vya habari katika elimu ya amani; kujifunza kutoka katika  Maandiko; ibada, tasaufi na elimu kwa ajili ya amani; kuzuia na upatanisho; kushirikisha  na matarajio ya maendeleo na ekolojia.

Sehemu ya tatu inatoa angalisho kwa mambo kumi ya kutafakari

Hatimaye, sehemu ya tatu inatoa mapendekezo kumi ya kutafakari kwa makini kwenye makanisa, taasisi za elimu za Kikristo na mihimili ya kidini,  kitaifa na ya kikanda: Kujifunza Hati na kuutafakari juu ya nini kinaweza kuwa mbinu bora za elimu zinazohusiana na amani; kuendeleza rasilimali za elimu na kozi ya kujifunza; kuongeza nguvu na kuendeleza ubunifu, zana za elimu, zinazomhusu mwanafunzi kwa ngazi mbalimbali (kutoka katika familia hadi katika jumuiya  kidini, kutoka taasisi za elimu kufikia  jamii kwa ujumla); kuchunguza na  kuchangamotisha dhana zilizopita na za sasa ambazo zimechangia kukuza vurugu; kutia moyo na kuhimiza taasisi za elimu za kikristo na mashirika ya kanisa, hususan wale ambao hutoa mitaala ya katekesi  kwa ajili ya watoto na vijana, kuanzisha vipengele vya elimu kwa ajili ya amani katika malezi ya kiroho na ya kibinadamu; kuthibitisha kama ni vipengele vya maisha ya kidini, ikiwa ni pamoja na uelewa  wa maandiko, ibada ya umma, sala na liturujia vinaweza kukuza ushirikiano wa kibinadamu katika jamii ya haki zaidi na amani.

Kuhakikisha taasisi za kikristo zina soma hati ya ushuhuda wa kikristo iliyotolewa 2011

Aidha katika Hati hiyo inaonesha ulazima wa  kuhakikisha kwamba taasisi za Kikristo duniani kote zinasoma kwa njia ya maombi  hati ya (Christian Witness in a Multi-Religious World: Recommendations for Conduct (2011)… Ushuhuda wa Kikristo katika dini nyingi:Mapendekezo ya Maadili ulitolewa 2011), ili kuweza kuondokana na migogoro inayohusiana na uelewa mbaya wa utume; uongofu na upropaganda; Kukumbuka historia za maisha ya watu maalum ambao walikabiliana kwa namna ya pekee ya kiekumena na kidini masuala ya kidini, masuala ya haki, amani na ekolojia; kuhimiza serikali ili kuendeleza mifano ya elimu ambayo inalenga kuhamasisha na kukutana na wakati huo huo kutoa kipaumbele cha amani; na kusali pamoja kwa ajili ya amani.

22 May 2019, 15:13